Samia kapitishwa kimakosa kugombea urais. Katiba ya CCM haikufuatwa

Kwanza tuelezwe na Nchimbi na timu yake zile shilingi millioni Samia alikua anachangiwa kuchukua fomu ya chama kugombea kuteuliwa kugombea urais zimeenda wapi.

Hilo ni jambo linaonyesha kuna taratibu za chama ukitaka kugombea uteuliwe kua mgombe urais. Nchimbi ameongoza uhuni kwa kukiuka utaratibu na katiba ya CCM. Ni haki kwenye katiba ya CCM mwanachama yeyote mwenye kutaka kugombea urais kupewa haki hiyo.

Hili lilotokea Dodoma kwa kuwalaghai watanzania na hasa wanaCCM eti kikao kilichoitishwa cha mkutano mkuu ni kwenda kujaza nafasi wazi ya makamu mwenyekiti na kupokea taarifa za utendaji wa serikali kisha kushtukizwa kumchagua Samia mgombea urais ni uhuni mtupu.

Nchimbi kwa hilo akazawadiwa kua mgombea mwenza. WanaCCM tusikubali chama kunajisiwa.
WanaCCM tusikubali na tudai mkutano mkuu wa kuteua mgombea urais muda utakapofika uitishwe huu uhuni usitishwe wanachama waweze kupewa haki kugombea na kupata mgombea wanayomtaka.
Mhe. Rais Samia kapiga hat-trick; tumepata mgombea Urais wa Muungano, Zanzibar na Mgombea Mwenza wa Muungano. Pia, sielewi Mhe. Dk. Nchimbi kosa lake nini wakati hoja ilianzia kwa wajumbe kutaka utekelezaji . Nilidhani tuwapongeze viongozi wakuu wa CCM kuwa wasikivu #Nimeipenda hat-trick ya kwanza kwa mwaka 2025.
 
Saa 100 anaogopa hata kivuli chake ......anaogopa mitihani ndio hulka yake ....
 
Msajiri yupo wapi Sheria zinataka mgombea kabla hajapitishwa na chama aende majimboni kupata saini za wapiga kura
 
Chama Cha kijani na utapeli ni kama Pete na kidole. Wanalumumba poleni na hongereni kwa kutapeliwa kwa mara nyingine.
 
Mhe. Rais Samia kapiga hat-trick; tumepata mgombea Urais wa Muungano, Zanzibar na Mgombea Mwenza wa Muungano. Pia, sielewi Mhe. Dk. Nchimbi kosa lake nini wakati hoja ilianzia kwa wajumbe kutaka utekelezaji . Nilidhani tuwapongeze viongozi wakuu wa CCM kuwa wasikivu #Nimeipenda hat-trick ya kwanza kwa mwaka 2025.
Mkutano ulikuwa wa kumchagua mrithi wa Kinana. Huyu mrithi wa Mipango si angesubiri atakapo jiuzulu.
 
Jana nimeandika CCM wamevunja ibara ya 100 (5) c ya katiba ya CCM ya 1977 toleo la Disemba 2022.
Unaweza kutuweka hapa maelezo yake , tuone kama Sharia za mirathi zimefuatwa.
 
downloadfile.jpg
 
Unaweza kutuweka hapa maelezo yake , tuone kama Sharia za mirathi zimefuatwa.
Katiba ipo online, hata mimi nimei Google nikaipata kama PDF online.

Katiba ya CCM ya 1977, toleo la Disemba 2022.
 
Fuata ninavyo kwambia. Usifuate ilivyoandikwa. Kauli ilitoka kwenye mkutano mkuu mmoja wa CCM akijibiwa mjumbe aliyetaka katiba ifatwe.
 
Kwanza tuelezwe na Nchimbi na timu yake zile shilingi millioni Samia alikua anachangiwa kuchukua fomu ya chama kugombea kuteuliwa kugombea urais zimeenda wapi.

Hilo ni jambo linaonyesha kuna taratibu za chama ukitaka kugombea uteuliwe kua mgombe urais. Nchimbi ameongoza uhuni kwa kukiuka utaratibu na katiba ya CCM. Ni haki kwenye katiba ya CCM mwanachama yeyote mwenye kutaka kugombea urais kupewa haki hiyo.

Hili lilotokea Dodoma kwa kuwalaghai watanzania na hasa wanaCCM eti kikao kilichoitishwa cha mkutano mkuu ni kwenda kujaza nafasi wazi ya makamu mwenyekiti na kupokea taarifa za utendaji wa serikali kisha kushtukizwa kumchagua Samia mgombea urais ni uhuni mtupu.

Nchimbi kwa hilo akazawadiwa kua mgombea mwenza. WanaCCM tusikubali chama kunajisiwa.
WanaCCM tusikubali na tudai mkutano mkuu wa kuteua mgombea urais muda utakapofika uitishwe huu uhuni usitishwe wanachama waweze kupewa haki kugombea na kupata mgombea wanayomtaka.
CCM mna kazi kubwa ya kuwa chama chenye demokrasia.
 
Back
Top Bottom