bandeko andeko
JF-Expert Member
- Oct 20, 2021
- 1,080
- 2,143
lakini bora yeye kuliko wezi wa mali za umma.Za mchina zilee mkuu ndio hizi anadaiwa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
lakini bora yeye kuliko wezi wa mali za umma.Za mchina zilee mkuu ndio hizi anadaiwa
Huyo ndio pdidy wakongwe tunamjua hajui kuandika vizuriSijaambulia kitu!
Alikumbwa na siasa za wakati uleHuyu walimrusha rusha tu
Kaongezewa na masifuri
WakTi wakina manga waliuza mawe ya zaidi ya bln 20 na walikuwa kimya
Any way hyo lazier amlipe mchina wa watu hela yake
Ova
Mabalaa yameanza kumwandamaLazier lipa bana atujazoea kuringishana huku tunadhulumu watu
ARUSHA: Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite katika Mji wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Saninu Laizer maarufu kwa jina la Bilionea wa Tanzanite amemwangukia Mwekezaji raia wa China, Jun Fang akiomba wakae mezani kutafuta suluhisho ya mgongano wa kimaslahi kati yao.
Bilionea Laizer ameyasema hayo Jijini Arusha baada Fang kutaka kutaka kuomba msaada wa Balozi wa China nchini ili apate haki yake ya fedha na mali vyenye thamani ya Sh bilioni 8.5 ambazo (Laizer) anadaiwa kuonesha dalili za kutaka kumdhurumu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha Laizer alikiri kuingia ubia na mwekezaji Fang toka mwaka 2011 hadi mwaka 2021 kwa mwekezaji huyo kumiliki hisa asilimia 70 na yeye kama mzawa kumiliki hisa asilimia 30 kwa makubaliano kuwa Fang kuleta vifaa vyote vya kisasa vya uchimbaji,mtaji na kulipa gharama zote za uendeshaji ikiwemo mishahara ya wafanyakazi na alifanya hivyo.
Alisema baada ya mkataba kumalizika mwaka 2021 alimtaka mwekezaji Fang kuingia makubaliano (MOU) ya awali ambayo hakuyataja lakini raia huyo wa China aligoma kusaini makubaliano hayo.
‘’Mimi niko tayari kufanya kazi na Mchina wakati wowote na aje mezani tutatue changamoto zilizopo na tufanye kazi ya uchimbaji madini ya Tanzanite katika kitalu D kama zamani’’alisema Laizer.
Picha na John Mhala
Una maoni usisite kutuandikia
-
#MwangwiwaUkarimu
#echoesofkindness
#HabarileoUPDATES
View attachment 2881674
Na tanzanite za mchongo......kumbeAlikumbwa na siasa za wakati ule
Mi nilihisi tu yale mawe yalikuwa ya watu wakubwa zile zilikuwa mbinu tu za kuyatoa Nje ya Geti pesa zitumike kwa mambo ya wakati ule.ile ilikuwa ni mambo ya kisiasa tu, jamaa mgodi ulikuwa unaendeshwa na huyo mchina na washirika wengine, yale mawe waligawana na huyu mchina na washirika wengine