Mkataba wetu na mgombea upo kwenye ILANI, kupitia huo mkataba tunajua atatufanyia nini na kipi hatafanya, na kwa vigezo hivyo ndiyo maana tunamchagua. Kama atafanya kinyume na huo mkataba maana yake ni kuvunja mkataba.
“Nakumbuka 2015 yapo ambayo wala hayakuwa kwenye ilani ya Uchaguzi. Ilani haikuagiza kununua Ndege 11 tumenunua, haikuagiza kujenga Bwawa la Nyerere kwa Trilioni 6.5, tumefanya, haikueleza tujenge SGR kwa Trilioni 7.026, tumejenga”. Dkt. Magufuli.
Kwahiyo Magufuli anamaanisha kwamba hata hii ilani ya zaidi ya page 300 anayoinadi kwa sasa haina maana, hatoitekeleza ni porojo tu wala siyo muhimu kwake.
Nataka mwana CCM mwenye uwezo wa kujenga hoja atufafanulie hili. Je, tuendelee kumwamini kwa ahadi anazotupa kupitia ilani hii ya 2020 au tujue ni porojo tu za kuombea kura na kudanganya wananchi.