Sanduku la kura lirudi mahala pake, tuchague viongozi tuwatakao

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, shalom!

Kwa kuwa kura halali zilitiwa ndani ya Sanduku la kura zikichangamana na kura fake tena chini ya usimamizi wa waandalizi wa uchaguzi wenyewe kama asemavyo Judge Warioba, zoezi Zima linageuka kuwa haramu.

Tunaweza kujisahihisha Kwa kufuta huu uchafuzi na kurudisha Sanduku la kura mahala pake Ili kuwachagua na kuwakataa viongozi tutakavyo Kwa HAKI na uwazi kabisa. Kwamba 2025 tukachagua viongozi wa mitaa Oct 27, October 28, tukachagua diwani, Mbunge na Ile ya juu Kwa Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi.

"Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa."

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen
 
Mboga mboga watakubali?
Lazima wawepo wasemao Rudisha,

Na imekuwa.

Huwezi kunajisi Sanduku la kura ukawa na maendeleo.

Enough is enough.

Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa.
 
Si ndiyo wanatuua sasa...kinakibao
Nguvu hiyo na silaha zitumikazo na posho wanayolipwa ni Kodi za wananchi.

Ndipo ujue, hayo nayo umma wa wananchi ukiamua yafike mwisho, yatakoma.
 
Unataka kuua ccm?
 
Mkuu Rabbon nje ya mada, hadi sasa sijajua majina na majimbo yao wabunge waliopata ajali, vipi ww umebahatika kuwajua?
Ngoja watibiwe kwanza,

Tutajua baadae majimbo Yao tukienda kuwapa mkono wa pole.

"Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa".
 
Ngumu sana.
Hawawez kukubali
 
Ngumu sana.
Hawawez kukubali
Wao ni wangapi wakataao,

Na umma wa Watanzania ni wangapi watakao HAKI katika chaguzi?

" Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa".
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…