Salamu za Shukrani kwa Wanachama wa JamiiForums

Salamu za Shukrani kwa Wanachama wa JamiiForums

WAlioomba ufafanuzi ulikuwa mtego, Mello au Mod mwingine yeyote angejitokeza kutoa kauli, ingekuwa NI kesi kubwa kwamba amekiuka zuio Kwa kuendesha JF. Mshana arejeshe Ile namba, uchangiaji ufanyike lakini Mello au Mod wakae kimya ili kutojiingiza matatizo.
Pia anayetuma, asitumie namba yake, tuma direct Kwa wakala maana mifumo inasomana
Na sasa kuleta huu uzi wa shukrani tena kwa kutumia official account ya JF unafikiri bado hawajavunja masharti? 😳😳😳
 
Mnachofeli ni kuendelea kuwatolerate hawa machawa ambao wanaendelea kushusha thread za uchawa bila kujali mama yao ameifungia jf!! Aisee siku mkiwalima hawa machawa kama ban ya mwaka mimi pia nitachangia.
 
Kufuatia zuio lililotolewa Septemba 6, 2025 na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikisitisha leseni ya utoaji maudhui nchini humo kupitia Jukwaa la JamiiForums kwa siku 90, member wa JF, Mshana Jr alianzisha uzi (https://www.jamiiforums.com/threads/tusimame-na-jf-yetu-kipindi-hiki-kigumu.2387883/) kuhamasisha wanachama na wapenzi wa JF kuungana nasi katika kipindi hiki.

Mpaka kufikia leo Septemba 27, 2025 tumepokea kiasi cha Tsh. 233,603.00/-

Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kila aliyejitoa kuungana nasi kwa salamu za pole, kuchangia na hata kuwa nasi kwa njia ya maombi wakati huu JamiiForums imezuiwa kutoa huduma zake nchini Tanzania.

Tunathamini sana umoja na mshikamano mliotuonyesha na mnaoendelea kutuonyesha🙏.
Mbona ndogo sana.
 
Back
Top Bottom