Salome Mgaya (Mama Kibonge) akamatwa kwa ukwepaji Kodi za Mabilioni ya fedha Bandarini

Mi nadhani nyeupe isemwe nyeupe na nyeusi isemwe nyeusi ukwepwaji wa kodi kwa wafanyabiashara upo mwingi sana na hii haipingiki kupitia stoo inajulikana, kutoa risiti za mzigo pungufu kithamani nayo kawaida. Wafanyabiashara nchi hii si wazalendo yajulikana upande wa pili napo tatizo kuna vikodi vingi vingi na vya kipuuzi ambavyo mwisho wa siku mpaka upande wa pili wanapata sababu kuleta haya yaliyotokea.

Hitimisho: NANI AMVISHE PAKA KENGERE
 
Mwigulu anashida ya kiburi
 
Mama kibonge kashinda vita....
 
Yule wa container 15 na kudaiwa bilioni 30 mara 10 mara 3.5 ndiyo wa mapicha picha na mkubwa?
 
Ila tuacheni utani kodi TRA kubwa sana bila ujanja janja hakuna kutoboa.
Uwiano wa manunuzi katika uagizaji na tozo na kodi sio sawa.
Mfano ukiagiza gari,kodi na tozo ni sawa au zaidi ya thamani ya gharama ya kuagiza gari,(uagize gari kwa Tshs.milioni 10,kodi na tozo milioni 15,mpaka utoe bandari gharama jumla inakuwa Tshs.milioni 25 ).
PENDEKEZO:
1.TRA ibadilishe tafsiri ya kumiliki gari kuwa ni anasa,bali ni bidhaa muhimu katika kukuza uchumi wa taifa,kwani wamiliki wakiwa wengi watachangia kodi kwa kununua mafuta.
2.Kodi ya uagizaji magari ipunguzwe hasa "import duty".
 
Tunahangaika na kina Mama Kibonge pekee na kuwasahau / kujifanya hatuoni wanayoitafuna iliyoshakusanywa !!!!, Anyway hili limetupa Nishati nguvu za kusifia....,

By the way wamejuaje alikuwa anakwepa kwa muda mrefu ? Kwahio walikuwa wanamuona na kumfumbia macho ?
 
Siwezi watetea hao hata siku Moja ni wakwepaji Kodi wakubwa na hawatakiwi kuchelewa..

Pamoja na Changamoto za watu wa TRA ila kucheka na Hawa watu umekwisha,hakuna mfanyabishara anataka kulipa Kodi Kwa hiari hayupo hata Mimi Huwa silipi inavyotakiwa labda Kwa kubanwa.
 
Tutimize wajibu kwanza ili tudai uwajibikaji.
 
Sera ya Tanzania Ina discourage magari used ndio maana unaona Iko hivyo.
 
Ona huyu amehama kutoka kwenye mada ya kero za kulipa Kodi amehamia kwenye siasa Kwa kudia Kodi inaliwa

Mpaka hapo huo unakuwa ni mgomo wenye msukumo wa Kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…