Samia aizika CCM rasmi: Ugonjwa wa mbeleko za kisiasa zaanza kuitafuna CCM yenyewe

Naona hata mzee wa Msoga katika maelexo yake66 alikuwa na kigugumizi lakini akajishtukia na kuona kama maelezo yake hayamsaidii Mama!
Huku akielemewa na kelele za chawa wa Mama akaamua kuunga mkono maamuzi.
Hata Mimi niligundua hilo, nadhani amekuwa surprised au ni janja janja yake asieleweke yupo upande gani !
 
Kwa kweli kile kilichofanyika mchana huu ni maajabu.Hata Nyerere pamoja na kuwa na Mamlaka makubwa mno hakudiriki kuburuza wajumbe kiasi hicho.
Jambo hilo litaleta mgogolo ndani ya chama.
CCM hii hakuna wakuweza kuleta mgogoro ndugu, ni kama wamemezeshwa dawa fulani - Yaani ni kama libwata kwenye mapenzi au msukule - hawahoji, hawalalamiki, hawaulizi chochote..
Imagine et mtu anashinda kwa asilimia 100..hata mmoja wa kupinga hayupo..labda kama huyo mtu ni Mungu mwenyewe.
Tanzania tuna-bahati mbaya sana - chama tawala - CCM wanalinda maslahi yao na watu wao na familia zao, CDM ni kama genge la wahuni tu sasa hivi nao, hakuna descpline, hakuna utaratibu, mara rushwa, kusalitiana, ACT - hawa hata hawaeleweki wako wapi..huku ni kama extension ya CCM na serikali huku tena wanajinasibu kama chama tawala etc..hao waliobaki bora wafutwe tu...
Tuna bahati mbaya sana
 
Ccm ni chama , na tasisi ya umma, sio cha mwenyekiti kwa kilichofanyika kamati za kinidham zinatakiwa kukaa na kutoa adhabu ikiwa ni pamoja kuwavua nyadhifa na uanachama wote walioshiriki,
CCM ni mali ya Mwenyekiti huwezi kumfanya kitu chochote Mwenyekiti wa CCM kama ilivyo kwa upande wa Rais wa nchi hata akifanya nini yupo juu ya sheria
 
CCM ni mali ya Mwenyekiti huwezi kumfanya kitu chochote Mwenyekiti wa CCM kama ilivyo kwa upande wa Rais wa nchi hata akifanya nini yupo juu ya sheria
Iko vile bandugu na itabaki kuwa vile mpaka itakapokuwa vinginevyo !!
Hata Mzee wa karibu na Kibaigwa aliyepotea kwenye anga za siasa anajua hivyo ! Mwenyekiti sio mchezo !
😳!
 
Kumbe siku hizi CCM hamna suala la kuchukua fomu na kupigiwa kura...ni mwendo wa kusonta tu kidole kisha mtu anapata kura zote za ndio...what a step!, poor Tanzania.
 
CCM imefanya jambo jema kabisa, mivutano imekwisha sasa, pia hili litaokoa fedha za chama maana kutakuwa hakuna haja ya kuitisha vikao vingine ambavyo huwa na gharama kubwa kweli it's a cost cut mission thank you mama Samia umawaweza
 
Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanaopewa dhamana huahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo, a.k.a kujizima data
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…