Samsung kuachana na Google Kama Search Engine

Samsung kuachana na Google Kama Search Engine

Mzee wa kupambania

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2022
Posts
21,111
Reaction score
53,092
Imeripotiwa kuwa Samsung wana mpango wa kuanza kutumia Bing ya Microsoft kama default search engine.

Taarifa zinasema kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya AI ambapo ChatGPT iliyo chini ya Microsoft kuonekana kuwavutia wengi imefanya Samsung wafikirie kutumia Bing kama default search engine.

Kutokana na uamuzi huu Google itapoteza mapato yenye thamani ya $3 billion kwa mwaka kutoka Samsung

Jumatatu ya leo mauzo ya hisa za Microsoft yalipanda kwa 1.4% huku ya Google yakishuka kwa 3.2%

Google bado ni search engine inayopendwa zaidi duniani ikiwa na matumizi kwa 90% na Bing ni chini ya 3%
 
Itakua patashika nguo kuchanika
emoji26.png
emoji22.png
Kupitia Apple google wanaingiza $20 bln kwa mwaka imagine nao wahame kama Samsung
 
Nafikiri ile hasara kubwa waliyoipata Samsung ya karibu $3 bln katika mauzo ya semiconductor ndani ya robo ya kwanza ya mwaka huu 2023 (Jan-March) imewachanganya sana wanaanza kufanya maamuzi ambayo huenda yakawa-cost
Hasara hyo ilitokana na nini mkuu
 
Back
Top Bottom