Samia Suluhu baada ya kutembelea ziara Korea Kusini, wamarekani watoa uzushi

MTANZANIA620

Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
65
Reaction score
81
Na Bollen Ngetti
0683 226539
B-pepe bollenngeti@gmail.com

SIKU tatu kabla Rais Samia Suluhu Hassan hajaelekea Korea Kusini kuhenyea kwa ajili ya nchi yake niliandika huko kwa Max (X) kwamba, "Rais Samia unaenda Korea Kusini lakini jiandaye na matusi, kejeli , dhihaka na hata uzushi kutoka Marekani".

KWELI, Rais Samia Suluhu Hassan amefika Korea na kufanikisha dili la mkopo wa Shilingi 6.57 Trilioni wa sharti nafuu ikiwamo riba ya 0.01% kwa muda wa miongo 4 inayoanzia 2026. Fedha ambayo itaelekezwa katika miradi ya kimkakati inayolipa kama sekta ya usafirishaji na uchukuzi!

Mara baada tu ya Rais kufanikisha jambo letu HIMA Marekani kupitia sauti yake, Voice of America, VoA ikaandika uzushi, dhihaka na matusi kwamba, "Tanzania imesaini mkopo wa fedha na Korea Kusini kwa sharti la kugawa sehemu yake ya bahari na madini". Ujinga uliovuka mawingu!

Hivi, katika hali tu ya kawaida Rais Samia ni mwendawazimu, mjinga, asiye na akili wala uzalendo kiasi gani hadi atoe sadaka ya sehemu ya bahari na madini yetu kwa gharama ya mkopo ambao bado tutailipa? Kwa nini isingekuwa mbadilishano wa hayo matrilioni na kipande cha bahari na madini ili lojiki iwepo? Yani unaenda kwa Mangi unamwambia akukopeshe mchele wa kilo 50 kwa ajili ya shughuli ya binti yako utamlipa mwisho wa mwezi na hapo hapo unamwambia njoo nyumbani nikupe fremu bure pamoja na kwamba mchele wako nitakulipa mwisho wa mwezi! VoA na Joseph Biden mmetukosea sana kwa ujinga huu. We can be stupid but not fool to that extent!

Watanzania tuelewe mambo mawili hapa kama si moja kubwa! Na atakayeelewa awaeleweshe wengine 10 wasio na smart phones. Kwanza kuna vita kubwa ya kiuchumi duniani. Kila Taifa linatumia kila aina ya mbinu halali na haramu kujiweka sawa kiuchumi maana uchumi ndio kila kitu.

Na moja ya mbinu ya mataifa makubwa ni pamoja na kudhoofisha nchi zingine kiuchumi, kiteknolojia na ikibidi hata kisiasa na kijeshi. Marekani kupitia shirika lake la kijasusi ilitumia kila mbinu chafu kuwatenganisha ndugu wa tumbo moja KOREA ikazaliwa Korea Kusini na Korea Kaskazini huku USA ikilalia Korea Kaskazini na kumuona Korea Kusini kama "nunda" na adui. Korea Kusini imewekewa vikwazo chungu nzima na Marekani hasa katika eneo la ubunifu wa teknolojia ya zana za kivita bila mafanikio.

Wananchi wa Korea Kusini waliamua kushikamana na kujenga uzalendo kwa nchi yao wa kupigiwa mfano baada ya kuona, "hatuna ndugu wala mjomba, lazima tujikomboe wenyewe" na pakwanza walipoanzia na kupambana na kushinda saratani ya rushwa na ufisadi na kumtambua kila Mkorea Kusini alipo ndani na nje ya nchi yao na anafanya nini kwa maslahi ya Korea Kusini!

Nimkumbushe Mtanzania jambo ambalo limewahi kutokea lakini haikuandikwa popote na kokote rasmi! Miaka michache tu zilizopita Jeshi letu la Ulinzi limewahi kuwa na haja ya Rada kwa ajili ya Ulinzi wa anga ambayo ingefungwa Morogoro. Maombi yalienda kwa nchi nyingi ikiwemo USA ya Joseph Biden aka Joe Biden bila mafanikio.

Ni hawa hawa Korea Kusini walikubali kutufungia mitambo hiyo tena kwa "Siri Kubwa" Marekani isijue maana ingeleta mushkeli wa kidiplomasia kati yetu na wao. Wakijifanya wakulima wa mboga -mboga mchana lakini kumbe ni mainjinia walifuzu, Wakorea walifunga mitambo.

Hata hivyo USA ilipogundua ilileta shida lakini kwa ukomavu wetu wa kidiplomasia Tanzania ya Jakaya Kikwete iliwaambia USA, "sisi tuna shida ya Rada, kama hamtami hawa watufungie basi mtupe yenu". USA ilikubali lile sharti na Korea Kusini ikafungasha virago maana na wao hawakuona sababu ya magomvi yao kutuathiri. Tuna historia ndefu na Korea Kusini kuliko USA kama nitakavyoeleza kupitia gazeti moja ya gazeti la wiki!

Kwa mantiki hiyo sikushangaa hata kidogo kwa Marekani kupitia TBC yao ya umma kutoa uzushi wa kijinga wenye lengo la kumchonganisha Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi wake kupitia mawakala wao ndani ya nchi kusambaza ujinga huo kuelekea Uchaguzi wa S/M kisha Uchaguzi Mkuu 2025 kwamba "Samia anauza nchi yetu" ili tu Samia achukiwe na chama chake! Huu ni uzushi wa kipumbavu usiovumilika na ninaamini USA itaomba radhi.

Tanzania ni nchi huru na sera yetu siku zote ni kutokufungamana na upande wowote katika vita za kiulimwengu. Hatuchaguliwi adui wala rafiki. Tunachoangalia ni maslahi mapana kwa nchi yetu na watu wake. Leo Iran imewekewa kila aina ya vikwazo vya kiuchumi lakini sisi ni marafiki na Iran na tunafanya nao biashara chungu mzima ikiwemo gesi asilia.

RAIS Samia wewe piga kazi! Hizo ni kelele tu za chura! Wewe hata chama Cha Hamas kikikubali kutujengea Zahanati kila kila Kijiji wewe nenda kasaini mikataba. Tungesikia kelele zao leo tungekuwa na Hospitali ya Palestina pale Sinza? Uongo ukiachwa kusikika sana hufikia hatua ya kuaminika kuwa ni kweli. Ukemewe mapema na kila mzalendo wa nchi YETU!
04/6/2024
Time: 11:23
Dar es salaam

Pia soma: VoA: Tanzania imepokea mkopo kutoka kwa Korea Kusini na kutoa sehemu ya bahari na madini

Na Bollen Ngetti
0683 226539
B-pepe bollenngeti@gmail.com

SIKU tatu kabla Rais Samia Suluhu Hassan hajaelekea Korea Kusini kuhenyea kwa ajili ya nchi yake niliandika huko kwa Max (X) kwamba, "Rais Samia unaenda Korea Kusini lakini jiandaye na matusi, kejeli , dhihaka na hata uzushi kutoka Marekani".

KWELI, Rais Samia Suluhu Hassan amefika Marekani na kufanikisha dili la mkopo wa Shilingi 6.57 Trilioni wa sharti nafuu ikiwamo riba ya 0.01% kwa muda wa miongo 4 inayoanzia 2026. Fedha ambayo itaelekezwa katika miradi ya kimkakati inayolipa kama sekta ya usafirishaji na uchukuzi!

Mara baada tu ya Rais kufanikisha jambo letu HIMA Marekani kupitia sauti yake, Voice of America, VoA ikaandika uzushi, dhihaka na matusi kwamba, "Tanzania imesaini mkopo wa fedha na Korea Kusini kwa sharti la kugawa sehemu yake ya bahari na madini". Ujinga uliovuka mawingu!

Hivi, katika hali tu ya kawaida Rais Samia ni mwendawazimu, mjinga, asiye na akili wala uzalendo kiasi gani hadi atoe sadaka ya sehemu ya bahari na madini yetu kwa gharama ya mkopo ambao bado tutailipa? Kwa nini isingekuwa mbadilishano wa hayo matrilioni na kipande cha bahari na madini ili lojiki iwepo? Yani unaenda kwa Mangi unamwambia akukopeshe mchele wa kilo 50 kwa ajili ya shughuli ya binti yako utamlipa mwisho wa mwezi na hapo hapo unamwambia njoo nyumbani nikupe fremu bure pamoja na kwamba mchele wako nitakulipa mwisho wa mwezi! VoA na Joseph Biden mmetukosea sana kwa ujinga huu. We can be stupid but not fool to that extent!

Watanzania tuelewe mambo mawili hapa kama si moja kubwa! Na atakayeelewa awaeleweshe wengine 10 wasio na smart phones. Kwanza kuna vita kubwa ya kiuchumi duniani. Kila Taifa linatumia kila aina ya mbinu halali na haramu kujiweka sawa kiuchumi maana uchumi ndio kila kitu.

Na moja ya mbinu ya mataifa makubwa ni pamoja na kudhoofisha nchi zingine kiuchumi, kiteknolojia na ikibidi hata kisiasa na kijeshi. Marekani kupitia shirika lake la kijasusi ilitumia kila mbinu chafu kuwatenganisha ndugu wa tumbo moja KOREA ikazaliwa Korea Kusini na Korea Kaskazini huku USA ikilalia Korea Kaskazini na kumuona Korea Kusini kama "nunda" na adui. Korea Kusini imewekewa vikwazo chungu nzima na Marekani hasa katika eneo la ubunifu wa teknolojia ya zana za kivita bila mafanikio.

Wananchi wa Korea Kusini waliamua kushikamana na kujenga uzalendo kwa nchi yao wa kupigiwa mfano baada ya kuona, "hatuna ndugu wala mjomba, lazima tujikomboe wenyewe" na pakwanza walipoanzia na kupambana na kushinda saratani ya rushwa na ufisadi na kumtambua kila Mkorea Kusini alipo ndani na nje ya nchi yao na anafanya nini kwa maslahi ya Korea Kusini!

Nimkumbushe Mtanzania jambo ambalo limewahi kutokea lakini haikuandikwa popote na kokote rasmi! Miaka michache tu zilizopita Jeshi letu la Ulinzi limewahi kuwa na haja ya Rada kwa ajili ya Ulinzi wa anga ambayo ingefungwa Morogoro. Maombi yalienda kwa nchi nyingi ikiwemo USA ya Joseph Biden aka Joe Biden bila mafanikio.

Ni hawa hawa Korea Kusini walikubali kutufungia mitambo hiyo tena kwa "Siri Kubwa" Marekani isijue maana ingeleta mushkeli wa kidiplomasia kati yetu na wao. Wakijifanya wakulima wa mboga -mboga mchana lakini kumbe ni mainjinia walifuzu, Wakorea walifunga mitambo.

Hata hivyo USA ilipogundua ilileta shida lakini kwa ukomavu wetu wa kidiplomasia Tanzania ya Jakaya Kikwete iliwaambia USA, "sisi tuna shida ya Rada, kama hamtami hawa watufungie basi mtupe yenu". USA ilikubali lile sharti na Korea Kusini ikafungasha virago maana na wao hawakuona sababu ya magomvi yao kutuathiri. Tuna historia ndefu na Korea Kusini kuliko USA kama nitakavyoeleza kupitia gazeti moja ya gazeti la wiki!

Kwa mantiki hiyo sikushangaa hata kidogo kwa Marekani kupitia TBC yao ya umma kutoa uzushi wa kijinga wenye lengo la kumchonganisha Rais Samia Suluhu Hassan na wananchi wake kupitia mawakala wao ndani ya nchi kusambaza ujinga huo kuelekea Uchaguzi wa S/M kisha Uchaguzi Mkuu 2025 kwamba "Samia anauza nchi yetu" ili tu Samia achukiwe na chama chake! Huu ni uzushi wa kipumbavu usiovumilika na ninaamini USA itaomba radhi.

Tanzania ni nchi huru na sera yetu siku zote ni kutokufungamana na upande wowote katika vita za kiulimwengu. Hatuchaguliwi adui wala rafiki. Tunachoangalia ni maslahi mapana kwa nchi yetu na watu wake. Leo Iran imewekewa kila aina ya vikwazo vya kiuchumi lakini sisi ni marafiki na Iran na tunafanya nao biashara chungu mzima ikiwemo gesi asilia.

RAIS Samia wewe piga kazi! Hizo ni kelele tu za chura! Wewe hata chama Cha Hamas kikikubali kutujengea Zahanati kila kila Kijiji wewe nenda kasaini mikataba. Tungesikia kelele zao leo tungekuwa na Hospitali ya Palestina pale Sinza? Uongo ukiachwa kusikika sana hufikia hatua ya kuaminika kuwa ni kweli. Ukemewe mapema na kila mzalendo wa nchi YETU!
04/6/2024
Time: 11:23
Dar es salaam
#SafiriNaSamia2025
Andiko refu limejaa ulalamishi halituambii kama VOA waongo je ukweli ni upi kuhusu masharti? Mana tunajua hizo purpose diversion of fund imekua ikifanyika mara zote na hakuna kitu tutafanya,nyingine porojo tu
 
Mleta mada unawapinga VoA kwa vigezo gani??

Elewa Kwa watu kutoka 'shiti holu kantriiz' kuingia mikataba kama hiyo sio jambo la ajabu.
Ule uliosanuliwa na mwendazake ambao ilikuwa tuingie na wachina si ujinga huo huo!?
 
Back
Top Bottom