Samia na Mbowe hand shaking.: Je hii ni dhihaka, dharau na kejeli dhidi ya CHADEMA na Tundu Lissu?

Samia na Mbowe hand shaking.: Je hii ni dhihaka, dharau na kejeli dhidi ya CHADEMA na Tundu Lissu?

Kwahiyo Mbowe ndio kamweka ndani Lissu ?.
Lissu amekaa gerezani miezi mitatu only.
Mbowe amekaa gerezani miezi nane,leo unamwita Msaliti ?.
Mbowe mashamba yake na biashara zake zimevurugwa leo unamwita msaliti kwasababu kaudhuria uzinduzi wa dira ya maendeleo !.

Wakati Mbowe anatukanwa anabagazwa anachafuliwa kwa kila aina ya matusi mlikaa kimya mkiwasifu wachafuaji.
UWezi kuniweka ndani miezi nane bila kosa hata uwe malaika sishikani mikono na wewe hiyo kazi wanaiweza wanafiki tu.
 
Wanafanya spinning ya matukio. Juzi ilikuwa Polepole, akawa Lissu mahakamani, akawa Gwajima jana.. so wanataka tusahau yote hayo. Wimbo mpya uwe ni Mbowe na Dira ya taifa .
 
Manakumbuka kipindi cha kesi ya COVID 19, walipoitwa kuhojiwa HALIMA MDEE alimvaa Mwenyekiti wake akamwambia hata wewe Mwenyekiti unajufanya ujui mwenyekiti akazugazuga pale,

Magu alipoona wanataka mshika shrubs akapiga pin no ruzuku no nini kudadedi wakaona hapa nikukimbia tu
Mbowe alikataa kupokea ruzuku. Hakuwahi kunyimwa ruzuku.

Amandla...
 
FAM alikuwa anatudanganya tukaandamane kumbe ni script anasoma!

Wale vijana wamepotea wengine wamekufa jamaa anazuga kuwaongelea kumbe yuko kinyume nao?

Mdude?kibao?...Mbowe ni mnyama na katili sanaa!
Mbowe aliita maandamano kshinikiza serikali kuhusu vifo vya wakina na kupotea kwa wengine. Akatokeza binti yake peke yake. Katibu Mkuu wake akaenda kujificha kwa masista na Makamu Mwenyekiti wake akalala nyumbani kwake huku ikijulikana wazi kuwa hatua ya kwanza itakayochukuliwa ni kuzingira nyumba yake.

Mdude amepotea wakati wa uongozi wa wakina Lissu. Lema anasema kuna wengine wengi tu wamepotea. Uongozi wa sasa umechukua hatua gani kuishinikiza serikali kutoa majibu kuhusu hatma yao? Umebaki kumlaumu Mbowe.

Amandla...
 
..lakini Lissu alimtetea Mbowe.

..Na alisafiri nchi mbalimbali za ulaya kumsemea Mwenyekiti wake.

..mara alipokutana na Rais Samia Ubelgiji, Lissu alisema amemueleza Rais kuwa Mbowe hana hatia.
Na Mbowe alihakikisha Lissu hatibiwi Tanzania. Inaaminika kuwa kufanya vile kuliokoa maisha ya Lissu.

Wakati Lissu anampigania Mbowe akiwa nje ya nchi wakina Catherine Ruge hawakuchoka kumpambania on the ground. Wamekaa sana mahabusu kwa ajili ya Mbowe. Leo wanaitwa wasaliti. Go figure.

..uchaguzi umekwisha, na kila mwanachama anapaswa kukipigania chama, na kuwatetea viongozi wake.
 
Katika mazingira ambayo, Tundu Lissu, mwenyekiti wa Chadema yupo gerezani akishtakiwa kwa makosa ya uhaini (ambapo ikiwa atatiwa hatiani hukumu yake itakuwa ni kunyongwa hadi kufa) huku dunia nzima ikilaani kukamatwa kwake na kupiga kelele aachiwe huru mara moja, na hapo hapo CHADEMA ikiwa imezuiliwa kufanya shughuli zake zote za siasa nchi nzima,

Mwenyekiti mstaafu wa Chadema na mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya Chadema, Freeman Mbowe ameibuka katika tukio la uzinduzi wa dira ya taifa ya 2050 akiwa kama 'mgeni mtarajiwa mahususi', na kupiga picha huku akiwa na tabasamu zito la bashasha na akishikana mikono na Rais Samia Suluhu ikiwa ishara ya kuunga mkono juhudi zote za mama Samia!

Kitendo hicho huenda kinatoa tafsiri ya moja kwa moja kama dharau, kejeli na kebehi kubwa zaidi kwa Chadema iliyo chini ya Tundu Lissu. Kwa sasa huenda Mbowe anatafsiriwa na kuonekana ni msaliti namba moja dhidi ya CHADEMA na harakati zote za kupambania mabadiliko chini ya vugu vugu la No Reform, No Election.

Baadhi wa wadadisi wanasema, huenda siku ya leo itakuwa imeandika historia nyingine katika siasa za mageuzi hapa Tanzania kwa kupata mtu atakayesimama kama alama ya kudumu ya usaliti wa siasa za mageuzi hapa Tanzania.

Soma Pia: Freeman Mbowe apata picha ya kipekee na Rais Samia

Hatua ya leo huenda ikawa ndio mwanzo wa hatua mbili zingine zinazotarajiwa kufanywa na Freeman Mbowe wiki chache zijazo, ambazo duru za ndani zinasema Mbowe anategemewa kujitoa Chadema ili kuhamia rasmi CHAUMMA na kubeba jukumu la kugombea urais kupitia chama hicho.

Muda ni mwalimu mzuri.

Mwenyekiti mstaafu wa Chadema na mjumbe wa kudumu wa kamati kuu ya Chadema, Freeman Mbowe ameibuka katika tukio la uzinduzi wa dira ya taifa ya 2050 akiwa kama 'mgeni mtarajiwa mahususi', na kupiga picha huku akiwa na tabasamu zito la bashasha na akishikana mikono na Rais Samia Suluhu ikiwa ishara ya kuunga mkono juhudi zote za mama Samia!
 
Manakumbuka kipindi cha kesi ya COVID 19, walipoitwa kuhojiwa HALIMA MDEE alimvaa Mwenyekiti wake akamwambia hata wewe Mwenyekiti unajufanya ujui mwenyekiti akazugazuga pale,

Magu alipoona wanataka mshika shrubs akapiga pin no ruzuku no nini kudadedi wakaona hapa nikukimbia tu
🤣🤣🤣🤣🤣😁
 
Mimi siku ya maandamano alipoonekana na kukamatwa yeye na mwanae nilimtilia mashaka sana na mashaka yangu yamedhihirika leo.itatuchukua muda mrefu kupata wapinzani wa kweli.wengi wao ni watu wa mfumo.imeonekana upinzani uko juu wameona wamtumie sasa kijana wao kama alivyotumika Lipumba kuimaliza CUF.umemsikia Lipumba? yupo kimya anakula keki ya Taifa.
Naam Jamaa wanakuwaga undercover wale Mrema lipumba Huyu DJ ni watu wa mfumo
 
Mwamba alimchukia sana JPM maana hakumpa nafasi kama hizi na zile za kunywa juisi ikulu
Alimnyoosha kisawa sawa lakini pia Kuna time walipiga deal pamoja siasa hainaga adui wa kudumu wale covid 19 Mzee DJ alipewa mihela kibao ili kuruhusu kupitishwa Kwa ule mchakato
 
Muda ni mwalimu mzuri.
EEEEeeenHEEEEeenHEEEE!

Mimi nimesoma hiyo picha tu inayo andamana na mada. Ni picha moja yenye taarifa mbalimbali.

Hebu iandgalie tena kwa makini hiyo icha ya hao watu wawili.

Tanzania kweli ni nchi ya kuwa na viongozi wa namna hii, jamani?
 
Back
Top Bottom