Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini

Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini

Embu tupe data kidogo Mkuu...sijui km namfaham sana so far as navyojua ni mwanamama aggressive aliyetumia kalamu yake vizuri kuiibia serikali!...sina hakika na kumbu kumbu zangu!

Duh Mwizi wa mali ya umma anapewa 'kudos' kaaazi kweli kweli
 
Hivi huyu mwanamama alimaliza kifungo chake? Mnakumbuka kosa lake na jinsi ambavyo kesi yake ilikuwa ni kama simulizi la kutosadikika.. Hivi akisikia yanayofanyika hivi sasa huko aliko si anaona aliwahi kidogo tu..

impunity ... I say Impunity and lack of political will ...a sign of writing in the wall Bro. Mwanakijiji
 
kama huna kumbukumbu ya zamaniiiiii basi una matatizo.. au mwenzetu umefuta kumbukumbu yako yote unaishi katika sasa tu?
aMEAMUA KUWA MTANZANIA HALISI KABISA... HUWA HATUTUNZI KUMBUKUMBU ZAIDI YA ZILE KIBABA-BAA SHULE NA KULEWA SANA, KUIBIWA AU KUIBA:twitch:
 
was late 1980's or early 1990's........FRONT PAGE kwenye gaeti la MFANYAKAZI

Gazeti la Mfanyakazi la James Nhende na makala zake za unazi wa YANGA....duh... Mkulu yule alikuwa anapenda vibaya?

Anyway....twende mbele turudi nyuma...tulikuwa na changamoto zetu kama taifa lkn tulifurahia sana maisha kwa jinsi ileile kama yalivyokuwa...those days are gone....its like... upo kwenye familia,ambapo baba anawaambia nendeni shule bila hela ya matumizi hali mbaya, ninyi watoto mnaondoka bila kinyongo na wala mama yenu halalamiki, kwani kweli mkimtazama baba(Mwl Nyerere) mnaona kweli siku hiyo hana minyeng'ule.

Lakini pale baba anaposema hana minyeng'ule halafu mnamkuta yupo wapiwapi's bar anasakata muziki wa Maquiz ya akina Dekula Kahanga Vumbi huku akiwa amezungukwa na vishtobe.....ahhhhhh.... HAMTOKUBALI........LAZIMA MKAMCHUKUE MAMA AJE KULETA VARANGATI...

Tunatakiwa tumfuate mama sasa hivi...aje...kubomoa.......potelea mbali...tutajenga kesho
 
Mwanakijiji (nimeamua kuita jina kamili)...

Huyu mama alinisikitisha sana kwani alikua na watoto wake wawili walikua wadogo sana wakisoma primamry moja wilaya ya kinondoni na walikua very cool, wapole na wana nidhamu ya hali ya juu... nina imani walipata shida sana kwani enzi zile haya mambo yalikua very rare... siku hizi ukiwa mtoto wa fisadi ni pride, JAMII IMEOZA

Nakumbuka hata jinsi kesi yake ilivyokua movie kwenye gazeti la mfanyakazi (kama sikosei), maana tulikua tunaamshwa tukanunue gazeti ili baba asome hii kesi ndio tuwahi shule... enzi zile hata gazeti tulikua tunapata kwa foleni

Pia kesi yake inakumbusha jinsi kesi zilivyokua zinaweza kuendeshwa kwa haraka, siku hizi kesi zote za wizi watu hawafungwi, kesi inaenda four eyars inakauka tu

cest la vie
 
Mkuu Mwanakijiji una kumbukumbu sana,mimi binafsi nilimchukulia Sara Martin Simbaulanga kama mtu hatari sana hasa ukizingatia magazeti ya wakati ule yalivyokuwa yakiripoti habari ile.

Kuna mtu anakumbuka jina lingine alilokuwa akilitumia ambalo kama sikosei lilikuwa la kiislamu hivi khadija or jina kama hilo.
 
NBC yetu iliumizwa na wengi na wengine ni matajiri wazawa sasa. Enzi hizo mwizi ulionekana ni mwizi kweli. Ulichukiwa na kila mtu. Sasa mnawaita wajasiriamali, wawekezaji, mnawachagua kuwa madiwani, wabunge na kuwateua kuwa mawaziri!
 
Daah mwanakijiji umenikumbusha mbali sana, yaani huyu mama alionekana kama shetani flani hivi vyombo vyote vya habari vilitangaza kesi yake kama vile uchumi wa TZ ulikuwa unateketezwa na huyu mama.

Nakumbuka kipindi hicho nipo shule ya msingi mzee wangu alikuwa analaumu sana kuhusu huyu mama na alikuwa akikutana na wenzake ndio lawama usiseme, na gazeti letu la mfanyakazi ndio lilikuwa mstari wa mbele kuandika mwenendo wa kesi ya huyu mama.

Sijui kama yu hai leo ili ashuhudie vile vitendo walivyoviasisi vikisimamiwa kwa uthabiti na JK,EL na RA na wachakachuaji yaani MAFISADI hivi sasa ni wafalme na si wahujumu kama yeye. Daaaah TANZANIA imebadilika sana.
 
Ninachokumbuka ni kuwa huyu Mama alikuwapua dola za marekani nyingi sana akataka kutoroka nazo nje ya nchi ila kabla hajafanikiwa dili likafumuka wakawa wanafukuzwa mpaka walipo kamatwa na hela mkononi. Nakumbuka kuna wakati yaliwahi toka mashati ya ujiuji (Kitambaa kama cha magauni ya CHARANGA kwa wanaoyakumbuka) yenye picha za dola za marekani tukawa tunayaita SIMBAULANGA.

Kweli kabisa mwanakijiji huyu mama aliwahi, maana enzi zile wizi ulikuwa haulindwi wala kusukiwa mikakati IKULU kama ilivyo sasa ambapo angechukua kiualaini na kuzikuta nje zinamsubiri badala ya kukimbia na bulungutu.

Nakumbuka kuwa yeye na hawara yake walinunua Min Bus za kutosha kwa ajili ya biashara ya Tours vikataifishwa. Miaka hiyo kulikuwa na waendesha mashtaka na mahakimu........siku hizi sina uhakika
 
Nakumbuka kuwa yeye na hawara yake walinunua Min Bus za kutosha kwa ajili ya biashara ya Tours vikataifishwa. Miaka hiyo kulikuwa na waendesha mashtaka na mahakimu. siku hizi sina uhakika

Dah Sarah Simbaulanga, watanzania tumekutana na visa vya kila aina lakini unaweza kuona ni namna gani tumepoteza viongozi waadilifu na tumeshindwa kujifunza kutoka kwao, tumebaki kusherekea vifo vyao.

Kama alivyosema bw.Mkinga siku ya kongamano chuo kikuu, viongozi waadilifu enzi zile za Mwl. Nyerere walikuwa wakisema wanaichukia rushwa unaziona dhamira zao kwa vitendo lakini siku hizi serikali imegeuka kuwa kimbilio la wanyang'anyi na waporaji.

Kwa mfano huu ufisadi tunaouimba kila siku, EPA, Richmond, CIS, DOWANS, IPTL n.k ingekuwa enzi zile za mwalimu, hawa mabig fish wote wangekuwa lupango, hakuna cha EL,RA wala wajomba zao.
 
Hii thread itatuonyesha under ages ni akina nani humu JF

Muhishimiwa under age tupo wengi humu, but still we can be GREAT THINKERS. Umri hauna nafasi now, ila uelewa, au umemsahau Malaria Sugu? Kama hujui anacheza na 40+ but probably ndo anayeongoza kwa kuandika udaku humu ndan.
Plz tuambien who iz this woman?
 
Namjua vizuri sana mama Sarah Martin Simbaulanga ni mlokole na ni mlalahoi anaonekana maeneo ya Mwenge mar chache chache. Anajutia sana kitendo alichofanya wakati ule,Mwenyewe anasema haukuwa utashi wake bali aliponzwa na mpenzie Toroha Mohamed Toroha.Amemrudia Mungu na anaendelea kuishi kwa amani tu.

I take your word:
Basi ni hatua nzuri sana...kama amejutia kosa na kuungama na kaucha basi huyu ni raia mwema wa Tz sasa. Mbaya ni haya majambazi ya sasa ambayo si tu kwamba hayaoni makosa na ufisadi wao bali yanafanya kampeni chafu kujisafisha.
 
Phillemon Mikael,

Mkuu Heshima yako,

Una kumbukumbu nzuri sana juu ya kesi ile, Sara na mumewe Toroha walitoka nadhani kwa msamaha wa rais, walikuwa wanaishi kule Kawe Mzimuni, mumewe nadhani alifariki kama sikosei mwaka juzi.
 
Hivi huyu mwanamama alimaliza kifungo chake? Mnakumbuka kosa lake na jinsi ambavyo kesi yake ilikuwa ni kama simulizi la kutosadikika.. Hivi akisikia yanayofanyika hivi sasa huko aliko si anaona aliwahi kidogo tu..
Mkuu itakuwa inamuuma sana na hasa haka kamethali. Mkuki wa Nguruwe kwa Binadamu Mchungu!:coffee:
 
Back
Top Bottom