GE2025 Samia Suluhu Hassan kuapishwa kesho, Novemba 3, 2025 saa 4 asubuhi

GE2025 Samia Suluhu Hassan kuapishwa kesho, Novemba 3, 2025 saa 4 asubuhi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Makumbele

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2009
Posts
312
Reaction score
1,433
Kutoka BBC | Novemba 2, 2025

IMG_8797.jpeg


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuapishwa rasmi Jumatatu Novemba 3 Jijini Dodoma.

Kulingana na taarifa ya serikali iliyotangazwa kupitia runinga ya kitaifa ya TBC, sherehe ya uapisho itafanyika katika uwanja wa kijeshi ambapo raia wa kawaida hawatakubaliwa kuhudhuria.

TBC itarusha matangazo hayo mubashara kutoka Dodoma kwa taifa.

Rais Samia alitangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29 kwa kujinyakulia asilimia 97.66 ya jumla ya kura zote zilizopigwa.

INEC imetangaza kwamba ushindi mkubwa wa Rais Samia ambao haujawahi kushuhudiwa nchini Tanzania katika awamu tano za kwanza za uongozi wa nchi hiyo.

Wapiga kura milioni 37 walisajiliwa kushiriki kwenye uchaguzi wa mwaka huu huku INEC ikisema kwamba Samia alipata jumla ya kura milioni 31.

Aidha tume hiyo imesema pia kwamba asilimia 87 ya waliosajiliwa kupiga kura walijitokeza kushiriki kwenye uchaguzi huo ambao ulishuhudia maandamano huku mji wa Dar es Salaam ukikabiliwa na amri ya kutotoka nja kati ya saa 12 jioni na saa 12 asubuhi.
 
“Mimi ndiye Amir jeshi mkuu” - halafu unaenda kuapishwa jeshini kama kuruta anayemaliza mafunzo?

Tumemkataa. Hata aapishiwe wapi, kamwe hawezi kuwa rais wetu. Sote tuseme HAPANA. Hii haina uvyama. Umeua ndugu zetu, hatuwezi kukusamehe.
 
Kwa kuwa ni nchi moja tu ya Somalia ndo raisi wake katoa salamu za pongezi.

Na kwa kuwa maraisi Kagame, Ruto na Museveni na wengine kama Zambia, Namibia na Botswana nchi ambazo ni wanachama wa SADC nao bado wafanya tathmini watume salamu au wasitume.

Na kwa kuwa Umoja wa Ulaya, Umoja wa Mataifa wameonyesha kutoridhishwa na namna uchaguzi huu ulivyotendwa.

Na kwa kuwa nchi kama Uingereza, Marekani, Canada, Sweden, Ujerumani, Denmark na zingine zote bado hawatoa kauli yoyote.

Na kwa kuwa vyombo vya habari vya nje zimeambiwa na mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam Albert Chalamila kwamba havina hadhi ya kuripoti habari yoyote ile kutoka Tanzania isipokuwa vile tu vilivyopo Tanzania vikiwemo Crown media, Wasafi, na vingine.

Na kwa kuwa bado amri ya kutotembea baada ya saa 12 jioni haijaondolewa.

Basi uapisho wa Samia Suluhu Hassan huko Dodoma umejaa mashaka mno na utaendelea kuwa na mashaka mengi huko tuendako.
 
Nina uhakika 💯, anaapishwa alafu anajiuzulu ili nchi ashike Nchimbi (makamu wake)…inshort wanalazimisha kuokoa CCM, maana akiachia ngazi sasa, inabidi serikali ya mpito iwekwe ambako kuna asilimia kubwa CCM kufutwa kama sio kutoka madarakan. Ni akili za kawaida kujua haka kamchezo wanakotaka kufanya. JWTZ have let us down.
 
Nina uhakika 💯, anaapishwa alafu anajiuzulu ili nchi ashike Nchimbi (makamu wake)…inshort wanalazimisha kuokoa CCM, maana akiachia ngazi sasa, inabidi serikali ya mpito iwekwe ambako kuna asilimia kubwa CCM kufutwa kama sio kutoka madarakan. Ni akili za kawaida kujua haka kamchezo wanakotaka kufanya. JWTZ have let us leo na kesho akaapishwa Nchimbi.

Kwanini asijiuzulu na kisha kumpisha Nchimbi aapishwe hiyo kesho kisha nae ajiuzulu?

Na hata kama akijiuzulu ataishi wapi?
 
Nina uhakika 💯, anaapishwa alafu anajiuzulu ili nchi ashike Nchimbi (makamu wake)…inshort wanalazimisha kuokoa CCM, maana akiachia ngazi sasa, inabidi serikali ya mpito iwekwe ambako kuna asilimia kubwa CCM kufutwa kama sio kutoka madarakan. Ni akili za kawaida kujua haka kamchezo wanakotaka kufanya. JWTZ have let us down.
Bado tutamkataa Nchimbi. Kukubali ni sawa na kusema uchaguzi ulifanyika. Tunahitaji kusafisha huu uchafu wote na kuanza upya kama taifa la kisasa lenye watu wanaojitambua. Hizi takataka za Nyerere ziishe. Inatosha.
 
Nina uhakika 💯, anaapishwa alafu anajiuzulu ili nchi ashike Nchimbi (makamu wake)…inshort wanalazimisha kuokoa CCM, maana akiachia ngazi sasa, inabidi serikali ya mpito iwekwe ambako kuna asilimia kubwa CCM kufutwa kama sio kutoka madarakan. Ni akili za kawaida kujua haka kamchezo wanakotaka kufanya. JWTZ have let us down.
Mange kimambi alisema hili, walikuwa wana negotiate na wenzao, on the table kulikuwa na options 2 ila hii kwao ndio wanaiona ni sahihi but i'm sure haitasaidia chochote
 
HAMAKI ZINAZIDI KUPAA NA WAMTAKA RAIS MTEULE AACHIE NGAZI

02 November 2025

Tanzania Election; The Aftermath Hezrom Obadiah LIVE from Tanzania​



View: https://m.youtube.com/watch?v=EQ9EZsLlQ8s
Raia waapa rais mteule aachie ngazi kwa kuwa hawataacha kuandamana hadi aachiwe ofisi ya wananchi

Tabora, Mwanza, Lindi, Songwe, Mbeya, Kahama, Geita, Tanga maandamano siku hii ya tano hayajakwama ...
 
Akijiuzulu sasa, maana yake sio Nchimbi atachukua nchi bali ni Philip mpango…na wao hawataki nchi ishikwe na mtu ambaye sio mwana mtandao mwenzao wasije kunyongwa au kufilisiwa.
Lakini ndivyo inavyotakiwa kwani hadi sasa ni raisi mteule hivyo aweza kabisa kujizulu na kumpisha Dr Mpango.

Hapo ndipo kakosekana Mabeyo.
 
Waseme tu ukweli. Kesha apishwa somewhere else! Hiyo kesho wanarusha video tu. Hakutakuwa na kitu chochote hapo Dodoma.
Kwani nini hata wahangaike kumuapisha wakati matokeo wameyatunga? Si watangaze tu kuwa keshajiapisha mwenyewe….. like….who cares kwamba kesho ataapishwa?

Wamejitangaza kushinda na wajitangaze tu kuwa.keshajiapisha. Nobody cares.
 
Back
Top Bottom