King Kong III
Platinum Member
- Oct 15, 2010
- 64,227
- 98,761
Heche ,Maria Sarungi ,Mshabaha ,Diaspora wote wanaopiga spana kazeni hivyo hivyo wanaelekea kutema BUNGO.Watu wanadai kikundi kinachoteka na kupoteza watu alikiunda yeye ili kulinda kiti dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa. RIP Polepole.
Watu wanadai aliyetoa amri ya kupiga risasi za moto wananchi wanaoandamana ni yeye.
Aliyeteua kiongozi wa tume huru ya Uchaguzi ambayo ndo iliharibu uchaguzi ni yeye.
Aliyeenda kuapishwa kambi ya jeshi ni yeye.
Aliyebambikizia kesi ya Uhaini Lissu ni yeye.
Ilidaiwa watu walioua walitoka Uganda.
Hata hivyo hiyo tume kasema ni yake. Yeye ndo anajiita rais.(Tume ya Rais ya Uchunguzi).
Sisi tunataka tume ya mahakana, Ambayo matokeo yake yanakuwa kwa Wananchi. Hii ya Samia ni yake na matokeo ya Uchunguzi ni yake. Nyie mtapewa hadidu rejea na kutaja majina ya wapinzani wake ili kuwanyong'onyesha.
Kasema Jaji katoka SADC kusema kweli SADC haijahusishwa bali ni baada ya yule mama kuja Tanzania ndo akamuomba mtu wake.
Kataja East Africa Community imetoa jaji ni uongo, Jaji kapewa na Mseven ambaye hataki kutoka madarakani.
Basi angewaandikia SADC na EAC wwampe majaji. Ndo maana hujaona SADC representatives. Yeye amewataja sadc iili kuhadaa watu na kujivika ngozi ya kondoo.. Dunia ya sasa si zamani.. Siasa zimebadilika.. CCM wamezoea uonho uongo.
Kashazoea uraghai
KUMBUKA
Tulikataa Wachunguzi wa kimataifa kwa kigezo haya ni mambo yetu ya ndani! Hawa wa uganda na Namibia wa kazi gani?
Mtabana mtaachia.
Hakuna maridhiano mpaka wale walioua ndugu zetu Oct 29 mpaka 03 Nov 2025 wachukuliwe hatua.
Genge la utekaji livunjwe na washitakiwe kwa mauaji ya Kina Polepole,mdude,chaula,ben saanane ,rwajabe,kanguye,azory na wengineo wengi - Justice ipatikane kwanza.