Samsung yazidi kuwa Iphone

Wapo wanaohama kutoka flagship za Oppo, Vivo na ZTE kwenda Samsung. Watashangaa kutokuta charger
Usije uka-assume simu ni Samsung tu. Zipo simu nyingi tu za bei ghali
 
Wapo wanaohama kutoka flagship za Oppo, Vivo na ZTE kwenda Samsung. Watashangaa kutokuta charger
Usije uka-assume simu ni Samsung tu. Zipo simu nyingi tu za bei ghali
Ninauza simu mwaka wa 7 huuu Kaka naongea kwa exprience yangu sokoni
Hakuna anayetoa milion 3 kununua simu akalalamika chaja.....mteja anayetoka brand ulizotaja kuhamia Samsung si mgeni
Alikua anatumia akaenda kutangatanga sasa karejea nyumbani
Why?? user exprience yake huko haijaridhisha
Huyu ameshaelewa quality ya nini anataka
Pia anaelimu na vingi hawezi kushangaa chaji
Yaani utoe milioni 2...3 kununua simu ukose laki 1 ya chaja OG???
 
Charger original ya Sony Xperia 1 IV ya 30W inauzwa kwa 50£. Hii bei ni kubwa kwa charger ya 30W
Hiyo simu ulinunua sh ngapi? Ukicompare hapo, huwezi jibahilia kuchukua chaja nzuri kwa simu yako.
 
Hata mimi aisee nilijikuta navibanjua vile vispika hata nione basi waya umeachia lakini wapi[emoji16][emoji16]. Unajitahidi sana kutunza earphones ila tu ghafla sikio moja linaacha kupiga. Hizi za bluetooth sijawahi kuzipenda kwa kweli huwa natumia nyumbani tu.

Hapa nataka nikipita kkoo nikanunue tena za wire. Changamoto nayokutana nayo hapa ni kwamba port hiyohiyo ndio ya kuchaji simu sasa mda mwingine unacheza games chaji inakaribia kuisha inabidi uchomoe earphones port itumike kuchaji na simu zetu hizi refurb mateso matupu. Hizi tech mda mwingine zinaongeza stress tu [emoji16]
 
Kwani mkuu hawa jamaa haya mabadiliko ya kuzifanya earphones kuwa za type-C walishauriana na nani? mimi nahisi pale kwenye mic ndio kuna tatizo maana kwingine kote kuko sawa halafu earphones zenyewe nilinunua ghali sijui nilikosea wapi.
 
Nani anatumia waya siku hizi mambo ni Bluetooth tuu
 
Flagship za sasa kwenye box kuna
1. Vivo X90 Pro
-Simu yenyewe
- 120W charger
-Kava la simu
-6A rated USB C-C cable


2. Samsung Galaxy S23 Ultra
-USB C cable
-Simu yenyewe
-Stylus pen ndani ya simu

3. Xiaomi 13 Pro
-Simu yenyewe
-120W charger
-6A rated cable
-Kava la simu
-Protector juu ya screen ya simu

4. iPhone 14 Pro Max
-USB C-to-Lightning cable
-Simu yenyewe

5. Sony Xperia 1 IV
-Simu tu

6. Xiaomi 13 Ultra
-Kava la simu
-Simu yenyewe
-USB C cable
-90W charger
 
Vidogo kwako mkuu, utajiskiaje uziwe gari bila tank la mafuta ili ukachongeshe lako? 😀
 
samsung Tanzania, TECNO Tanzania , infinix hebu someni hapa
 
As long as tunaendelea kuzitumia hizi gadgets - kelele zetu ni za vyura tu

Labda tuanze kutengeneza zetu

Hawalazimishi tununue
 
As long as tunaendelea kuzitumia hizi gadgets - kelele zetu ni za vyura tu

Labda tuanze kutengeneza zetu

Hawalazimishi tununue
Hawalazimishi ununue Ila utalazimika ununue. Eti kisa Samsung haweku charger kwenye simu ndio usiinunue hiyo simu?
Hapana, kwa sasa kampuni kama Samsung tayari inatengeneza simu Bora Sana kwa hiyo wateja watanunua tu Ila ndio watalazimika kutafuta accessories wenyewe
 
Kwani mkuu hawa jamaa haya mabadiliko ya kuzifanya earphones kuwa za type-C walishauriana na nani? mimi nahisi pale kwenye mic ndio kuna tatizo maana kwingine kote kuko sawa halafu earphones zenyewe nilinunua ghali sijui nilikosea wapi.
Naona watu wakajiongeza baada ya kuona simu zinakuja na type c bila ya earphone jack port wakaona watengeneze earphones ambazo ni type C moja kwa moja!
Mimi zangu pia zilikuwa na mic, ila nilkuja kugundua shida ipo pale sehemu ya kuchomekea dizain uki-bend wire zinapiga zote ukiiacha normal sikio moja halipigi. Lakini nikashangaa mbona hazina damage yoyote na zilikuwa za rubber material kama hizi za Oraimo. Nikaja kuzitupa tu!
 
Haya mambo alianzisha Apple. Na kwenye hii dunia yetu kila anachoanzisha Apple watu wanaita Innovation [emoji28][emoji28]
Ila mi najua ni mbinu tu za kibiashara. Haya makampuni Yana akili sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…