Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Salma Kikwete, amewahamasisha wanawake kote nchini kujitokeza kugombea nafasi za udiwani na ubunge, huku akiwataka kuwaunga mkono wanawake wenzao kwa kura nyingi, hususan mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kanda ya Kusini, Salma alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika nafasi za maamuzi na uongozi.
Pia soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"Lazima wanawake tusiwe na ajizi. Rafiki wa mwanamke ni mwanamke mwenzake. Anaposimama mwanamke, ni jukumu letu kumsaidia kwa hali zote. Tunawaomba wanaume mtuunge mkono, tunataka kura za kihistoria ambazo hazijawahi kutokea hapa Tanzania, barani Afrika, na ulimwenguni kote," alisema.