Samia aizika CCM rasmi: Ugonjwa wa mbeleko za kisiasa zaanza kuitafuna CCM yenyewe

Samia aizika CCM rasmi: Ugonjwa wa mbeleko za kisiasa zaanza kuitafuna CCM yenyewe

Naona hata mzee wa Msoga katika maelexo yake66 alikuwa na kigugumizi lakini akajishtukia na kuona kama maelezo yake hayamsaidii Mama!
Huku akielemewa na kelele za chawa wa Mama akaamua kuunga mkono maamuzi.
Hata Mimi niligundua hilo, nadhani amekuwa surprised au ni janja janja yake asieleweke yupo upande gani !
 
Kwa kweli kile kilichofanyika mchana huu ni maajabu.Hata Nyerere pamoja na kuwa na Mamlaka makubwa mno hakudiriki kuburuza wajumbe kiasi hicho.
Jambo hilo litaleta mgogolo ndani ya chama.
CCM hii hakuna wakuweza kuleta mgogoro ndugu, ni kama wamemezeshwa dawa fulani - Yaani ni kama libwata kwenye mapenzi au msukule - hawahoji, hawalalamiki, hawaulizi chochote..
Imagine et mtu anashinda kwa asilimia 100..hata mmoja wa kupinga hayupo..labda kama huyo mtu ni Mungu mwenyewe.
Tanzania tuna-bahati mbaya sana - chama tawala - CCM wanalinda maslahi yao na watu wao na familia zao, CDM ni kama genge la wahuni tu sasa hivi nao, hakuna descpline, hakuna utaratibu, mara rushwa, kusalitiana, ACT - hawa hata hawaeleweki wako wapi..huku ni kama extension ya CCM na serikali huku tena wanajinasibu kama chama tawala etc..hao waliobaki bora wafutwe tu...
Tuna bahati mbaya sana
 
Ccm ni chama , na tasisi ya umma, sio cha mwenyekiti kwa kilichofanyika kamati za kinidham zinatakiwa kukaa na kutoa adhabu ikiwa ni pamoja kuwavua nyadhifa na uanachama wote walioshiriki,
CCM ni mali ya Mwenyekiti huwezi kumfanya kitu chochote Mwenyekiti wa CCM kama ilivyo kwa upande wa Rais wa nchi hata akifanya nini yupo juu ya sheria
 
CCM ni mali ya Mwenyekiti huwezi kumfanya kitu chochote Mwenyekiti wa CCM kama ilivyo kwa upande wa Rais wa nchi hata akifanya nini yupo juu ya sheria
Iko vile bandugu na itabaki kuwa vile mpaka itakapokuwa vinginevyo !!
Hata Mzee wa karibu na Kibaigwa aliyepotea kwenye anga za siasa anajua hivyo ! Mwenyekiti sio mchezo !
😳!
 
Leo huko DODOMA wametangaza rasmi wagombea wa CCM wa nafasi ya rais wa JMT na rais wa Zanzibar.

Kama mnavyojua kwenye siasa hakuna kitu cha bahati mbaya, ni dhahiri huo mpango wa kumpitisha Samia na Hussein Mwinyi kuwa wagombea kwa Kuwashtukiza wanachama ulisukwa mapema. Kwa hiyo hata kikao hiki cha kwenda kumtafuta makamu mwenyekiti kilikuwa zuga tu, lengo lilikuwa ni kumteua rasmi Samia kuwa mgombea wa Urais.

Hii maana yake nini, maana yake Samia kapita bila kufuata mchakato wa kawaida wa chama wa kuchukua fomu kutafuta wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchini. Na Hussein Mwinyi naye kakwepa mchakato wa kumtafuta Mgombea Urais huko Zanzibar. Ule Msemo wa Rais wa Zanzibar anatokea DODOMA Tanganyika umedhihirika leo.

Hiki alichokifanya Samia na kaka yake Hussein Mwinyi ni Kutafuta mteremko wa kisiasa na Unajenga Precedence moja mbaya sana. Sasa hivi wana CCM wajue tu kuwa in the future, hakuna Rais atakayetokana na chama hicho atakayejali hatua za vikao kadha wa kadha, yeye atakuwa anacheza na mkutano mkuu tu , mkutano ukishasema ndiyoooooo, hakuna cha mkutano wa halmashauri kuu wala kamati kuu utakaokuwa na sauti juu ya maamuzi mbalimbali mazito.

Staili hii hii Samia anaweza kuitumia kuilazimisha CCM iridhie ubadilishaji wa katiba kuondoa muhula wa vipindi vya uongozi au kuongeza muda.

Kwa kweli hii staili ya Mbereko, ya kupitisha watu bila kupingwa, ya kutafuta mbereko kwa kukwepa ushindani wa kisiasa ndani ya chama, CCM imeulea yenyewe na sasa madhara yanawarudia wao. Hakuna tena kufuata due process ya kupata wagombea, ni kuwashtukiza wajumbe tu walioshiba ubwabwa, na kulipiwa guest house za kufikia ili watoe sauti za ndiyooooo.

Hii ni disaster.
Leo Samia amekoleza safari ya CCM kujifia, kimegeuka chama cha maigizo, hakuna brainy aspects ya kila move chama hiki kinafanya kwa sasa. Kimegeuka kama chama cha sherehe ya wachoma nyama kula mapande ya minofu ya nchi bila kujali mustakbali wa vizazi vijavyo.

Yetu macho, lakini kwa sasa hakuna chama hapo ni genge la watafuna nchi huku likiwarushia wajumbe makombo ya posho kipindi cha vikao kama hivi vilivyotawaliwa na upambe, uchawa, mob psychology na group thinking.
Kumbe siku hizi CCM hamna suala la kuchukua fomu na kupigiwa kura...ni mwendo wa kusonta tu kidole kisha mtu anapata kura zote za ndio...what a step!, poor Tanzania.
 
Missile of the Nation hoja yako sidhani kama wengi wali iangalia kwa uzito wake. Ni kweli kuna tatizo

1. Mkutano mkuu ulikuwa na agenda ya kuteua Makamu wa Rais Bara.

2. Kulikuwa na hoja ya kuchapisha Fomu 1 ya Urais unaombwa na kuteuliwa na ndivyo ilivyokuwa kawaida

3. Hoja imeletwa kwa kushtukiza katika Mkutano mkuu. Kwa kawaida hoja huanzia vikao vya Kamati kuu, Halmashauri kuu na kuidhinishwa na Mkutano mkuu.

M/kiti Samia anatoa maagizo sekretariati iandae azimio baada ya hoja ya Mkutano mkuu! hapa ni kinyume na taratibu kwasababu Mkutano mkuu huwa ni kauli ya mwisho.

4. Mkutano mkuu umenyima Wanachama walionuia haki yao ya kugombea nafasi ya Urais

5. Consulatation imefanyika ndani ya kikao, kwa maana Kamati kuu na H/Kuu hawana taarifa

Kuna fukuto na tatizo kubwa sana, hii short cut inaashiria walichokifanya ni kukwepa tatizo

Nadhani wanataka kukwepa yale ya Lowassa! wakijua wakati huu kuna udhaifu mkubwa sana.

Pascal Mayalla tusaidie kwasababu wewe ni mwandishi, mwanasheria , mwana CCM na ''Privy''

Mag3 JokaKuu
CCM imefanya jambo jema kabisa, mivutano imekwisha sasa, pia hili litaokoa fedha za chama maana kutakuwa hakuna haja ya kuitisha vikao vingine ambavyo huwa na gharama kubwa kweli it's a cost cut mission thank you mama Samia umawaweza
 
Leo huko DODOMA wametangaza rasmi wagombea wa CCM wa nafasi ya rais wa JMT na rais wa Zanzibar.

Kama mnavyojua kwenye siasa hakuna kitu cha bahati mbaya, ni dhahiri huo mpango wa kumpitisha Samia na Hussein Mwinyi kuwa wagombea kwa Kuwashtukiza wanachama ulisukwa mapema. Kwa hiyo hata kikao hiki cha kwenda kumtafuta makamu mwenyekiti kilikuwa zuga tu, lengo lilikuwa ni kumteua rasmi Samia kuwa mgombea wa Urais.

Hii maana yake nini, maana yake Samia kapita bila kufuata mchakato wa kawaida wa chama wa kuchukua fomu kutafuta wadhamini kutoka mikoa mbalimbali nchini. Na Hussein Mwinyi naye kakwepa mchakato wa kumtafuta Mgombea Urais huko Zanzibar. Ule Msemo wa Rais wa Zanzibar anatokea DODOMA Tanganyika umedhihirika leo.

Hiki alichokifanya Samia na kaka yake Hussein Mwinyi ni Kutafuta mteremko wa kisiasa na Unajenga Precedence moja mbaya sana. Sasa hivi wana CCM wajue tu kuwa in the future, hakuna Rais atakayetokana na chama hicho atakayejali hatua za vikao kadha wa kadha, yeye atakuwa anacheza na mkutano mkuu tu , mkutano ukishasema ndiyoooooo, hakuna cha mkutano wa halmashauri kuu wala kamati kuu utakaokuwa na sauti juu ya maamuzi mbalimbali mazito.

Staili hii hii Samia anaweza kuitumia kuilazimisha CCM iridhie ubadilishaji wa katiba kuondoa muhula wa vipindi vya uongozi au kuongeza muda.

Kwa kweli hii staili ya Mbereko, ya kupitisha watu bila kupingwa, ya kutafuta mbereko kwa kukwepa ushindani wa kisiasa ndani ya chama, CCM imeulea yenyewe na sasa madhara yanawarudia wao. Hakuna tena kufuata due process ya kupata wagombea, ni kuwashtukiza wajumbe tu walioshiba ubwabwa, na kulipiwa guest house za kufikia ili watoe sauti za ndiyooooo.

Hii ni disaster.
Leo Samia amekoleza safari ya CCM kujifia, kimegeuka chama cha maigizo, hakuna brainy aspects ya kila move chama hiki kinafanya kwa sasa. Kimegeuka kama chama cha sherehe ya wachoma nyama kula mapande ya minofu ya nchi bila kujali mustakbali wa vizazi vijavyo.

Yetu macho, lakini kwa sasa hakuna chama hapo ni genge la watafuna nchi huku likiwarushia wajumbe makombo ya posho kipindi cha vikao kama hivi vilivyotawaliwa na upambe, uchawa, mob psychology na group thinking.
Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanaopewa dhamana huahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga wa kuigiza kwa viongozi wao, (unafiki), tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo, a.k.a kujizima data
 
Back
Top Bottom