Na hili ndio tatizo la wabongo wengi, kuweka doubt kwenye kila kitu ambacho hawakielewi.
Sasa unapima distance ya 2017 to 2023 na kuona kama ni mbali sana hivyo umbali huo lazima kuna vitu kuhusu mfumo wa chaji utakuwa umeboreshwa kwenye matoleo mapya, hivyo uone kuna uhitaji mkubwa wa kuwepo kwa chaja zinazoendana na mfumo huo mpya.
Haipo hivyo Mkuu
Umeambiwa existing users wataweza kutumia chaja zao za zamani kwenye devices mpya bila kikwazo kwasababu ya mfumo wa chaji walioweka ni very compatible na chaja zote.
Kampuni linapotoa tamko kama hilo linakuwa limefanya tathmini na kujihakikishia kuwa hakutakuwa na changamoto kwenye chaja za zamani kutumika kwenye devices mpya.
Huyo jamaa wako kivyovyote hakutumia chaja ya zamani ya Samsung, alikuwa anatumia chaja feki zile ambazo ndani kuna waya mbili
Mosi, Shambulia HOJA usimshambulie mleta hoja
Usiwafanye wabongo wote wajinga na hawana reasoning
Tunajua FACT na tunajua propaganda za kibiashara
Pili siongei kitu sikielewi bali naongea through experience
Nimekutolea mfano wa jamaa yangu na s23 na mimi mwenye na mke wangu
Nikinunua charger dukani au online stumii wembe kuchana ndani kukagua kuna nyaya ngapi ndani, natumia recommendations, reviews na na kusoma details zake
Shida yote hii ni kwasababu sijapewa charger original HAKUNA UTETEZI MWINGINE
Katika ulimwengu wa technology na haswa ya simu 2017 na 2023 ni mbingu na aridhi mkuu, ni parefu mmno na kuna manadiliko makubwa mmno
Hapa unazungumzia S8 Vs S23, Iphone 8 Vs iphone 14 pro max
Nimekuuliza kwani Samsung Wana charger moja standard kwa simu zao zote kuanzia 2017?
NOPE
S8 ina support charger ya wattt 15 wakati S23 ni watt 25 hadi 45
Ukitumia watt 15 kwa S23 unahitaji hadi masaa manne kujaza simu wakati ukitumia watt 25 ni chini ya lisaa limoja
Na hapo sijazungumzia cable
Numbers dont lie mkuu achana na porojo za mazingira
Nakupa mfano rahisi sana
Kama leo hii ikitoka S15 na ikauza simu milioni 10 inamaana kutahitajika charger milioni 10
Assume watu hawa waanze kutumia charger za zamani
Je zile simu walizotumia mwanzo huwa zinapotea hazitumiki tena?
Hata ukiuza au ukigawa au ukibadilisha bado itahitaji charger ili itumike
Kwahiyo watarudi tena kununua charger milioni 10 na kampuni zinapiga hela huku wewe umekomaa wanalimda mazingira