Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Nazingatia sana kanuni za uandishi Babu, habari naiandika kama ilivyo bila emotions.

Ubuyu kwa sasa nawapumzisha kidogo, nadeal na taasisi kwanza. Siku nikirudi kwenye ubuyu nitarudi na habari ya moto, kwa sasa soma ubuyu wa zamani Babu.
Nafurahi kusikia hivyo, kumbe Wazee hatukupoteza fedha zetu kukusomesha London University

Ndiyo maana tumemwambia Mkwe bila kuleta Ofa nono kwaajili ya Posa yako, hatukuachii kirahisi 😜

We real appreciate 🙏
 
Nilitafakari baada ya kupewa hii habari… au ndio maana Mo alitishia kufunga viwanda vyake huenda sababu ndio hii?
Acha uongo suala la MO kutaka kufunga viwanda vya chai ni kwasababu ya kuporomoka kwa bei ya zao la chai! Na pia serikali kuongeza kodi kwenye zao la chai na kuondoa ruzuku! Na kuruhusu chai nyingi kutoka nje ya nchi ambazo ni bei rahisi,hivyo viwanda kuwa na mzigo ambao hauna pa kwenda.

Sio yeye hata shivajee wamefunga viwanda vyao vya Vitu vingine ingieni hata google kuona soko la chai kuporomoka jameni! Uongo mwingi mpaka kero
 
Zahera aliibeba sana Yanga,ingawa na yeye alikua na mtu nyuma
Niliwahi kusikia hilo, kuwa Zahera alikuwa na tajiri mkubwa nyuma yake huko Kongo na walikuwa na mpango wao kabambe kwa misaada ile ila sikuwahi kumjua wala kuujua mpango maana kipindi hicho nilipoteza mawasiliano na chanzo changu.
 
Acha uongo suala la MO kutaka kufunga viwanda vya chai ni kwasababu ya kuporomoka kwa bei ya zao la chai! Na pia serikali kuongeza kodi kwenye zao la chai na kuondoa ruzuku! Na kuruhusu chai nyingi kutoka nje ya nchi ambazo ni bei rahisi,hivyo viwanda kuwa na mzigo ambao hauna pa kwenda.

Sio yeye hata shivajee wamefunga viwanda vyao vya Vitu vingine ingieni hata google kuona soko la chai kuporomoka jameni! Uongo mwingi mpaka kero
Hiyo ni tafakuri yangu binafsi sio sehemu ya habari niliyoileta, soma uelewe acha mihemuko.
 
NImekusoma Nifah ,hii kitu ukiitazama kisoka soka na kiushabiki inachekesha na utaishia kufurahi msoto wa simba, ila kwa uoande wa ki business management lazima umuonee huruma Try again kama haya ni ya kwel?. Na hii ni mbaya sana kwakua wewe ndio uko front intouch na players katika kutimiza majukumu ya kila siku, wao wanakuona wewe. Wao ni rahis kuamini wewe pengine unacheza na maslahi yao, pengine boss anatoa ila wewe na wenzako mnakula. Hii situation lazima tu imuweke pagumu. Nakumbuka mimi kioind hiko sasa salary zna delay muda wa kutosha, watu ofisin wanakununia wewe 😂.
Ikafika kipind nikaona no way hapa lazima i have to withdraw some of them, unawaondoaje kazin na wana madai yao??? Na unawaachaje ofisin wakat madai ndio yatazid kusoma?.

Huyu Try again kama anaweza , wala asisite, ampige pindu tu. Ila azichange karata zake vizuri, ugomvi na tajiri unahitaji uwe umejipanga 😂😂
Try Again sio mzembe, ana backup ya kutosha. Zingatia aya yangu ya pili kutoka mwisho.
Mpaka unaona Mo anahaha kwa siasa za kwenye derby ujue ana hali mbaya.
 
Niliwahi kusikia hilo, kuwa Zahera alikuwa na tajiri mkubwa nyuma yake huko Kongo na walikuwa na mpango wao kabambe kwa misaada ile ila sikuwahi kumjua wala kuujua mpango maana kipindi hicho nilipoteza mawasiliano na chanzo changu.
Zahera wala hakuwa na tajiri kutoka Congo bali ni wajanja wa hapa hapa Bongo wakina Ndama na wenzake waliokuwa wananufaika na utengenezaji was jezi za Yanga,kila wiki walikuwa wanafyatua jezi mpya.
 
Habari zako ni za kuokoteza! Uyo bahkressa kwa Sheria za FIFA hana uwezekano wa kuichukua Simba kwa namna yeyote labda kwanza aivunje Azam fc na ni kitu kisichowezekana!
Pili serikali haikusema mchakato uanze upya bali ilisema Simba ifanye mabadiliko ya katiba ili iweze kukidhi vigezo vya kufanya mabadiliko ya kimfumo! Mabadiliko ambayo Simba walifanya yalipitishwa na mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika miezi minne iliyopita.
Suala la MO kutotoa pesa ni uongo! MO anatoa pesa kila mwezi millioni 200 TSH. Kulingana na makubaliano ya uwekezaji!
Try again Abdala Muhene na swaiba wake Mangungu wana kashfa ya kushirikiana na baadhi ya wachezaji kuhujumu timu mechi ya yanga ile Simba aliyofungwa goli tano! Taarifa ziko zilijadiliwa kwenye board na ushahidi ukatolewa!
Pia Muhene na Mangungu wana kashfa ya kupangisha frem zilizopo jengo la club ya Simba bila utaratibu ambapo kiasi cha millioni 500 TSH. Hazionekani. Ndio zilioleta ugomvi yeye na Barbra!
MO sio msimamizi wa timu wala operation, za kila siku za timu hivyo matokeo mabovu yeyote ni kazi ya benchi la ufundi la timu,wachezaji na secretary ya timu chini ya CEO kajura pamoja na bodi chini ya Abdala try again.
Sijakulazimisha kukubaliana na habari yangu, kama unaona napotosha fungua uzi wako uandike ukweli halafu muda ndio utaamua.
Huna unachokijua, acha kushupaza shingo.
 
Nilitafakari baada ya kupewa hii habari… au ndio maana Mo alitishia kufunga viwanda vyake huenda sababu ndio hii?
Umetafakari ukaona hii sababu ina uzito wa kuchuka maamuzi ya kufunga viwanda. Ok boss.
 
Acha kutumalizia MB zetu, mwajiriwa aliwahi kumfukuza mwajiri tangu lini? Haya mambo Yako kisheria, muwekezaji ana mamlaka ya kuteua na kutengua watu wake. Hayo mengine ni matango unatulisha
 
Acha kutumalizia MB zetu, mwajiriwa aliwahi kumfukuza mwajiri tangu lini? Haya mambo Yako kisheria, muwekezaji ana mamlaka ya kuteua na kutengua watu wake. Hayo mengine ni matango unatulisha
Kwani umetumwa kusoma au ni wewe na kiherehere chako? Threads zipo kibao nenda huko.
 
Back
Top Bottom