Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Nazingatia sana kanuni za uandishi Babu, habari naiandika kama ilivyo bila emotions.

Ubuyu kwa sasa nawapumzisha kidogo, nadeal na taasisi kwanza. Siku nikirudi kwenye ubuyu nitarudi na habari ya moto, kwa sasa soma ubuyu wa zamani Babu.
Nafurahi kusikia hivyo, kumbe Wazee hatukupoteza fedha zetu kukusomesha London University

Ndiyo maana tumemwambia Mkwe bila kuleta Ofa nono kwaajili ya Posa yako, hatukuachii kirahisi 😜

We real appreciate 🙏
 
Nilitafakari baada ya kupewa hii habari… au ndio maana Mo alitishia kufunga viwanda vyake huenda sababu ndio hii?
Acha uongo suala la MO kutaka kufunga viwanda vya chai ni kwasababu ya kuporomoka kwa bei ya zao la chai! Na pia serikali kuongeza kodi kwenye zao la chai na kuondoa ruzuku! Na kuruhusu chai nyingi kutoka nje ya nchi ambazo ni bei rahisi,hivyo viwanda kuwa na mzigo ambao hauna pa kwenda.

Sio yeye hata shivajee wamefunga viwanda vyao vya Vitu vingine ingieni hata google kuona soko la chai kuporomoka jameni! Uongo mwingi mpaka kero
 
Zahera aliibeba sana Yanga,ingawa na yeye alikua na mtu nyuma
Niliwahi kusikia hilo, kuwa Zahera alikuwa na tajiri mkubwa nyuma yake huko Kongo na walikuwa na mpango wao kabambe kwa misaada ile ila sikuwahi kumjua wala kuujua mpango maana kipindi hicho nilipoteza mawasiliano na chanzo changu.
 
Hiyo ni tafakuri yangu binafsi sio sehemu ya habari niliyoileta, soma uelewe acha mihemuko.
 
Try Again sio mzembe, ana backup ya kutosha. Zingatia aya yangu ya pili kutoka mwisho.
Mpaka unaona Mo anahaha kwa siasa za kwenye derby ujue ana hali mbaya.
 
Niliwahi kusikia hilo, kuwa Zahera alikuwa na tajiri mkubwa nyuma yake huko Kongo na walikuwa na mpango wao kabambe kwa misaada ile ila sikuwahi kumjua wala kuujua mpango maana kipindi hicho nilipoteza mawasiliano na chanzo changu.
Zahera wala hakuwa na tajiri kutoka Congo bali ni wajanja wa hapa hapa Bongo wakina Ndama na wenzake waliokuwa wananufaika na utengenezaji was jezi za Yanga,kila wiki walikuwa wanafyatua jezi mpya.
 
Sijakulazimisha kukubaliana na habari yangu, kama unaona napotosha fungua uzi wako uandike ukweli halafu muda ndio utaamua.
Huna unachokijua, acha kushupaza shingo.
 
Nilitafakari baada ya kupewa hii habari… au ndio maana Mo alitishia kufunga viwanda vyake huenda sababu ndio hii?
Umetafakari ukaona hii sababu ina uzito wa kuchuka maamuzi ya kufunga viwanda. Ok boss.
 
Acha kutumalizia MB zetu, mwajiriwa aliwahi kumfukuza mwajiri tangu lini? Haya mambo Yako kisheria, muwekezaji ana mamlaka ya kuteua na kutengua watu wake. Hayo mengine ni matango unatulisha
 
Acha kutumalizia MB zetu, mwajiriwa aliwahi kumfukuza mwajiri tangu lini? Haya mambo Yako kisheria, muwekezaji ana mamlaka ya kuteua na kutengua watu wake. Hayo mengine ni matango unatulisha
Kwani umetumwa kusoma au ni wewe na kiherehere chako? Threads zipo kibao nenda huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…