Habari zenu wanajamii forum popote pale mlipo ulimwenguni!
Jana nilijikuta nawaza juu ya hawa wana ccm waliothubutu kusema mambo yasiyowapendeza uongozi wa juu wa ccm hususani mwenyekiti wake raisi Samia!
Ikitokea Samia akashika madaraka ya nchi tena, je nini kitafuata kwao hawa wana ccm! Maana mpaka sasa sote tunajua Samia ukipishana nae kidogo yanakukuta mazito! Wapinzani wamesulubiwa na wanaendelea kusulubiwa, alimpa kesi ugaidi mbowe kabla ya kumtoa na kumlambisha asali,
Sasa hivi kamtupa Mwenyekiti wa chadema ndugu Lissu mahabusu kwa kesi nzito ya uhaini, vijana kama kina soka, mdude, na wengine wengi hawajulikani walipo! Na mengine mengi ya utekaji na uuaji wa wanaokosoa utawala wake!
Sasa najiuliza kina POLEPOLE na Gwajima wataishi vipi ikiwa huyu mama ataendelea kuwa madarakani, sipati picha.
Ila nawapongeza sana wote wanaosimama kwa ujasiri kumkosoa ama kusema mambo mabaya yanayofanywa na uongozi wa samia.
Nitoe wito kwa watanzania tusimame na hawa wenye ujasiri wa kusema juu ya mabovu ya Samia, maana kuna watu na viongozi wakuu wa sasa ama zamani wanaogopa kukemea uovu sababu wanahofia maisha yao kuharibiwa na Samia!
NB:kama uko upande wa samia usikomenti chochote maana sina mood ya kuhangaisha mwili na akili kujibizana na watetezi wa Samia.