Salamu ya Rais Samia Suluhu 'Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano' ni salamu bomba sana

Salamu ya Rais Samia Suluhu 'Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano' ni salamu bomba sana

Hiyo ni sakaam ya kiislam acheni ubishi japo ina maana nzuri.huwezi kuitumia kanisani.ni sawa na kusena bwana asifiwe msikitini utakuwa wa ajabu.kwenye nchi ya dini kama hizi tuachane na hizo salaam za kidini au tutumie zote
Makanisa ya gwajima huwezi kuitumia ila makanisa ambayo yapo Egypt. Iraq na uarabuni wanaitumia kwa sababu ni lugha yao.

Usiwe kiazi
 
Wanabodi siku ya uapisho wa Katibu Mkuu Kiongozi ndugu katanga kuna jambo lilitokea, Bwana katanga alisalimu Raia kwa lugha moja tu ya dini ya kiislamu yaani Salaam Allahkum na akaendelea na hotuba yake,

Ikumbukwe pale kuna makundi mengi

Mama Samia aligundua kundi kubwa halijaridhika na ile Salamu Yeye akasalimia kwa Salamu mpya yaani"Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ni maoni yangu tu bora kama mtu anaona kusalimia kwa lugha za dini ni kero basi atumie" Habari zenu wananchi"

Wanasiasa wanasalimia kwa lugha zote ili kuleta umoja, Sasa ukisalimia kwa imani yako tu hii itagusa watu fulani tu

Nakupongeza sana Mama Samia kwa kuliona hilo na kulirekebisha pale pale kuna ujumbe umetuma kwa huyo msaidizi wako
Ila mibongo mnazozaaaaa mnazozaaaaa mnooooo.

Hamjui hata mnachotaka ni Nini ???
 
Most of hawa waimba kwaya hudhan kama mtu alisema Asalaam aleykum basi ni uislam umeingia,hiyo ni lugha tu ya kiarabu,infact hata christian arabs huitumia salam hiyo katika hadhira zao,ni kukosa elimu na exposure kunawajengea uzuzu wa kias kikubwa Kama hiko
 
Nakwambia kwa Kweli. Wajinga nchi hii wako wengi sana . Hawajui hata hao waarabu wapo wakristo, waislamu na hata wasio dini na wote wakisalimiana wanatumia salamu iyoiyo.

😀😀😀

Hahaha kama hadi hapa hajaekuelewa basi ana tatizo kichwani.
 
Kwani unajua maana ya salamu aliyoitoa katanga ni nini????

Kwa akili zenu mfu mnadhani salamu ya Katanga ni ya kidini??? Kweli hili taifa bado sana na ndo mana Mwendazake aliweza kuwa brainwash.

Salamu aliyotoa katanga simply means Amani iwe nawe, ni sawa na myahudi akikwambia Shalom. Zote zinamaanisha Amani iwe nawe.

kuna clip Jenerali ulimwengu amelielezea Hilo itafute uelimike mataga wewe!
Matusi yanakujaje hapa we mwehu? Mataga kwa lipi? Mmeendekeza dini hadi mnajisahau kama wengine wapo. Nyambaf
 
Wajinga ni wengi sana hapa Tanzania. Yaani jitu zima linaanzisha mada kuwa As-Salaam Alyakum ni salamu ya kiislamu alafu linajiona Lina akili kinyama. Kumbe limejilisha tango Pori tu
Most of hawa waimba kwaya hudhan kama mtu alisema Asalaam aleykum basi ni uislam umeingia,hiyo ni lugha tu ya kiarabu,infact hata christian arabs huitumia salam hiyo katika hadhira zao,ni kukosa elimu na exposure kunawajengea uzuzu wa kias kikubwa Kama hiko
 
Udini gani??? Hivi Unajua maana ya salamu aliyotoa Katanga ni nini???

Kwa akili yako wewe ulivyoaminishwa kuwa ni salamu ya kidini basi unataka hata sie tunaojielewa tuione kuwa ni ya kidini wakati sio??? Acheni ujinga wenu

Salaam Allahkum Kama inavyotamkwa simply inamaanisha amani iwe nawe.
Kwanini watanzania tusalimiane kwa lugha za kiarabu au kiyahudi ktk shughuli za kitaifa, kisiasa n.k.?
 
Matusi yanakujaje hapa we mwehu? Mataga kwa lipi? Mmeendekeza dini hadi mnajisahau kama wengine wapo. Nyambaf
Nani ameendekeza dini??? Kivipi???

Tena Kwa taarifa yako mimi ni mkristo niliyebatizwa kabisa kikristo.

Mataga ndo wana izo akili Kwa sababu mlishazoea kuwa brainwashed na huyo mwendazake wenu kwa kujifanya anamtaja Mungu kila wakati kumbe alikuwa mkabila, muuaji na mbambikaji kesi watu mkubwa.
 
Kwanini watanzania tusalimiane kwa lugha za kiarabu au kiyahudi ktk shughuli za kitaifa, kisiasa n.k.?

Mbona hilo hukohoji kipindi Cha mwendazake uje uhoji leo??

Nin kimekuwasha na jamaa zako hadi muilete HOJA hiyo leo Tena kwa chuki ya waz waz kabisa?

Ofcourse tunajua most of you guys mnatuchukia Sana muslims,na hatuujui kosa letu ni nin,may be ni kwa kuwa kwetu waislam,lakin basi punguzeni chuki basi,hadi Salaam tuh Tena ni salaam universal kabisa inasababisha uamshe hisia za malumbao ya kidini kweli??

Acheni hizo nyinyi jamaa.
 
Na kuna wengine hawana dini pia, au hawaamini kabisa uwepo wa Mungu.

Salaam aleykum,maana yake ni Aman ya bwana mungu muumba iwe nanyi,

Tofaut hapo ni hiyo lugha iliyotumika tuh,nadhan ingetumika lugha ya kiswahili au kiingereza isingeleta shida hapo,

Sasa HOJA yenu ilipaswa kuwa salaam za lugha ngeni,Kama za kiarabu au kiingereza zisitumike kwenye hafla za taifa,na siyo kusema salaam ya kiislam au kukimbilia kulalamika udini katika jambo Kama hilo,inaonesha either kuna kitu hukifaham au una chuki umezificha nyuma ya hilo
 
Back
Top Bottom