Samia akitoka Dubai kutua moja kwa moja Tanesco Nyakato Mwanza

Samia akitoka Dubai kutua moja kwa moja Tanesco Nyakato Mwanza

Mama Samia akitoka Dubai kuna taarifa ya yeye kutua moja kwa moja Mwanza kisha kuelekea Tanesco Nyakato Mwanza.

Hii inafuatia kutokupata majibu anayoyataka kwa miezi kadhaa sasa.

Ikumbukwe kuwa kituo hicho kina uwezo wa kuzalisha MW 60 kikifanya kazi kwa asilimia mia, lakini kwa miezi kadhaa sasa kimekuwa kikiwasha jenereta moja huku mengine 9 yakiwa yamezimwa.

Kilichomshutua mama ni baada ya kupata taarifa kuwa kituo kikubwa kama hicho kinafanyiwa ukarabati na watu 5 ambao hutumia masaa 4 kwa ajili ya chai na lunch kati ya masaa 8 ya kazi.

Karibu sana mwanza
Dubai amefuata nini cha maana kama sio kuchezea kodi zetu tu
 
Hii ndiyo CCM ninayoijua na hapo kuna RC/RAS/RPC/RSO/DC/DAS/DED/DSO/OCD na Mbunge wote hapo wapo tu
Sisi tulimshauri mama toka mwanzo asiwalee hao watu awakimbize mchakamchaka, yeye akatusagia na nyie nyumbu na chawa mkamshangilia kwa kusema anaupiga mwingi. Matokeo yake ndiyo haya sasa, anasainishwa mikataba ya kistupid, umeme hakuna japo vyanzo vipo, na kila mahali lazima aende yeye kusimamia. Mtamuua kwa presha huyo mama.
 
Shida sio mfumo, shida hapa ni uzembe wa watu,
Unataka nambia Waziri/katibu wa wizara anashindwa solve issue hii?
Kama amei - sovu, huyo Rais anakwenda kufanya nini huko?

Hoja tu kuwa Rais anakwenda kujua kulikoni kati ya genereta 10 za kuzalisha umeme ni 9 tu zinafanya kazi, ni jibu tosha kuwa wameshindwa kutatua tatizo hilo..

Nadhani swali ulilopaswa kuniuliza ni kwanini wote hao wameshindwa kutatua...

Jibu ni hilo: Mfumo mbaya na dhaifu usiosababisha matokeo chanya ktk kutoa huduma kwa wananchi...

Kwa sababu;

1. Ni mfumo uliojaa urasimu kwa sababu mamlaka ya maamuzi yamekuwa centralized kwa mtu mmoja tu anayeitwa Rais. Pengine hata pesa tu za kukarabati mashine hizo mpaka Rais aje atoe maamuzi..!!

2. Je, unajua DG wa TANESCO anawekwa na nani kwenye nafasi hiyo? In case hujui ni Rais ndiye anayemteua! Kama ni hivyo unadhani RC au Mayor au DC na hata Waziri tu (ambaye naye ni mteuliwa tu kama alivyo huyo DG) watamfanya nini DG wa TANESCO zaidi ya kurusha maneno ya kisiasa tu?

## Ndio nikasema kuwa tukitaka kusogeza huduma kwa wananchi kwelikweli, basi ni lazima decentralization of power & authority kwenye local governments ziimarishwe kikatiba. Viongozi wachaguliwe na wananchi na wawajibike kwa wananchi wa maeneo husika Kwa mambo yote ya kiutawala na fedha..

##Nafasi za ma RCs au DCs na ma - DEDs hazipaswi kuwa za kuteuliwa. Hawa wachaguliwe na wananchi wa maeneo husika..
 
Kwani mwanza haijaungwa grid ya taifa? Matumizi ya jenereta ina maana bado wanategemea umeme wa dizeli?
 
Mama Samia akitoka Dubai kuna taarifa ya yeye kutua moja kwa moja Mwanza kisha kuelekea Tanesco Nyakato Mwanza.

Hii inafuatia kutokupata majibu anayoyataka kwa miezi kadhaa sasa.

Ikumbukwe kuwa kituo hicho kina uwezo wa kuzalisha MW 60 kikifanya kazi kwa asilimia mia, lakini kwa miezi kadhaa sasa kimekuwa kikiwasha jenereta moja huku mengine 9 yakiwa yamezimwa.

Kilichomshutua mama ni baada ya kupata taarifa kuwa kituo kikubwa kama hicho kinafanyiwa ukarabati na watu 5 ambao hutumia masaa 4 kwa ajili ya chai na lunch kati ya masaa 8 ya kazi.

Karibu sana mwanza
Mmezidi siasa badala ya kuwajibika kwa wananchi.
Mbona nchi za jirani zetu hawana hizi malalamiko!!
 
Biteko kazi imemshinda inabidi aje Rais mwenyewe.

Tulisema wizara ya nishati ni jumba bovu hata waziri awe nani matokeo ni Yale Yale. Huwezi pata umeme mkubwa wakati una vyanzo vidogo. Hili sio swala la kisiasa ni science.
 
🤣🤣mama fika mwanza,Kuna uozo mwingi ofisi za serikali, halmashauri zote zimeoza,watu wanafanya kazi kwa mazoea,na wengine wamejigeuza miungu watu,wanasema wao ni wazawa,Wana miaka zaidi ya kumi kituo kimoja,wamegeuza ofisi za Umma Kama ofisi binafsi
Anzia ilemela,nyamagana, Misungwi,yamejaa mafisi na kazi haizendi sababu ya urasimu na uenyeji,fumua mkoa wa Mwanza mama ,utanishukuru🙏
 
Huyu mama alipe kwanza hela za wadau kwa wakati...unasupply mzigo wa zaidi mil500 kwenye taasisi ya serikali, umekopa kwa producers mzigo mali kauli alafu mama anakuwekea mil2 ndani ya mwezi mzima si ni kifiro icho??
 
Kuna mfanyakazi namfahamu ambaye ni fundi wa hicho kituo huwa anakesha Bar hadi asubuhi kwa siku za kazi. Najiulizaga hivi akienda kazini na hizo pombe zake anafanyaje kazi!!!. Na je hamnaga viongozi kwenye hicho kituo mpaka mtu aende kazini kalewa!!.? Au viongozi wao nao ndio walewale.?.
Hawa watendaji wa ngazi za chini ndio wanaborongoga na kufanya serikali ionekane haifanyi kazi. Si vyema matatizo yanayoweza kutatuliwa na watendaji wa chini Rais aje kuyatatua.
 
Tanesco kumejaa uchafu mwingi sana,wanaishi nyumba ya muda sana ..kuna miji mikubwa huko kusini haina huduma ya umeme wa uhakika ni mgao wa masaa 6 kuwasha 6 kukata
 
Mama Samia akitoka Dubai kuna taarifa ya yeye kutua moja kwa moja Mwanza kisha kuelekea Tanesco Nyakato Mwanza.

Hii inafuatia kutokupata majibu anayoyataka kwa miezi kadhaa sasa.

Ikumbukwe kuwa kituo hicho kina uwezo wa kuzalisha MW 60 kikifanya kazi kwa asilimia mia, lakini kwa miezi kadhaa sasa kimekuwa kikiwasha jenereta moja huku mengine 9 yakiwa yamezimwa.

Kilichomshutua mama ni baada ya kupata taarifa kuwa kituo kikubwa kama hicho kinafanyiwa ukarabati na watu 5 ambao hutumia masaa 4 kwa ajili ya chai na lunch kati ya masaa 8 ya kazi.

Karibu sana mwanza
Hii tukubali tu CCM hawawezi.
 
Back
Top Bottom