kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Rais wetu Mama Samia ametoa udhamini wa wanafunzi 600 katika elimu ya juu waliofanya vizuri masomo ya sayansi, sina hakika kama watanzania wengi wanalifahamu jambo hili jema kiasi hiki, maana elimu ni mti wenye mizizi mirefu sana, majani mengi na matunda yenye mbegu nyingi zisizohesabika idadi yake. Hili ni miongoni mwa yale mambo mema ambayo kiongozi wa nchi anaweza kufanya. Tumpongeze kwa hili pia kwakuwa amefikiria mbali zaidi.
Kazi kubwa iko kwa watendaji wetu wenye dhamana ya kuchagua ni mtoto yupi apate na yupi akose kwa uadilifu na haki.
Sio jambo la kushangaza kuona watu wengi wa kanda fulani, dini fulani, kabila fulani na chama cha siasa fulani na shule fulanifulani tu na kuwaacha wale waliostahili. Mfano, kumpa scholarship mtoto aliyesoma shule za FEZA, Marian, Mazinde juu walikosoma watoto wao na kumuacha yule mtoto aliyesoma Korogwe, Jangwani, Msalato, Benjamin Mkapa au King'ong'o, Iliboru kisa kapitwa ufaulu na waleee wa kwao. haitakuwa sawa hata kidogo mbele ya macho ya Mungu. Itakuwa sawa na TFF kuruhusi timu isajili wachezaji 12 wa kigeni washindanie namba na wazawa.
Watoto waliosoma shule hizi za wananchi na kufaulu vizuri ndio wanaostahili zawadi hii ya Rais wao. Ni njia ya kuonyesha uzalendo kwa shule zetu hizi za watoto wa wamachinga na wauza vitumbua.
Ni maoni yangu tu.
Msikilize Waziri mwenye dhamana ya elimu.