Samsung yazidi kuwa Iphone

Samsung yazidi kuwa Iphone

Mimi sijasema mbaya Boss...embu fikiri anayenunua earpod ya laki 3 akakaa nayo miaka na anayenunua za elfu 80 kila miezi 6 nani anasave? Hapo sijaangalia quality ya bidhaa na more advanced features.

By exprience mtu anayenunua Simu hatoki simu ya laki 2 akahamia milioni 2, katika 100 mteja huyu ni 1 na huwa wanatambo sana so swala la kununua huwa sio shida zake

Watu hupanda ngazi na kufika milions
Na cha ajabu sasa hata baadhi ya simu za Aseries mbona hazina chaji wala earphones pia
Wapo wanaohama kutoka flagship za Oppo, Vivo na ZTE kwenda Samsung. Watashangaa kutokuta charger
Usije uka-assume simu ni Samsung tu. Zipo simu nyingi tu za bei ghali
 
Wapo wanaohama kutoka flagship za Oppo, Vivo na ZTE kwenda Samsung. Watashangaa kutokuta charger
Usije uka-assume simu ni Samsung tu. Zipo simu nyingi tu za bei ghali
Ninauza simu mwaka wa 7 huuu Kaka naongea kwa exprience yangu sokoni
Hakuna anayetoa milion 3 kununua simu akalalamika chaja.....mteja anayetoka brand ulizotaja kuhamia Samsung si mgeni
Alikua anatumia akaenda kutangatanga sasa karejea nyumbani
Why?? user exprience yake huko haijaridhisha
Huyu ameshaelewa quality ya nini anataka
Pia anaelimu na vingi hawezi kushangaa chaji
Yaani utoe milioni 2...3 kununua simu ukose laki 1 ya chaja OG???
 
Charger original ya Sony Xperia 1 IV ya 30W inauzwa kwa 50£. Hii bei ni kubwa kwa charger ya 30W
Hiyo simu ulinunua sh ngapi? Ukicompare hapo, huwezi jibahilia kuchukua chaja nzuri kwa simu yako.
 
Mkuu wewe ni kama mimi sipendi za bluetooth kabisa, ninazo kama case mbili ila sizitumii, nikanunua za nokia original nmezitunza sana tahamaki nikazisahau pale bandarini wakati wa kusubiri usafiri.

Nikaona isiwe tabu nikanunua nyingine original za vietnam za waya lakini type-C dah juzi naona sikio moja halipigi nimegoma kukubali nazifumua nitizame waya umekatikia wapi niziunge sitaki kabisa adha ya kucharge earphones.
Hata mimi aisee nilijikuta navibanjua vile vispika hata nione basi waya umeachia lakini wapi[emoji16][emoji16]. Unajitahidi sana kutunza earphones ila tu ghafla sikio moja linaacha kupiga. Hizi za bluetooth sijawahi kuzipenda kwa kweli huwa natumia nyumbani tu.

Hapa nataka nikipita kkoo nikanunue tena za wire. Changamoto nayokutana nayo hapa ni kwamba port hiyohiyo ndio ya kuchaji simu sasa mda mwingine unacheza games chaji inakaribia kuisha inabidi uchomoe earphones port itumike kuchaji na simu zetu hizi refurb mateso matupu. Hizi tech mda mwingine zinaongeza stress tu [emoji16]
 
Hata mimi aisee nilijikuta navibanjua vile vispika hata nione basi waya umeachia lakini wapi[emoji16][emoji16]. Unajitahidi sana kutunza earphones ila tu ghafla sikio moja linaacha kupiga. Hizi za bluetooth sijawahi kuzipenda kwa kweli huwa natumia nyumbani tu.

Hapa nataka nikipita kkoo nikanunue tena za wire. Changamoto nayokutana nayo hapa ni kwamba port hiyohiyo ndio ya kuchaji simu sasa mda mwingine unacheza games chaji inakaribia kuisha inabidi uchomoe earphones port itumike kuchaji na simu zetu hizi refurb mateso matupu. Hizi tech mda mwingine zinaongeza stress tu [emoji16]
Kwani mkuu hawa jamaa haya mabadiliko ya kuzifanya earphones kuwa za type-C walishauriana na nani? mimi nahisi pale kwenye mic ndio kuna tatizo maana kwingine kote kuko sawa halafu earphones zenyewe nilinunua ghali sijui nilikosea wapi.
 
Flagship za sasa kwenye box kuna
1. Vivo X90 Pro
-Simu yenyewe
- 120W charger
-Kava la simu
-6A rated USB C-C cable
07_49_07_gsmarena_001.jpg


2. Samsung Galaxy S23 Ultra
-USB C cable
-Simu yenyewe
-Stylus pen ndani ya simu
07_51_04_gsmarena_001.jpg


3. Xiaomi 13 Pro
-Simu yenyewe
-120W charger
-6A rated cable
-Kava la simu
-Protector juu ya screen ya simu
07_53_39_gsmarena_001.jpg


4. iPhone 14 Pro Max
-USB C-to-Lightning cable
-Simu yenyewe
07_56_42_gsmarena_003.jpg


5. Sony Xperia 1 IV
-Simu tu
07_59_16_gsmarena_042.jpg


6. Xiaomi 13 Ultra
-Kava la simu
-Simu yenyewe
-USB C cable
-90W charger
08_02_46_images.jpg
 
Wenzio wanafanya mabadiliko wakiamgalia na soko jinsi linavyoenda

Kipindi hicho Samsung kuweka earphone jack kwenye simu zao ilikuwa ni idea nzuri kwasababu wireless pods, earbuds zilikuwa bado hazijakaa vizuri sokoni.

Charger nayo ni ya kuiletea complain kweli?

Watu wanaangalia mazingira, mitaani miwaya miwaya imekuwa mingi na hii yote kwasababu ya kuzagaa kwa charger.

Hivyo unakuta mtu ananunua simu ambayo imekuja na charger wakati huo charger yake aliyokuwa anaitumia kwenye simu ya zamani bado ipo.

Ni vitu vidogo ila we umevifanya vionekane vikubwa.
Vidogo kwako mkuu, utajiskiaje uziwe gari bila tank la mafuta ili ukachongeshe lako? 😀
 
Mimi ni mpenzi mkubwa Sana wa simu za android na simu yangu pendwa ni Samsung lakini huku tunakoelekea naona kabisa nitaisaliti chama.Sababu ni kuwa Samsung wanaiga vitu vingi Sana ambavyo havina msingi kutoka Kwa kampuni ya simu ya Iphone.

Hivi ni vitu baadhi ambavyo Samsung kaiga kutoka Kwa Iphone na vimeleta mabadiliko hasi Sana kwa watumiaji wa hizi simu za Samsung;


1 Wameiga kuondoa 3.5 mm jack kutoka kwenye simu za Iphone ;

Mwaka 2017 iphone waliondoa 3.5mm jack ya kuingiza Ear phones kutoka kwenye simu zao za Iphone 7. Matokeo yake Iphone walipondwa Sana na watumiaji wake na kukemewa vikali na kupondwa na makampuni ya simu ikiwemo Samsung.Chanzo Cha kuondoa 3.5 mm jack ilikuwa ni sababu Iphone walishindwa kutengeneza kioo full screen huku 3.5mm Jack ikiwepo.Iphone wanadai kwamba waliondoa 3.5 mm jack Ili waweze kutengeneza full screen BIla kizuizi.Kitu ambacho simu za android ilishaweza kutengeneza huku 3.5 mm jack ikiwepo.Tuseme tu android phones ZIPO mbele kiteknlolojia zaidi ya iPhone .

Swali langu ninajiuliza kwanini Samsung waliamua kuondoa 3.5 mm jack kwenye simu zao Kwa kumuiga iPhone wakati wanajua Iphone waliondoa hicho kitu sababu ya kukosa teknolojia ya kutengeneza full screen BIla kutoa 3.5mm jack?

2 Wameiga kutoweka charger na cover za simu kwenye Box la Simu mpya kama wanavyofanya Iphone ;

Nasikitika Sana kuona Samsung wamepata ujasiri wa kupakia simu tu kwenye Box BIla charger Wala Cover kama simu zingine za Android zinavyofanya.Watu wanatoa mamilioni lakini hawapati product zilizokamilika kwenye Box.Ni upuuzi mtupu.


Wakati simu zingine za Android zinajitahidi kuweka Hadi pre installed screen protector na accessories za simu zinazohitajika Sana Samsung wapo busy wanazidi kuziondoa.


Mimi ni mdau wa Samsung lakini hapa niseme tu Samsung wamefeli pakubwa.

Ni ajabu kukuta Flagship phone kama galaxy S23 ultra imekuja tu na USB Haina charger ni upuuzi mtupu tu.

NI BORA NIHAMIE KAMPUNI ZINGINE ZA SIMU MAANA SAMSUNG WAMEBADILIKA KUWA IPHONE SIO WAO TENA.

Shame on you ShameSung
samsung Tanzania, TECNO Tanzania , infinix hebu someni hapa
 
As long as tunaendelea kuzitumia hizi gadgets - kelele zetu ni za vyura tu

Labda tuanze kutengeneza zetu

Hawalazimishi tununue
 
As long as tunaendelea kuzitumia hizi gadgets - kelele zetu ni za vyura tu

Labda tuanze kutengeneza zetu

Hawalazimishi tununue
Hawalazimishi ununue Ila utalazimika ununue. Eti kisa Samsung haweku charger kwenye simu ndio usiinunue hiyo simu?
Hapana, kwa sasa kampuni kama Samsung tayari inatengeneza simu Bora Sana kwa hiyo wateja watanunua tu Ila ndio watalazimika kutafuta accessories wenyewe
 
Kwani mkuu hawa jamaa haya mabadiliko ya kuzifanya earphones kuwa za type-C walishauriana na nani? mimi nahisi pale kwenye mic ndio kuna tatizo maana kwingine kote kuko sawa halafu earphones zenyewe nilinunua ghali sijui nilikosea wapi.
Naona watu wakajiongeza baada ya kuona simu zinakuja na type c bila ya earphone jack port wakaona watengeneze earphones ambazo ni type C moja kwa moja!
Mimi zangu pia zilikuwa na mic, ila nilkuja kugundua shida ipo pale sehemu ya kuchomekea dizain uki-bend wire zinapiga zote ukiiacha normal sikio moja halipigi. Lakini nikashangaa mbona hazina damage yoyote na zilikuwa za rubber material kama hizi za Oraimo. Nikaja kuzitupa tu!
 
Haya mambo alianzisha Apple. Na kwenye hii dunia yetu kila anachoanzisha Apple watu wanaita Innovation [emoji28][emoji28]
Ila mi najua ni mbinu tu za kibiashara. Haya makampuni Yana akili sana
 
Back
Top Bottom