Serikali ya Tanzania imesaini mkataba wa ujenzi wa barabara ya Lusahunga – Rusumo yenye urefu wa kilomita 92 kwa kiwango cha lami mradi utakaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 153.
Akiongea na wananchi wa mkoa kagera katika hafla ya utiaji saini iliyofanyika katika mji wa Benaco wilayani Ngara, waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuiunganisha Tanzania na Nchi Jirani ili kuweza kuinua uchumi wa wanakagera na watanzania kwaujumla.
Waziri Mbarawa Ameongeza kuwa baada ya kusainiwa mkataba huu kati ya serikali na mkandarasi ajulikanae kama Chines Civil Engineering Company LTD, Mradi huu utatakiwa kuanza kutekelezwa ndani ya miezi mitatu.
Amesema lengo la kujenga barabara hii upya ni kuwaondolea wananchi adha kubwa ya usafiri na usafirishaji ikiwa ni kufungua fursa upya za biashara.
Aidha amesema kuwa barabara huyo ni muhimu kwa nchi za Africa Mashariki katika kusafirisha mazao ya kilimo na kuongeza kipato kwa watanzania wa maeneo haya.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wa TANRODS Mhandisi Logatusi Mativila amesema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi 24 huku mbunge wa jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruholo akiomba vijana wa wilaya za Ngara na Biharamulo wapate ajira pindi mradi huo utakapoanza.
Pia, soma:
1).
Kwa hilo la barabara ya Lusahunga hadi Rusumo Serikali inacheza na hatari!
2).
Barabara Rusahunga Benaco haipitiki kwa nini Tanroads Biharamulo wasitumbuliwe?
3).
Ushauri wa Bure kwa Polisi barabara ya Ngara - Isaka Kipande cha Benaco Nyakanazi