Sanduku la Agano liko wapi?

Sanduku la Agano liko wapi?

BIKIRA MARIA NI SANDUKU LA AGANO JIPYA KWA SABABU ANA SIFA SAWA NA LA KALE

Sanduku la Agano kwenye Agano la Kale lilikuwa ni kisanduku kidogo ambacho kilibebwa na Waisraeli wakiwa njiani kutoka utumwani Misri kwenda nchi ya ahadi. Kuna mambo kama sita hivi yanayohusu Sanduku la Agano ambayo yanahusianishwa na Bikira Maria.

(1) Ndani ya Sanduku la Agano Waisraeli waliweka vitu vifuatavyo:

(i) mana, mkate wa ajabu ulioshuka kutoka mbinguni (Kut. 16). Mana ni kile chakula cha ajabu walichopewa Waisraeli kutoka mbinguni baada ya kulalamika kuwa hawana chakula wakiwa jangwani kuelekea nchi ya ahadi.

(ii) fimbo ya Haruni, kuhani mkuu (Hes. 17). Fimbo ya Haruni ni ishara ya ukuhani/upadre wa Haruni.

(iii) vibao vya Amri Kumi za Mungu (Kut. 20). Kwenye tafsiri ya Kiebrania “amri za Mungu” walizopewa Waisraeli mlimani Sinai zimetafsiriwa kama “maneno ya Mungu” (Kiebrania dabar). Kwa hiyo amri za Mungu kwa Kiebrania zimeitwa “maneno” ya Mungu.

Mana, fimbo ya Haruni na maneno kumi ya Mungu vilivyokuwa katika Sanduku la Agano ni viashiria vya Kristo Mwenyewe. Bikira Maria ni Sanduku jipya la Agano kwa sababu alimbeba Yesu Mwenyewe katika tumbo lake- Yesu ambaye ni:

(i) mkate halisi- chakula cha kweli kilichoshuka kutoka mbinguni kama ilivyokuwa kwa mana (Yoh. 6:32)

(ii) Neno aliyefanyika mwili. Yesu ni Neno wa Mungu aliyefanyika mwili (Yoh. 1:14). Kwenye Sanduku la Agano kulikuwa na vibao viwili vya “maneno ya Mungu” (amri za Mungu), ndani ya tumbo la Bikira Maria kulikuwa na “Neno” aliyefanyika mwili. Uwepo wa Neno aliyefanyika mwili ndani ya tumbo la Bikira Maria unamfanya Bikira Maria awe Sanduku laAgano kama vile maneno ya Mungu yalivyokuwa ndani ya Sanduku la Agano lile la kwanza.

(iii) Kuhani wetu mkuu (Waebr. 3:1).

(2) Mfalme Daudi “aliruka na kucheza kwa furaha” mbele ya Sanduku la Agano lilipokuwa linapelekwa Yerusalemu kwa maandamano (2 Sam. 6:16). Kadhalika Yohane Mbatizaji “aliruka kwa shangwe” katika tumbo la Elisabeti wakati Bikira Maria alipomsalimia Elisabeti (Lk. 1:41). Hivyo, Yohane Mbatizaji anaruka kwa furaha mbele ya Bikira Maria ambaye ni Sanduku Jipya la Agano kama mfalme Daudi alivyoruka na kucheza kwa furaha mbele ya Sanduku la Agano.

(3) Mfalme Daudi, baada ya kushuhudia nguvu na kazi za Mungu zilizotendeka kwa njia ya Sanduku la Agano, anashikwa na mshangao na kusema “Litaniijiaje sanduku la Bwana? (2 Sam. 6:9). Naye Elisabeti, akiwa amejazwa Roho Mtakatifu, anatamka kama Daudi, “Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? (Lk. 1:43). Kuna uhusiano mkubwa kati ya yale anayotamka Daudi kuhusu Sanduku la Agano katika Agano la Kale na yale anayotamka Elisabeti kumhusu Bikira Maria (ambaye ni Sanduku jipya la Agano) katika Agano Jipya. Ndiyo maana Bikira Maria anaitwa Sanduku la Agano.

(4) Sanduku la Agano lilikaa katika nyumba ya Obed-edom kwa muda wa miezi mitatu (2 Sam. 6:11). Bikira Maria naye alikaa nyumbani mwa Elisabeti kwa muda wa miezi mitatu (Lk. 1:56). Bikira Maria ni Sanduku la Agano maana yale yaliyotendeka juu ya Sanduku la Agano katika Agano la Kale yanatendeka pia kwa Bikira Maria- Sanduku Jipya la Agano linalopatikana katika Agano Jipya.

(5) Wingu (ambalo kwenye Agano la Kale ni ishara ya uwepo wa Mungu) “liliifunikiza” (overshadowed) hema ya kukutania ambapo ndani yake kulikuwa na Sanduku la Agano (rejea Kut. 40:34-35). Neno la Kigiriki linalotafsiri neno “kuifunikiza” (overshadow) ni “episkiasei”. Neno hilo hilo “episkiasei” ndilo analotumia malaika Gabrieli kwa Bikira Maria: “Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu “zitakufunika” [episkiasei] kama kivuli…” (Lk. 1:35). Kama ambavyo hema ya kukutanikia ambayo ndani yake kulikuwa na Sanduku la Agano lilivyofunikwa na wingu kutoka juu (ambayo ni ishara ya uwepo wa Mungu), kadhalika Bikira Maria ambaye ni Sanduku jipya la Agano anafunikwa kwa nguvu za Aliye juu (Aliye juu ni Mungu).

(6) Kwa kadiri ya Agano la Kale, hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kulishika kwa mikono yake sanduku la Agano au hata kutazama tu kilichomo ndani isipokuwa kuhani mkuu peke yake kwa kuwa Sanduku la Agano lilikuwa takatifu sana. Mtu yeyote ambaye angeligusa au hata kulitazama kwa ndani alipata adhabu ya kifo. Bibilia imetupatia mifano ya waliouawa ama kwa kosa la kuligusa Sanduku la Agano au kulichungulia kwa ndani: baadhi ya watu wa Beth-shemeshi (rejea 1 Sam. 6:19) na Uza (rejea 2 Sam. 6:7). Kadhalika, Mungu hakuruhusu Bikira Maria ambaye ni Sanduku jipya la Agano, aguswe na mtu yeyote. Ndiyo maana Bikira Maria amebaki bikira (bila kuguswa na mwanaume yeyote, hata Yosefu hakumgusa kimwili) ili kuonesha kuwa naye ni Sanduku jipya la Agano. Sanduku hili la Agano (yaani Bikira Maria) ni takatifu sana kwani ni Mama wa Mungu
 
Pia ukisoma ufunuo kwa makini kuna ujumbe ambao tunaweza kupata kuhusu sanduku la kale na Bikira Maria. Ukisoma Ufunuo 11:19 na Ufunuo 12:1 utaona mara baada tu ya kuzungumzia kuonekana sanduku la agano hekaluni kwenye ufunuo 11:19 then sura inayofuata inaanza na habari ya ishara kuu kuonekana mbinguni, mwanamke aliyevikwa nyota 12 ....

Kwanza hapo habari za huo mstari mwanamke huyo unaweza kutafsiri kama Kanisa lakini pia kama Bikira Maria! Kinacholeta picha zaidi ni kuwa Biblia hapo awali haikuwa na chapters and verses. Hivyo andiko juu ya Sanduku la agano na habari za huyo mwanamke zimefuatana si bahati mbaya!

Binafsi siamini hilo sanduku limesafirishwa hadi hekalu ya mbinguni bali lilikuwa kivuli tu na sanduku linalozungumziwa kuwepo hekaluni ni Bikira Maria.

Kazi ya sanduku la agano ni sawa na safina ya Nuhu ambavyo baada ya picha ya awali kupitia agano la kale ilikuwa ni kivuli cha agano jipya! Kama mana ya agano la kale ndio Yesu Kristo aliye mzima ktk maumbo ya mkate na divai.
 
Wale wanaodanganya kuwa manabii wa zamani kuanzia abraham walikuwa ni waamini wa ile imani ya kibla wanaweza kusema wanayo ndio wamefukia pale kwenye kale kasanduku keusi wanako kazungukaga na baadaye kumpiga thetani asiyeonekana mawe
Ungesema hoja yako vizuri tu bila kuchokoza mani zingine...hakuna na wala hatotokea mtu wa imani ya kibla kusema hilo sanduku liko Ka'abah! kuhusu kumpiga shetani asiyeonekana mawe...ajabu kuna shetani anayeonekana!?
 
Kaburi la Musa liko wapi? Tungeanzia hapo ndio tuelekee kuuliza sanduku la agano liko wapi? Vingekuwepo hivi na aina ya akili za watu wa kizazi hiki vingesha geuzwa kuwa ibada za sanamu. Watu wanaomuamini mfalme zamuradi ama sheikh majini loooo?!
 
Halitajwi kati ya vyombo vilivyopelekwa Babiloni hekalu lilipohabiriwa mwaka wa 607 K.K. wala halitajwi kati ya vyombo vilivyorudishwa Yerusalemu baadaye.—2 Wafalme 25:13-17; Ezra 1:7-11
Nebuchadnezzar anajua Saduku alikolipeleka. Yaonekana huyu Mfalme alitaka kutawala ulimwengu mpaka Mwenyezi Mungu akaingilia kati baada ya Kufuru na dhihaka zake. Kuna vyombo aliviiba kule Jerusalemu baada ya kumuua mfalme Sadekia na maaskari wake akavamia Hekalu akapora vyombo vyote yawezekana na Sanduku la Agano likabebwa kwenda Babiloni, hii ilikuwa dhihaka kubwa kwa wana wa Islael kwa kweli.

Alipokufa mwanae Balishezer akarithi kiti cha ufalme babaye.... kama kwendeleza wa dhihaka siku moja akaalika watu kibao kuja kufurahia mvinyo na matanuzi kwa kutumia vyombo vile vile alivyovitoka madhabahauhi Jerusalemu....

Aisee yakamkuta makubwa... Mwenyezi Mungu akaingilia kati ya kuhoji ufalme wake..!!

Daniel 5:

Karamu ya Belshaza (Mtoto wa Nebuchadnezzar)

1Siku moja mfalme Belshaza aliwaandalia karamu kubwa maelfu ya wakuu wake na kunywa divai pamoja nao. 2Kutokana na kunywa divai, mfalme Belshaza akatoa amri vile vyombo vya dhahabu na fedha ambavyo mfalme Nebukadneza, baba yake, alivichukua kutoka hekalu la Yerusalemu, viletwe ili avitumie kunywea divai pamoja na maofisa wake, wake zake na masuria wake. 3Basi, vile vyombo vya dhahabu na fedha vilivyochukuliwa hekaluni Yerusalemu vikaletwa. Mfalme, maofisa wake, wake zake na masuria wake wakavitumia kunywea. 4Walikunywa huku wanaisifu miungu iliyotengenezwa kwa dhahabu, fedha, shaba, chuma, miti na mawe
 
Naomba wajuvi wa mambo wanisaidie - utawala wa Nebukadneza mfalme wa Waashuruna baadaye Mwanawe Belishaza na hatimaye mfalme Dario - Je kwa sasa hilo taifa ni lipi? Hapo ndipo pa kuanzia kulisaka sanduku letu maana ndiye aliyekwanga kuvunja helalu alilojenga Suleiman kule Islael na kupora vitu vyote hekaluni.
 
Mafundi wa zamani waliwezaje kutengeneza chombo kizuri kilichong'aa namna hivyo?
 
Liko Afrika, mahala ambako ndiko chimbuko lake, ndiomaana wazungu na jamii zote za watu weupe hawakomi kuja afrika kwa mgongo wa utalii, kumbe behind wanawinda mali za kale ambazo zina nguvu ya Uungu.

Kuna mengi waafrika hamuyajui sabbu ya ninyi kushikiria mambo ya kipumbavu ya utandawazi na kujiona naninyi mmekuwa wazungu na kusahau mila zenu.

Uzungu mwingi mwishoe mnadharau mpaka asili yenu.

Elimu, siasa na dini ndivyo vimeharibu mfumo mzima wa maisha ya muafrika, ndiomaana tunasahau jukumu letu duniani.

Kama tukijua sili ya maisha ya Uafrika basi tutaitawala dunia, babu zetu walifeli kuanza kuwakaribisha wagen(watu weupe) na kuwapa sili wasizotakiwa kujua, mwisho wa siku ndio hayo usaliti ukatokea kwa waafrika kuuza sili kwa watu weupe, ndipo walipoanza kujua weakness za muafrika ni imani ndiomaana walikazana kutumezesha ujinga wa dini na elimu za uongo ili watutawale na watusahaulishe historia yetu..

Hilo sanduku hakuna wa kuliona mpaka Kristo wa kweli aamue kufichua mahala lilipo lkn kulingana na mafundisho yake, lipo afrika na lilifichwa na manabii wa kiafrika ambao hao mashetani wanaojiita waisrael wa Middle east walidanganya ktk biblia zao za uongo kuwa ni weupe.
 
Huu ni mfano wa sanduku la agano ambalo wana wa Israel waliambiwa watengeneze na Mussa wakiwa nyikani wakitoka Egypt (Misri) wakielekea promised land (Nchi ya ahadi). Sanduku hilo lilikuwa ni kama box la mbao lililotengenezwa na aina moja ya mbao inayoitwa (acacia wood) iliyofunikwa na dhahabu. Lilikuwa la urefu wa 1.15 metres, upana wa 0.7 metres na kimo cha 0.7 metres.

Ilikuwa inabebwa na mishikio miwili mirefu ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa mbao hiyo ya acasia ambazo pia zilikuwa zimefunikwa na dhahabu. Juu ya sanduku kuliwekwa makerubi wawili waliokuwa wamegeukiana mabawa yao yakiwa yamegusana. Uwepo wa Mungu haukuwepo ndani ya sanduku bali ulikuwa juu yake katikati ya hao makerubi.

Uwepo wa Mungu juu ya sanduku hilo ulikuwa kama nuru. Kuhani mkuu alipaswa kufunika macho asiione nuru hiyo ("hakuna mwanadamu anionaye na akaishi" Kutoka 33 : 20) kila alipokuwa akiingia lilipokuwa sanduku ambapo ni patakatifu pa patakatifu.


Hapa ndipo ambapo Mungu alipokuwa akiionana na Musa. Sanduku hili lilikuwa likibebwa na wana wa Walawi pekeyake hakuna mwingine aliyeruhusiwa kulishika, yeyote aliyedhubutu kulishika pasiporuhusiwa alikufa papohapo. Hao makerubi wawili wanawakilisha utukufu wa Mungu. Ndani ya sanduku hili kulikuwa na:
  • Mawe mawili yaliyokuwa yameandikwa amri kumi za Mungu
  • Fimbo ya Aron iliyoota mauwa
  • Chombo cha dhahabu kilichokuwa na manna waliyokula wana wa Israel nyikani
Sanduku hilo lilikuwa linakaa patakatifu pa patakatifu, chumba cha ndani kabisa katika hema la kukutania. Aliyekuwa anaruhusiwa kuingia mahala hapo lilipokuwa sanduku hilo ni kuhani mkuu na alikuwa anaruhusiwa kuingia mara moja kwa mwaka. Kabla ya Kuhani mkuu kuingia patakatifu pa patakatifu alikuwa ni lazima aingie na damu ya mwana kondoo kwa niaba ya dhambi zake yeye mwenyewe na dhambi za wana wa Israel.

View attachment 1760924

Sanduku la agano lilikuwa ndani ya hekalu lililojengwa na Solomon mpaka hekalu hilo lilipokujwa kuvunjwa mikononi mwa utawala wa Babylon ukioongozwa na Nebuchadnezzar. Kilichotokea kwa sanduku hilo hakijulikani ingawa haiwezekani kuwa lilichukuliwa na majeshi ya Babylon kama vilivyochukuliwa vyombo vingine vya hekalu kwasababu katika list ya vitu walivyovichukua sanduku la agano halikutajwa.

Halitajwi kati ya vyombo vilivyopelekwa Babiloni hekalu lilipohabiriwa mwaka wa 607 K.K. wala halitajwi kati ya vyombo vilivyorudishwa Yerusalemu baadaye.—2 Wafalme 25:13-17; Ezra 1:7-11

Kulingana na baadhi ya vyanzo vya habari inasemekana kuwa mfalme Josiah, mmojawapo wa wafalme wa mwisho kutawala enzi za hekalu la kwanza, kutokana na unabii uliokuwa umetolewa alijua kuwa Jerusalem itavamiwa na Babylon, akalificha sanduku la agano.

Alipolificha sanduku imekuwa kitendawili. Chanzo kingine cha habari kinasema kuwa mfalme Solomon alionyeshwa kuwa Hekalu litakujwa kuvunjwa na majeshi ya Babylon, kwahiyo akaandaa pango karibu na bahari ya shamu (dead sea) ambapo Josiah akaja kulificha sanduku.

Na pia inasemekana nabii Yeremia (Jeremiah) alilificha sanduku chini ya Hekalu lililojengwa na Solomon.

HEKALU LA MBINGUNI


Alafu musa hakumuona mungu zaidi ya isharaze na sautiye
Samahani kwa kuongea kidigo
 
Kaburi la Musa liko wapi? Tungeanzia hapo ndio tuelekee kuuliza sanduku la agano liko wapi? Vingekuwepo hivi na aina ya akili za watu wa kizazi hiki vingesha geuzwa kuwa ibada za sanamu. Watu wanaomuamini mfalme zamuradi ama sheikh majini loooo?!
Alifia mlima Nebo na kuzikwa na Mungu
 
Kaburi la Musa liko wapi? Tungeanzia hapo ndio tuelekee kuuliza sanduku la agano liko wapi? Vingekuwepo hivi na aina ya akili za watu wa kizazi hiki vingesha geuzwa kuwa ibada za sanamu. Watu wanaomuamini mfalme zamuradi ama sheikh majini loooo?!

Yuda 1 aya ya 4 na ya 9.
 
Back
Top Bottom