Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,776
- 42,933
Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Salum Mwalim amefunga ndoa na kada wa chama hicho Moza Ally. Taarifa kutoka chanzo kinachoaminika kimetueleza kuwa Salum na Moza walifunga ndoa Ijumaa ya Februari 13, 2026 japokuwa picha zimeachiwa leo mtandaoni.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram @mozaally_ amechapisha picha zao huku akiambatanisha na ujumbe "Kila mja ana siku yake. Mwenyezi Mungu amenijalia neema kufika na kufurahia siku yangu. Subira, uvumilivu na imani ni muhimu ili kufikia siku kama hii. Asante Allah, wazazi wangu, familia yangu, marafiki na ndugu, na hasa mume wangu kwa Kuniona, kunipenda na kuniamini."