Pulchra Animo
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 3,718
- 3,465
Ama hakika sijawahi kusikia maneno ya kijeuri ya watawala kuzidi awamu hii.
Hawa wagombea wawili wa CCM, Samia na Magufuli wameonyesha hali fulani ya kutoheshimu hisia, wala nguvu ya mwananchi katika kutumia haki yake ya kuchagua amtakaye
Magufuli yeye bila wasiwasi anawaambia wananchi kuwa wakichagua mbunge kutoka chama kingine tofauti na CCM basi hapeleki maji!
Samia yeye anapita njiani anawaambia wananchi kuwa mtupigie kura au msitupigie sisi tunashinda tu!
Huku kutoheshimu wananchi kunatokana na nini hasa? - Kwamba wao wana command ya majeshi au kitu gani?
Kwa kauli zao hawa wagombea wawili ni dhahiri hawaamini katika serikai ya wananchi, iliyowekwa na wananchi kwa ajili ya wananchi (The government of the people, by the people and for the people)
Kama kweki tungekuwa na tume huru ya uchaguzi hizi kauli za kubagaza, na kubeza power ya mwananchi kufanya maamuzi huru katika kuiweka serikali madarakani ingekuwa imeshawahoji kuwa wana maana gani haswa?
Sasa hebu fikirieni hili jambo, kama Magufuli anasema wazi kuwa atabagua wananchi kwa kufuata misingi ya kisiasa, Na kama Mgombea wake mwenza anasema kuwa kura zetu kwake si kitu na watashinda tu, zje hawa kweli wanatuheshimu sisi wananchi au wanatuona kama vikaragosi fulani hivi visivyo na maana?
Kwa kauli hizi mbili za hawa watu wawili ni dhahiri hawatoshi kuendelea kutuongoza, TUWAKATAE
View attachment 1602568
Kamanda, you have unleashed a lot of words, but your call to action isn’t grounded in the power of reason!
Hivi mtu anayesema anajua watashinda na mwingine ambaye anajiita Rais kabla ya Uchaguzi (na hajawahi kuwa Rais) ni nani jeuri zaidi?