Wanabodi siku ya uapisho wa Katibu Mkuu Kiongozi ndugu katanga kuna jambo lilitokea, Bwana katanga alisalimu Raia kwa lugha moja tu ya dini ya kiislamu yaani Salaam Allahkum na akaendelea na hotuba yake,
Ikumbukwe pale kuna makundi mengi
Mama Samia aligundua kundi kubwa halijaridhika na ile Salamu Yeye akasalimia kwa Salamu mpya yaani"Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ni maoni yangu tu bora kama mtu anaona kusalimia kwa lugha za dini ni kero basi atumie" Habari zenu wananchi"
Wanasiasa wanasalimia kwa lugha zote ili kuleta umoja, Sasa ukisalimia kwa imani yako tu hii itagusa watu fulani tu
Nakupongeza sana Mama Samia kwa kuliona hilo na kulirekebisha pale pale kuna ujumbe umetuma kwa huyo msaidizi wako