Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Kwa haraka haraka huyo ni mwalimu wa daraja E1. Na anaonekana alishamaliza deni la bodi ya mikopo au hakupata kabisa kusomeshwa kwa udhamini wa HESLB kwa hiyo kaenda kajitungua milioni kama 25+ . Yeye ndo anajua kama amekamilisha malengo au bado.
Tukope kwa sababu maalum.
Tukope tukiwa tumeshafanya upembuzi kamili kwa miradi au mradi tunayoifanya
Kwa miaka 7 amekopa 10 to 15 mil
 
hiyo salary sleep kama yangu tu , ila sijutii mzee hata ungesema niwalipe bank den lao nawalipa , mkopo niliochukua ulibadili kila kitu kwenye maisha yangu
 
Mkopo mtamu siku umeingizwa, ipite miezi kadhaaa , mtu anaanza sikilizia maumivu
Nilikopa ila sijawahi kujuta.Nilikopa nikaanzisha project ambayo ilikuwa inaniingizia kipato ambacho kilikuwa zaidi ya kile nilichokuwa nakatwa japo ile project ilikuwa ya muda.Kile kipato plus kamshahara kalikobaki kila mwezi nikatumia kupata pesa ya Kula na kuanzisha project nyingine ya kudumu.Nilimuomba Mungu hiyo project ya Kwanza itakapokoma niwe nimemaliza kuwekeza kwenye project mpya hivyo nipate kipato Cha ziada kupitia project hii.Kweli Mungu amejibu,project ya Kwanza imekoma wakati namalizia project hii ya kudumu na mkopo bank nimemaliza kulipa.Ni furaha iliyoje kamshahara kangu kanaingia kote na chimbo linatema.We acha tu mkopo Ni mzuri Kama ukiwa na malengo.
 
View attachment 2200989

Basic salary: 940,000
......
Michango/makato yake

Chakuhawata contribution 5000
PSSSF 47,000
PAYE 94,200
Nmb bank loan 42,870,300 (451,266)
NHIF fund employees 28,200
......
NET AMOUNT DUE.. 314,333.68 Tshs
Ondoa hiyo NMB loan ijimlishe kwenye pesa anazochukua benki(takehome), sababu alikopa au alichukua sehemu ya mshahara wake kabla ya mwisho wa mwezi.
 
Back
Top Bottom