Uchaguzi 2020 Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania

Wanao lalamika kuwa wanaibiwa kura. Mtu gani makini unaibiwa? Mabwege na mazuzu ndiyo huibiwa. Kwa habari ya trh 28, hilo sitajadili maana sinaga tabia ya kujadili ndoto aotazo mchana mwenye njaa kali.
 
Kwani hata kuna anakuwa umuhimu kiasi cha kudhani una wa kumtisha hata kama ana madhara? 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Sielewi umeandika nini apo,labda ufanye kujijibu mwenyewe.
 
Kwani hata kuna anakuwa umuhimu kiasi cha kudhani una wa kumtisha hata kama ana madhara? 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Niambie hapo 🖕 uilimaanisha nini? Kwamba wewe una kiswahili cha kipekee kiasi kwamba hakuna anaeweza kukielewa? Kama yupo mtag aje afafanue ulichoandika hapo.

Kwa kudhania "apo" ni kiswahili si ajabu kuwa huwezi kuelewa ninachoandika.
Huna lolote unaloweza kujadili kuhusu siasa, na hii mada tayari imekushinda kwahiyo jitaahidi kusubiri hoja mserereko utembee nazo.
 
Tafsiri, hata tusipopata kura zenu tutaiba tu kura na kuunda serikali kwa hila.

Watu kweli mnakuwa wagumu wa kuelewa. Mtu anayekubalika na wengi ukimnyima kura wewe haitasaidia, kwa sababu bado atashinda na kuunda serikali. Uchaguzi uliopita baadhi ya majimbo yalichukuliwa na upinzani, lakini hilo halikutosha kuinyima CCM overall victory na ridhaa ya kuunda serikali!

Kwa ujumla, Upinzani bado hawajajua jinsi ya kushinda uchaguzi. Nguvu ya CCM iko chini, ambako hata social media kwao ni msamiati au luxury. Hao ndio “the silent majority” wanaoibeba CCM. If the Opposition doesn’t capture this gigantic cluster, losing an election to CCM is inevitable. Upinzani watabaki kulialia tu kwamba wameibiwa kura.
 
Naona ametofautiana na bossi wake, boss wake amesema kama hujachagua ccm hakuletei maendeleo yeye anasema wataleta maendeleo kote, ccm kule bara kumbe muarobaini wao ilikuwa ni Tundu Lissu, ni wazi ccm wanahofu ya TL sana, walijidanganya kabla ya uchaguzi eti upinzani hautakuwa na nguvu mana mkuu kajenga flyover na kununua ndege. sasa TL amevuruga kote kote juu chini juu hizo bara bara na ndege sasa hakuna kiongozi wa ccm anaweza kusimama kwenye kampeni akazitaja tena kila kitu alichofanya boss wake Lissu ameweka wazi huo ufisadi, sijui vitambulisho vya rais nadhan wamejuta kuleta hivyo vitambulisho kumbe havina ata jina la mtumiaji kila kitu ni ufisadi mtupu tena uliokubuhu.

Naamini mkuu kiwanja cha ndege alichojenga nyumbani kwao sasa anakiona kama mavi, kimemkost kwenye kampeni hizi lakini hana uso ata kwa majirani zake ni aibu kubwa kiongozi aliyesimama na kuapa atapambana na ufisadi lakini nyuma yake yeye mwenyewe ana maskendo kibao.
 
Ana hofu huyo, kimbunga cha Lissu kinawavuruga na kuwafanya waishi kwa hofu ya kushindwa uchaguzi.

Nikivyokuwa namheshimu huyu mama, sikuwahi kudhania kuwa anaweza kufikia kiwango cha chini kiasi hiki! CCM kimemgaeibu kabisa huyu mama!
 
Utajuaje unakubalika na wengi wakati uchaguzi haujafanyika bado?
 
Kumekuwepo na kauli na vitendo vya kutisha wapiga kura, kwamba, mwaka huu utake usitake ccm inashinda kwa kishindo. Hapa ccm wanacheza na saikolojia ya wananchi kwamba, wakate tamaa wasiende kupiga kura ya UKOMBOZI ili wao ccm kwakuwa wanategemea wanachama hai waweze kujishindia kwa Uraihisi.

Niwahakikishie tu, uchaguzi huu niwakipekee Sana, utakuwa wazi, Kila mtu atajua wapi wamepata ngapi na Nani kaongoza mapema tu kwa kuwa hawataweza kuzibiti mitandayo yote, itawalazimu NEC kusoma matokeo Kama yalivyo na hakutakuwa na wasiwasi, hivyo tuzidi kuhamasishana tujitokeze tukapige kura.

#kura ni haki yako, nenda kapige kura
 
Ama hakika sijawahi kusikia maneno ya kijeuri ya watawala kuzidi awamu hii.

Hawa wagombea wawili wa CCM, Samia na Magufuli wameonyesha hali fulani ya kutoheshimu hisia, wala nguvu ya mwananchi katika kutumia haki yake ya kuchagua amtakaye

Magufuli yeye bila wasiwasi anawaambia wananchi kuwa wakichagua mbunge kutoka chama kingine tofauti na CCM basi hapeleki maji!

Samia yeye anapita njiani anawaambia wananchi kuwa mtupigie kura au msitupigie sisi tunashinda tu!

Huku kutoheshimu wananchi kunatokana na nini hasa? - Kwamba wao wana command ya majeshi au kitu gani?

Kwa kauli zao hawa wagombea wawili ni dhahiri hawaamini katika serikai ya wananchi, iliyowekwa na wananchi kwa ajili ya wananchi (The government of the people, by the people and for the people)

Kama kweki tungekuwa na tume huru ya uchaguzi hizi kauli za kubagaza, na kubeza power ya mwananchi kufanya maamuzi huru katika kuiweka serikali madarakani ingekuwa imeshawahoji kuwa wana maana gani haswa?

Sasa hebu fikirieni hili jambo, kama Magufuli anasema wazi kuwa atabagua wananchi kwa kufuata misingi ya kisiasa, Na kama Mgombea wake mwenza anasema kuwa kura zetu kwake si kitu na watashinda tu, zje hawa kweli wanatuheshimu sisi wananchi au wanatuona kama vikaragosi fulani hivi visivyo na maana?

Kwa kauli hizi mbili za hawa watu wawili ni dhahiri hawatoshi kuendelea kutuongoza, TUWAKATAE


 
Swala ni kwamba, muamko kwa CCM ni wa kipekee mwaka huu 2020 kulinganisha na 2015. Watanzania sio watu wa kujaribu mambo wasio yajua, kwa sasa CDM inawaambia maneno mengi ambayo hata wao CDM hawayaamini.

Mfano, kuruhusu mifugo kuchungwa kwenye hifadhi za mbuga za taifa, au kulinda uhuru wa vyumbani kwa kisingizio cha kuwapa watu uhuru wa faragha. Je ikiwa mtu anamtwanga mkewe kabla ya kumlazimisha tendo la ndoa je, serikali ya CDM itakataa kuingilia kati kwa kuogopa uhuru wa faragha?

Hatujaongele kuweka madini yetu rehani na kuigawa TZ kwa majimbo huku majimbo yasio na rasilima na watu wa kutosha kubaki kuwa masikio kutupwa.
 

Hapo wametishiwa ama wameambiwa ukweli. Hakuna kampeni za kipindi cha miaka ya nyuma tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi ambapo CCM ina umaarufu na kukubalika kwa Watanzania kama 2020.

Hayati Nyerere alihangaika sana kumbeba Hayati Mkapa. Mama huyu Makamu wa Rais anajionea kwa macho yake, kwa nini asiwaambie ukweli watu wa aina ya kwako na Lissu?
 
hizi shule za kata ni balaa sana !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…