Salamu kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Passport za Tanzania zinakimbilia mikononi mwa wageni kupitia viongozi waandamizi na askari

Nishawahi kutana na jamaa Warundi huko ughaibuni, wana passport za bongo na wanazitumia kuzamia Canada na Australia kama wakimbizi...
 
Hapa mleta mada anasema 2016 ,2018 si ndio Mzee magu alikuwepo au ?
 
Sio passport tuu na utoaji vyeti vya kuzaliwa uangaliwe kwa umakini.
 
Nchi imekuwa ya hovyo sana,, Ujamaa pia unapelekea haya,,,Watu wanaoneana huruma wanashindwa kufuata sheria za nchi...

Kuanzia Rais ni corrupted, mawaziri,, wanakwaya wa ndugai hadi mtendaji wa kijiji....

Uzalendo umebakia wa wachache sana ambao wakiongea wanaitwa wametumwa na mabeberu...
 
Watu wengi wanaotafuta passport ya nchi ingine ni kwamba hawana sababu ya kihalali. Mfano mtu anataka kuzamia Ulaya au canada kama msomali atatafuta pasi ya kitanzania.

Wapo wa yemen na syria wanakuja wanaoa wanatafuta pasi sababu labda wana historia ya criminal ili wapate urahisi wa movement, wengine wanawekeza hapa ili wapate unafuu wa kumiliki hata ardhi inabidi watafute pasi ya kibongo.

Sasa hivi hata waturuki wameshtuka Tanzania nchi nzuri kuwekeza na kuoa wana opt kuomba uraia na kupata mkoba wa hapa.
 
Sijasoma yote Ila wewe jamaa inaonekana ni mzalendo kwerii kweriii.. kuna sehemu nilipita huko Kagera , wanyarwanda wamepata NIDA kibaoo, na wanajitambilisha kuwa wao ni watz wa kuzaliwa

Kuna mambo usiyojua kuhusu eneo unalolizungumzia. Toka mwaka 1959 katika vita ya kiraia, waliingia Tz na kupatiwa hifadhi. Baada ya hapo JK Nyerere aliwapa uraia. Hao ni watoto wa raia na wamezaliwa Tz. Kuongea lugha ya kinyarwanda Tz sio hoja.

Birthright gives one a citizenship! Na sio sheria ya nchi hii tu bali makubaliano ya kimataifa.
 
Mbona kuna Watanzania kibao tu wana passport za Sweden,Canada,UK and etc kwa kujifanya wakimbizi wa Nchi za jirani zao, sisi wakijifanya Watanzania tunalia Uzalendo.Hii issue nadhani ni ya duniani kote sema kwetu tatizo ni rushwa ikimewe.
 
Ipo siku hii nchi itaongozwa na mkongo kwa ujinga kama huu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haujaeleleweka au unamaanusha urahis wa kupata passport ni kila nchi wanamagummashi na sio tz pekee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rushwa rushwa rushwa rushwa rushwa rushwa 😎
 
Kuna jamaa anaitwa Juma yupo hapo Uhamiaji Kurasini ana Vanguard Nyekundu, hii ndiyo kazi yake ameajiri vijana mtaani kabisa wanadeal na hao wageni Wasomali, Wahindi na waarabu, jamaa ana hela sana kwa sasa anajenga ghorofa kubwa sana kibaha.
 
Mbona kuna Watanzania kibao tu wana passport za Sweden,Canada,UK and etc kwa kujifanya wakimbizi wa Nchi za jirani zao, sisi wakijifanya Watanzania tunalia Uzalendo.Hii issue nadhani ni ya duniani kote sema kwetu tatizo ni rushwa ikimewe.
Watanzania tulio wengi ni limbukeni ushamba na uzalendo wa kinafiki, huu ni mchezo dunia nzima na inchi zinazo eleweka kama US UK FR CND SA wageni wengi wana manipulate system zao na kupata passport bila kupigiwa kalele sembuse hapa kwetu hapa 3rd world country, wanatumia hapa tu kama exit door kutafuta rizki nje ni wachache wana opt kuka hapa milele hi nchi yetu ni shida raha na utajili viko kwenye nadharia havionekani.
 
Ukarimu unaanzia nyumbani. Weka hapa majina na passport zao zote huyo kamishna atayachukua hapahapa na jamii itapaza sauti kuanzia hapa. Pia yapeleke twitter, Facebook e.t.c kule pia kuna maofisa wa serikali wanaoweza kuchukua hatua. Tunataka tanzania salama japo tutapigwa mnada.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…