Uchaguzi 2020 Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania

Uchaguzi 2020 Samia Suluhu: Hata mkipigia kura kule kwingine CCM ndio inaenda kuunda Serikali, tutashinda vikubwa sana Tanzania

Ama hakika sijawahi kusikia maneno ya kijeuri ya watawala kuzidi awamu hii.

Hawa wagombea wawili wa CCM, Samia na Magufuli wameonyesha hali fulani ya kutoheshimu hisia, wala nguvu ya mwananchi katika kutumia haki yake ya kuchagua amtakaye

Magufuli yeye bila wasiwasi anawaambia wananchi kuwa wakichagua mbunge kutoka chama kingine tofauti na CCM basi hapeleki maji!

Samia yeye anapita njiani anawaambia wananchi kuwa mtupigie kura au msitupigie sisi tunashinda tu!

Huku kutoheshimu wananchi kunatokana na nini hasa? - Kwamba wao wana command ya majeshi au kitu gani?

Kwa kauli zao hawa wagombea wawili ni dhahiri hawaamini katika serikai ya wananchi, iliyowekwa na wananchi kwa ajili ya wananchi (The government of the people, by the people and for the people)

Kama kweki tungekuwa na tume huru ya uchaguzi hizi kauli za kubagaza, na kubeza power ya mwananchi kufanya maamuzi huru katika kuiweka serikali madarakani ingekuwa imeshawahoji kuwa wana maana gani haswa?

Sasa hebu fikirieni hili jambo, kama Magufuli anasema wazi kuwa atabagua wananchi kwa kufuata misingi ya kisiasa, Na kama Mgombea wake mwenza anasema kuwa kura zetu kwake si kitu na watashinda tu, zje hawa kweli wanatuheshimu sisi wananchi au wanatuona kama vikaragosi fulani hivi visivyo na maana?

Kwa kauli hizi mbili za hawa watu wawili ni dhahiri hawatoshi kuendelea kutuongoza, TUWAKATAE


View attachment 1602568

Kamanda, you have unleashed a lot of words, but your call to action isn’t grounded in the power of reason!

Hivi mtu anayesema anajua watashinda na mwingine ambaye anajiita Rais kabla ya Uchaguzi (na hajawahi kuwa Rais) ni nani jeuri zaidi?
 
Preelection polls zimefanyika na zinaendelea kufanyika!
Poll my foot, Tanzania utafanya poll vipi wakati watu hata kujadili tu wanafanya self censorship?

Umemsikia Mzee Butiku anavyolalamika woga wa Watanzania?

Poll utafanya vioi fair katika nchi ambayo ukitia poll results ambazo hazijapitishwa na serikali ni kosa la jinai?
 
Poll my foot, Tanzania utafanya poll vipi wakati watu hata kujadili tu wanafanya self censorship?

Umemsikia Mzee Butiku anavyolalamika woga wa Watanzania?

Poll utafanya vioi fair katika nchi ambayo ukitia poll results ambazo hazijapitishwa na serikali ni kosa la jinai?

Vuta subira; baada ya uchaguzi utajua kama zilikuwa fair au hazikuwa fair!
 
Vitoto vya kishua bwana watanzania hatutakagi hilo lichama na hatujuagi kiingereza msalimu dadiii
She has spoken a very good point,because it's hard for opposition to defeat CCM . People loves CCM alot and they gonna vote for it no matter what.
 
Dada unajiaibisha hujui kiingereza kabisa hata cha form 1
Nothing, just we are in the campaign trail. Everyone has to fight for their side, and when they speak, the other side will always find offended. But in the end, its politics. After the election is over, you'll get surprised to learn that your view of her is essentially not changed much.
 
Jamani sa kama hamjui simuandike kizaramo..view of her ?? Hahahahah
After the election is over, you 'll get surprised to learn that your view of her is essentially not changed much. .....
 
Ccm imekataliwa kila kona ya nchi hii, na yeye Samia anafahamu. Ccm haiwezi shinda sanasana watalazimisha kujitangaza. Watu wana siri mioyoni mwao. Karata waliyobakiwa Nayo ni kuwafukuza mawakala vituoni na hii ndio itawapa ushindi,maeneo ambayo upinzani wakikomaa hadi mwisho ccm watapoteza maeneo hsyo
 
Vitoto vya kishua bwana watanzania hatutakagi hilo lichama na hatujuagi kiingereza msalimu dadiii

Sio kila Mtanzania ana mawazo kama yako. Wapo wengi sana ambao wana mawazo tofauti kabisa na ya kwako!
 
Ccm imekataliwa kila kona ya nchi hii, na yeye Samia anafahamu. Ccm haiwezi shinda sanasana watalazimisha kujitangaza. Watu wanao siri mioyoni mwao.kkwa

Upinzani kukosa visingizio sio kawaida yao. Kama kawaida, safari hii pia vitakuwepo vya kumwaga!
 
Back
Top Bottom