Kulikuwa na bwana mmoja aliyeishi na mke wake, lakini siku moja wakazozana. Kama ilivyo kawaida wakati mwingine wanawake wakiwa na hisia kali, hasa wanapokasirika husema mambo mazito, mke alimwambia kuwa mimba aliyobeba si yake na akamtaja mwanaume mwengine ndie aliemjaza mimba huku akitoa maneno ya kumuumiza na kumdhalilisha mumewe.
Bwana huyo hakujibishana sana japo alijawa hasira, akaondoka zake na ndoa ikavunjika hapo.
Cha kushangaza, mtoto alipozaliwa, alifanana kabisa na yule mume wake waliyeachana. yule mwengine aliyedaiwa kuwa baba wa mtoto alipogundua hivyo, naye alikana kabisa kuwa ni mtoto wake.
Mama yule baadaye alianza kudai kuwa aliteleza kwa sababu ya kurogwa na kwamba hakuwa na akili timamu, Lakini mume wake wa zamani alishafunga ukurasa.
Wakati huo, mume wake wa zamani alikataa kabisa wazo la kulea mtoto kwa pamoja (co-parenting). Alisisitiza kuwa mtoto ama abaki huko huko au aje akae naye moja kwa moja.
Sasa swali linabaki: Je, katika hali kama hiyo, ni haki kumlaumu baba kwa kumtelekeza mtoto?