Write your reply...
nikisoma repry za watu humu napata ukakasi,hasira sana
samatta abaki genk kufanya nini? na umri unaenda?
pale epl atatakiwa kuwa misimu miwili au mitatu kuonesha ubora wake, sasa genk akibaki umri je? na tunajua waafrika kwa kudanganya miaka tulivyo!.
genk ni chuo pale sitaki kuwataja waliocheza pale sote tunawajua!
halafu kwanza ma striker aina ya samatta wanatakiwa na klabu nyingi za epl, pia samagoal ana kichwa cha kuelewa mfumo haraka mno. sasa kama kacheza soka gumu la hapa africa ambalo wanakaba man to man , why ashindwe kucheza soka la epl wanalokaba njia tuu mara nying? anajua kujiposition kitu ambacho hata gonzalo higuain kinamshinda! why ashindwe?
muda ni jaji mzuri sana tusubiri kama akienda tuone kama mashangingi ya soka hayajakimbia humu!.
halafu nani kasema kucheza europa ni kazi rahisi?
kule unakutana na team ambazo wachezaji wake wanatafuta majina so wanacheza kwa spirit na moyo!
man u,athletico madrid,walipochukua europa hamkusema wanafunga vi timu vidogo?