The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Katika hukaha, kutapatapa na kuhanyahanya, Samia aliunda timu, siyo tume ya maridhiano.
Kwanza, anaridhiana na nani?
Pili, pesa ya kuendesha zoezi hili inatoka kwenye bajeti gani?
Tatu, ni kiasi gani?
Nne, ina faida gani?
Tano, je, walengwa nni nani?
Sita, kupata wajumbe, ametumia vigezo gani na kwanini?
Saba, je, wana udhu wa kutosha au wanatumika tu kuhalalisha haramu?
Nane, yeye na wateule wake wana uhusiano gani?
Tisa, nini hadidu zake za rejea?
Kumi, je, kuunda timu ndilo jibu sahihi na mujarabu?
Kumi na moja, ikishindwa itakuwaje na fedha zetu zitarudishwaje?
Kumi na mbili, nani ataitathmini utendaji wake?
Tuchunge tusijeingizwa mkenge mchana kweupe.