Salamu kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Passport za Tanzania zinakimbilia mikononi mwa wageni kupitia viongozi waandamizi na askari

watanzania wengi tuna tamaa kupitiliza, tuko tayari kuuza hata nchi ili tu upate hela ukafanyie uzinzi na kunywea pombe....

Waarabu, wahindi, wasomali hawa wengi wanauraia wa nchi mbili na uraia wa tanzania ni kichaka chao cha uzawa na kutupigia hapa kama watanzania...

Sasa hivi kuna wimbi la nigerians, senegalise, waganda, wanyarwanda kuwa na passport ya Tanzania kwa ajili ya mambo yao..
 
Shamba la bibi ndio huwa hivyo.
 
Mzalendo halisi
 
Nchi hii inafurahisha. Unaenda NIDA, unashtuliwa inabidi uwe na kiapo cha mzazi unalipa 12000 wanakupa kiapo cha mzazi wakati hata hayupo hawajawahi kumuona.
Kuna mtu nilipomwambia naenda kufuatilia kitambulisho, akasema usijisumbue we toa jina lako kamili utalewa tu nikabaki eh.
Yani nchi hii ipo ipo tu.
Na ukiwa mzawa ukafuata utaratibu wanakuzungusha sana ili mradi wapate rushwa.
Nilienda NiDA nikawapa kila kitu kuanzia cheti cha primary, cheti cha kuzaliwa, namba ya nida ya baba na ma, cheti cha sekondari, copy ya kitambulisho cha kupiga kura lakini bado wakataka nizingue, mpaka eti jamaa alipogundua tumatoka kabila moja. 🤣🤣
 
Mandela aliitwa gaidi kama ISIS wanavyoitwa magaidi leo. Nyerere alivyompa paspoti yule aliyejulikana kama gaidi mbona mlifyata hamkupiga kelele? Wakipewa Waarabu na Waislamu ndiyo mnaanza kupiga kelele. Halafu travel ban ya Trump ambayo unataka kuitumia kama kisingizio mbona imeisha sasa kelele za nini?
 
Tz ina chagamoto kubwa zenye athari moja kwa moja kwa mtu wa hari ya chini kama mkulima machinga mama tilie kuliko hi ya wa arabu na Wahidi kupewa passport, na hili limetokea kwa sabb raia wa kawaida wame wekewa masharti magumu kupewa passport na hawana pesa hiyo 200,000 ni nyingi, wale wa hindi wa somali na wa arabu wengi hawana shida ya kukaa hapa wa natumia Tz kama gateway to Europe America baada ya pass zao za nchi zao kua rejected na hizò nchi za ulaya ,......usijindaganye kwamba huu mchezo haujulikani na top leaders ata waziri wa mambo ya ndani anaujua vizri na ni chazo cha mapato, hauna athari kwa raia wa kawaida ni faida kwa viongozi na serikali kupata mapato,.....wivu na ignorance ndo shida kwetu tulioshindwa maisha, mgejua watanzania hapa jneburg wanao miliki pass za [emoji1221] bila kufuata masharti. Wa Tznia wanao ishi Kenya na pass za kenya ndo usiseme, sema tu nchi nyingi kuchukulia wa tz kama under dogs sio tishio kiuchumi kwasabb ya kukosa mitaji na elimu, neenda Rwanda utakutana na Wtanzania kibao na pass za uko, DRC wengi wapo na pass za congo uganda ndo basi shamba la bibi.
 
naona unasumbuliwa sana na udini na hivyo kupotoka na kuamini kuwa magaidi wote wa ISIS wanaotumia dini ya kiisalamu ni kama "wagombea uhuru dhidi ya marekani" bila hata kujua kuwa ISIS imeua waislamu wengi sana kuliko wamarekani hao. Mandela hakuwa anagombea uhuru kama Mkiristo bali alikuwa ni mgombea uhuru wa watu wote wa afrika ya kusini dhidi ya utawala haramu wa makaburu; katika wafuaisi wake kulikuwa na dini zote. na wala Alipopata hifadhi ya Tanzanai hakupewa kwa sababu ya dini yake. Na unapotumia statement ya generalization kwamba "...mlifyata na hamkupiga kelele" ni dalili za ukosefu wa busara na upungufu wa mkubwa wa uwezo wa kuwasiliana. Umachukulia sehemu ndogo sana ya mjadala na kuifanya swala la dini.

Issue iliyoko hapa ni udhidbi wa passport za Tanzania; kuwepo au kutokuwepo kwa travel ban siyo sehemu ya mada kabisa. Hii inarudi tena kama niliposema ni matokeo ya ukosefu wa busara na upungufu mkubwa wa uwezo wa kuwasiliana.
 
Wewe ndiyo unasumbuliwa na ubaguzi na udini. Unajua walichofanya Mandela na MK wenzake kule Afrika Kusini wangekifanya Marekani au Ulaya wangekamatwa wangenyongwa kabisa na siyo kufungwa tuu? Lakini walivyopewa paspoti za Tanzania na Nyerere wala hamkupiga kelele na mpaka leo mnajivunia kuwapa paspoti za Tanzania kwenda kufanya ugaidi. Leo mkiona Waarabu na Waislamu wanapata paspoti za Tanzania mnaanza kuleta maneno. Soma huu uzi tangu mwanzo utaona udini na ubaguzi uliokuwepo usikatae.
 
ukosefu wa busara na upungufu wa mkubwa wa uwezo wa kuwasiliana
 
Yaani hapo uhamiaji inaonekana kumeoza ni pa kupafumua pote kuanzia juu hadi chini

Nchi yetu inaonekana shamba la bibi kichaka cha nyani

Mtu yeyote kutoka huko anapesa passport kifala sana

Wakati mzawa anazungushwa weee hadi akome mwenyewe

Uhamiaji kumeoza
 
Pale kkoo Kuna mtaa unaotwa Omary Nundu sijui, ktk huo mtaa Kuna wasomali wanaongea kisomali waziwazi ..bila Shaka wale sio wa Tz Wanabiashara pale, unakuta
Wamejificha ktk maduka ila wame waweka na wa Swahili
Uhamiaji wafanyie kazi hii

Ni majukumu yao kuwatambua raia wa nchi zingine wanaoishi kinyemela nchini

Coz inatishia usalama wa taifa ,kiulinzi,na kiuchumi mbaya zaidi jamaa wanchuma hela hapa wanapeleka kwao huko
 
Yule mama yuko soft sio kwamba hana uwezo ila yuko soft sana
 
Weledi ziro
 
Umekuja kuchafua huu uzi hapa

Sio lazima uwe unavamia kila sehemu

Sehemu zingine uwe unasoma tu

Hehehe Ukishataja Kenya lazima mitambo yangu isimame wima, hapo mleta mada amemtuhumu Mkenya aliyekuja akatumia hela ndefu kusaka paspoti ya Tanzania, nikawa najiuliza ikiwa paspoti ya Kenya tayari ina nguvu kuizidi ya Tanzania, maana kwamba Mkenya anaruhusiwa kuingia kwenye mataifa mengi zaidi ya Mtanzania, sasa nini kimtume aje kusaka hiyo ya Tanzania tena kwa kulipia hela ndefu.

Sema inawezekana labda hakua Mkenya mzawa, labda mpigaji tu wa kutokea Somalia anajiita Mkenya, au iwe Mkenya ambaye amechafua Kenya anatafuta pakutokea, ni muhimu sana watu kama hao kukamatwa. Mleta mada angewatonya polisi kabisa waje wamkamate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…