Samia Scholarship ni uwekezaji wenye tija

Samia Scholarship ni uwekezaji wenye tija

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Rais wetu Mama Samia ametoa udhamini wa wanafunzi 600 katika elimu ya juu waliofanya vizuri masomo ya sayansi, sina hakika kama watanzania wengi wanalifahamu jambo hili jema kiasi hiki, maana elimu ni mti wenye mizizi mirefu sana, majani mengi na matunda yenye mbegu nyingi zisizohesabika idadi yake. Hili ni miongoni mwa yale mambo mema ambayo kiongozi wa nchi anaweza kufanya. Tumpongeze kwa hili pia kwakuwa amefikiria mbali zaidi.

Kazi kubwa iko kwa watendaji wetu wenye dhamana ya kuchagua ni mtoto yupi apate na yupi akose kwa uadilifu na haki.

Sio jambo la kushangaza kuona watu wengi wa kanda fulani, dini fulani, kabila fulani na chama cha siasa fulani na shule fulanifulani tu na kuwaacha wale waliostahili. Mfano, kumpa scholarship mtoto aliyesoma shule za FEZA, Marian, Mazinde juu walikosoma watoto wao na kumuacha yule mtoto aliyesoma Korogwe, Jangwani, Msalato, Benjamin Mkapa au King'ong'o, Iliboru kisa kapitwa ufaulu na waleee wa kwao. haitakuwa sawa hata kidogo mbele ya macho ya Mungu. Itakuwa sawa na TFF kuruhusi timu isajili wachezaji 12 wa kigeni washindanie namba na wazawa.

Watoto waliosoma shule hizi za wananchi na kufaulu vizuri ndio wanaostahili zawadi hii ya Rais wao. Ni njia ya kuonyesha uzalendo kwa shule zetu hizi za watoto wa wamachinga na wauza vitumbua.

Ni maoni yangu tu.

Msikilize Waziri mwenye dhamana ya elimu.
 
Samia scholarship ni mpango wa serikali ya awamu ya sita kuwafadhili wanafunzi 600 wanaomaliza kidato cha sita wenye ufaulu mzuri wa masomo ya sayansi, hii itachochea ufaulu mzuri wa masomo kwa wanafunzi wa Tanzania.

Mwamafunzi akienda kusoma chuo kikuu masomo ya Sayansi, Uhandisi, Elimu Tiba ana Full Scholarship Analipiwa Gharama Zote Za Kusoma Sio MKOPO Mpaka Amalize Masomo yake.

Rais Samia Suluhu Hassan anakuja na mikakati mbali mbali ya kutimiza lengo lake la kujenga Tanzania ya wasomi anastahili pongezi .
 
Jambo zuri sana ila nikipata nafasi ya kumshauri, ningemshauri kuwa hii scholarship isiwe kwa waliofaulu Sana iwe kwa wale Watoto maskini waliofaulu Ila hawana vigezo vya kupata mkopo.
Waliofaulu sana wana uhakika wa kupata mkopo na scholarship nyingi za aina nyingine.
 
..Samia Scholarship wakati ni fedha za masikini walipa kodi na tozo wa Tz.

..Kwanini inatangazwa kana kwamba ni ufadhili unaotokana na fedha binafsi za Ssh?
Utadhani anatoa mshahara wake mwenyewe, bora wangesema ni ufadhili wa serikali
 
Jambo zuri sana ila nikipata nafasi ya kumshauri, ningemshauri kuwa hii scholarship isiwe kwa waliofaulu Sana iwe kwa wale Watoto maskini waliofaulu Ila hawana vigezo vya kupata mkopo.
Waliofaulu sana wana uhakika wa kupata mkopo na scholarship nyingi za aina nyingine.

Na iwe ni nje ya nchi ili kuleta utaalamu tofauti ndani. Zaidi wangekazania kwenye kozi kama computer science na zinazohusiana na technology
 
Sasa mtoto wa masikini anatakiwa ajitahidi sana kusoma ili apate scholarship maana hii haijamlenga tajiri wala masikini lakini kwa atakaefaulu vizuri
 
Na iwe ni nje ya nchi ili kuleta utaalamu tofauti ndani. Zaidi wangekazania kwenye kozi kama computer science na zinazohusiana na technology
Kwanini nje ya nchi hata Tanzania tunaweza chini ya Rais Samia Suluhu elimu imeboleshwa sana
 
Jambo zuri sana ila nikipata nafasi ya kumshauri, ningemshauri kuwa hii scholarship isiwe kwa waliofaulu Sana iwe kwa wale Watoto maskini waliofaulu Ila hawana vigezo vya kupata mkopo.
Waliofaulu sana wana uhakika wa kupata mkopo na scholarship nyingi za aina nyingine.
Wazo zuri mkuu
 
Kigezo ni kufaulu vizuri hayo masomo ya historia za SAYANSI

Under philosophical point of view; science is all about discoveries, innovation, creativity and likewiseness. Hivi kwanini huwa hatuwajali wala kuwafadhiri wale walau walioonesha wapo kwenye mlengo huo?

Hivi kumfadhiri mtu alieweza kukariri au kukumbuka kile alichokaririshwa ni kuinua vipaji vya watoto au kutoa promotion for those who are in front lines kwenye hizo shule za wenye nacho??

Ningeweza kushauri labda tubadilike zitengenezwe jukwaa za kutafuta hawa innovators, discovers and those who can create something. Mkishawapata wapewe sasa hizo hands-on scholarships

Hawa wanafunzi wa kukariri historia za SAYANSI wazee wenzangu hatutofika
 
Walewale walamba asali wanagawana keki kwa namna ya kipekee.
ninachoamini mimi ni kwamba, hawa waliopewa scholarship wanauhakika wa kupata mkopo kutoka HESLB.
ushauri wangu scholarship hii ingelenga kuwasaidia watoto wanaotoka shule za serikali ambao wengi wao wana uchumi unaochechemea.
 
Kitu cha ovyo kupata kutokea, hapo watajazana watoto wa viongozi tu
 
Yaani mm sijaona lengo la hiii scholarship kwa maana watakao faulu weeng ni wale wale wanaojiweza kina feza,marian.n.k.....lengo la mkopo ni kusaidia wale wenye uwezo wa chini kujiiinua kwa kiasi chake vitu vingine vinafanyika kwa kuyokuwa na proper planning and organisation ulopita
 
Sijui kama mama anakifahamu hiki wanachokifanya akina Mkenda. Yaani wamewatafutia nafuu wale wenye uwezo wa kulipa. Watoto wao ndio watakaopata Samia scholarships na watakaoingia vyuo vya serikali vyenye ada nafuu.

Wanamzuga mama kwa kumwambia kuwa 65% ya watoto waliopata scholarships wanatoka shule za serikali, lakini hawamwambii kuwa hao wanaotoka shule za serikali walimaliza form kutoka shule gani. Ukweli ni kwamba haya mafisadi yalipeleka watoto wao private za msingi na sekondari hadi form 4, kisha wakapata nafasi ya kwenda shule nzuri za serikali kusoma form 5 na 6 na Sasa ndio hao kwenye 65% ya waliotoka shule za serikali. Hapa maana yake Rais amedanganywa kwa mara ya pili.
 
Ni initiative nzuri..lakin kulikuwa na haja ya kuuita Samia Scholarship? Au ni kumfanya mtu afurahi tu.
 
Samia scholarship ni mpango wa serikali ya awamu ya sita kuwafadhili wanafunzi 600 wanaomaliza kidato cha sita wenye ufaulu mzuri wa masomo ya sayansi, hii itachochea ufaulu mzuri wa masomo kwa wanafunzi wa Tanzania.

Mwamafunzi akienda kusoma chuo kikuu masomo ya Sayansi, Uhandisi, Elimu Tiba ana Full Scholarship Analipiwa Gharama Zote Za Kusoma Sio MKOPO Mpaka Amalize Masomo yake.

Rais Samia Suluhu Hassan anakuja na mikakati mbali mbali ya kutimiza lengo lake la kujenga Tanzania ya wasomi anastahili pongezi .
Kwa mara nyingine tena Wajanja wamebuni mpango wa kujisaidia wenyewe kwakua hawa waliopata ufadhili kupitia Samia scholarship ni watoto ambao wengi wao walisoma masomo ya sayansi, yaani PCM, PCB na EGM. Watoto na wazazi walijuwa kuwa 98% ya watoto ambao wanasoma masomo ya sayansi (physics, Chemistry, Biology, Hesabu, Agriculture, Zoology kule A' Level moja kwa moja wanalenga kwenda kusoma kozi za sayansi kule vyuo vikuu, hivyo sio kweli kuwa Samia scholarships zingewavutia watoto hawa kwenda kusoma fani za sayansi, kwakuwa kwa kusoma tahasusi za sayansi kule sekondari tayari walishaamua (narrow) kusoma kozi za sayansi huko mbele ya safari vyuo vikuu, hivyo Samia Scholarship sio kwaajili ya mtoto bali ni kwaajili ya mzazi kupunguziwa gharama za kumsomesha mwanawe ambae tayari walishaamua na mwanawe kusoma masomo ya sayansi ili hatimae wasome kozi za sayansi chuo kikuu.

Dhambi iko wapi hapo? Dhambi inakuja pale Samia scholarship inapogharamia hata wale watoto waliosoma shule za ada kubwa, automatically watoto hawa wana nafasi ya kusoma vyuo vikuu kozi za sayansi hata bila Samia scholarship wala mkopo. Hii maana yake imekwenda kupunguza uwezo wa watoto masikini kupata msaada wa kusoma vyuo vikuu kozi za sayansi.

Ikumbukwe kuwa 90 ya wanafunzi wanaosoma A' Level shule nzuri kama tabora boys, tabora boys, Kilakala, dakawa, Msalato, Iliboru, nk ni watoto ambao wamesoma shule za private za msingi na sekondari (O' Level) na kuchaguliwa kwenda hizo shule za vipaji maalum,

Hii maana yake ni nini?: Ina maana kuwa elimu itakuwa kwa watoto wa tabaka fulani tu, kwakuwa watoto wanaosoma hizi shule binafsi zenye walimu na mazingira mazuri ya kusoma ndizo zinazotoa watoto wenye ufaulu mkubwa wa kuweza kupata Samia scholarships, kuchaguliwa vyuo vya serikali vyenye ada nafuu na kupata mikopo pia. Hili ni kundi la watoto ambalo wazazi wao wana uwezo mkubwa wa ku lobby kwenye bodi ya mikopo na taasisi za fedha ili watoto wao wapate mikopo au ufadhili.

Samia scholarship ungebaki kuwa mfuko wa wanyonge tu waliofanya vizuri darasani kwenye masomo ya sayanzi, na hii ndio njia madhubuti ya kupunguza pengo kati ya wenye nacho na wasio nacho nchini.
 
Back
Top Bottom