Same: Watu 37 wafariki dunia kwa ajali, 29 wajeruhiwa. Mabasi yagongana na moto kulipuka

Same: Watu 37 wafariki dunia kwa ajali, 29 wajeruhiwa. Mabasi yagongana na moto kulipuka

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Basi la Channel one na Costa Mwami yamegongana na kuwaka moto. Cheki Point wilayani Same, umbali wa kilomita tatu kutoka Same Mjini.

Ajali hiyo ambayo imethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ua Same,Kaslida Mgeni,imetokea saa 12 jioni.

Aidha,inadaiwa watu kadhaa wamefariki dunia kwa kuungua na moto baada ya kushindwa kutoka ndani ya magari hayo.

Watu 36 wamefariki dunia na wengine 30 kujeruhiwa katika ajali ya moto iliyotokea leo Juni 28, 2025, katika eneo la Sabasaba, Kata ya Same, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa ya awali iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Same, Bi. Kasilda Mgeni kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, ajali hiyo imehusisha basi la abiria la kampuni ya Chanel One lenye namba za usajili T 179 CWL lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga, na basi dogo aina ya Coaster lenye namba T 199 EFX lililokuwa linatoka Wilayani Same.

Magari yote mawili yamegongana uso kwa uso na baadaye kuwaka moto, na watu wengi walishindwa kujiokoa.

Amesema Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu tayari amefika eneo la tukio na anatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu hatua zaidi zilizochukuliwa pamoja na hali ya majeruhi.

Screenshot 2025-06-28 192949.png
Screenshot 2025-06-28 193007.png
 
Abiria zaidi ya 10 wanahofiwa kufa baada ya magari mawili, basi la Channel One lililokuwa safarini kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro kugongana na basi dogo aina ya Toyota Coaster kisha magari yote mawili kuungua kwa moto.

Mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mdimila amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

IMG-20250628-WA0063.jpg
 
View attachment 3387212
View attachment 3387210
Maccm yashaanza kututoa kafara
 
InShot_20250628_201522293.jpg

Watu takribani 50 wanahofiwa kufariki dunia kufuatia ajali iliyohusisha magari mawili ya abiria moja aina ya basi la kampuni ya Chanel One na basi dogo aina ya Coaster, kugongana uso kwa uso kisha kuwaka moto katika eneo la Njoro wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Subiri Taarifa zaidi
 
Back
Top Bottom