GE2025 Samia: Awali hatukufanya haki kwenye kugawana ardhi, kiwanja kimoja kinamilikishwa watu watatu watatu

GE2025 Samia: Awali hatukufanya haki kwenye kugawana ardhi, kiwanja kimoja kinamilikishwa watu watatu watatu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
"Awali hatukufanya haki kwenye kugawana ardhi, kiwanja kimoja kinamilikishwa watu watatu watatu hasa hapa Dar Es Salaam, Migogoro ya ardhi unakuta shamba la mtu huyu anapewa hati mtu mwingine, lakini haya yote sasa yameondoka, ardhi yetu tumeipima, tunaendelea kuipima na kama mmesikia nilisema kwa miaka mitano ijayo tunakusudia pia kuipima ardhi ya Tanzania, kubaini maeneo yenye madini ili tuyajue na tujipange kuyavuna ili kukuza uchumi wetu." Amesisitiza Dkt. Samia.

Samia ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Oktoba 23, 2025 wakati wa Mkutano wake wa Kampeni kwenye Viwanja vya Tanesco Buza, Wilayani Temeke Mkoani Dar Es Salaam,

 
Ina maana upimaji Ardhi ni Kwa ajili ya kutafuta madini na sio Kwa ajili ya mipango miji ya kisasa ya kuishi wananchi.

Na hayo madini watayachimba waarabu au wa TZ ili wayachakate na kuyauza kwa bei nzuri

Ofisi ikulu , hotuba za raisi mbona Zina mapungufu sana , Muna fanya hivi ili kumdhalilisha ?.

Yan hotuba za raisi ni vituko na viroja, hotuba zinazo acha maswali mengi bila majibu kwa wananchi.

Inasikitisha sana
 
Mungu ni mkubwa sana sana. Anasema haya bila kuwaza ila haya ndio malengo yake ya dhati. Hapo ni kweli wanakwenda kuyavuna hayo madini mpaka tubakizwe watupuuuu. Tusipotoka 29, imekula kwetu..
 
Mungu ni mkubwa sana sana. Anasema haya bila kuwaza ila haya ndio malengo yake ya dhati. Hapo ni kweli wanakwenda kuyavuna hayo madini mpaka tubakizwe watupuuuu. Tusipotoka 29, imekula kwetu..
Kwahiyo kwako ulitaka madini yasivunwe au?
 
Back
Top Bottom