GE2025 Samia: Watu wengine huko wanalalamika kwanini Watanzania Mnajaza Viwanja vya CCM

GE2025 Samia: Watu wengine huko wanalalamika kwanini Watanzania Mnajaza Viwanja vya CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Mgombea Urais Jamuhuri ya Muungano wa Tanzannia Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan akiendelea kunadi sera kwa wananchi wa Iramba Mkoani Tabora, amewashukuru kwa muitikio wao Mkubwa katika Kampeni hizo

" Wananchi wa Mkoa wa Singida, kila Wilaya nilipoingia wananchi ni wengi mnoo, ni wengi mno. Mpaka watu wengine huko wanalalamika kwa nini Watanzania mnajaza viwanja vya CCM" amesema Mgombea Urais CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan

 
1000112357.jpg
 
Mgombea Urais Jamuhuri ya Muungano wa Tanzannia Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan akiendelea kunadi sera kwa wananchi wa Iramba Mkoani Tabora, amewashukuru kwa muitikio wao Mkubwa katika Kampeni hizo

" Wananchi wa Mkoa wa Singida, kila Wilaya nilipoingia wananchi ni wengi mnoo, ni wengi mno. Mpaka watu wengine huko wananlalamika kwa nini Watanzania mnajaza viwanja vya CCM" amesema Mgombea Urais CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Wanacholalamika ni kuwa watu wenu wanaojaza viwanja wanaletwa toka mikoa jirani kwa malori kama ng'ombe, pia hao wengi ni wafanyakazi wa serikali kama walimu, askari, polisi, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na wafanyakazi wa umma. Ni kwamba mnafeki.....mnafeki kuwa mnapendwa kumbe mnalazimisha.
 
Ina maana kiukweli ukweli kabisa hajui kinachoendelea???

Basi kama hajui hii nchi karibia inagawanyika na kua nchi mbili ndani ya mipaka ya nchi moja
 
Huyo content creator anashindana na kivuli chake .

Hawezi kuongea na kujenga hoja anachoweza ni mipasho.

Wamshauri ajikite huko maana hata matokeo yake kidato cha nne yanasadifu.
 
Nyomi inajazwa na wanafunzi kwa kusombwa na magari toka sehemu mbalimba. Kwa ujumla hii ni nyomi feki hata kama kuna watu wazima pia wamo. Jana kuna kosta iliishia kuambulia wanafunzi tu na wanachama wachache ikawapeleka mjini kuliko na mkutano
 
Ukweli ni kwamba hizi kampeni ni za ccm tu, hata wale vikaragosi wanaogombea kwa kuzuga kuwa ni wapinzani kampeni hizi wanazinogesha tu japo hazinogi imeshindikana. Hebu na hao vikaragosi wajiziwe nyomi kwa kusaidiwa na ccm wapewe wasanii kuvutia nyomi za watoto. Kama wana magari makali na ulinzi wa kufa mtu kwa nini wasisaidiwe kujaziwa nyomi kubwa feki na wao wakati tunajua ni wazugaji tu?
 
Back
Top Bottom