Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

Hii michezo hasa mpira wa miguu ilijaa ubabe sana. muda wowote ungeweza kutokea ugomvi mkubwa na mechi ikaishia hapohapo. baadhi ya marefa waliishia kukimbizwa kama wezi au hata kupata kichapo cha mbwa mwizi😆

kwa sababu hii baadhi yao walijihami kwa kuning'iniza silaha kama vile kisu kwenye upaja wakati anachezesha pale uwanjani. hii ilimjengea heshima refa huyu kwa wale wachezaji maana wanajua jamaa ana "moto"

na hii ilikuwa hata kwenye hii michezo ya ligi kuu mambo yalikuwa ivoivo. mambo yangeweza kubadilika muda wowote na mechi ikaishia hapo. refa akizingua anakula kichapo mechi inaishia hapo au anatafutwa refa mwingine mechi inaendelea kupigwa na wachezaji nao ni ivoivo wakizinguana zinachapwa mechi inaishia hapo.

sasa mambo yamebadilika sana.
 
sio hilo tu,ata vichaa wamekuwa wapole sana,ila machungaji wamekuwa wapigaji!!!
 
Zamani hakukua na bifu za wanaume peke ake hata wa kike..unakuta kuna mdada darasani anaeogopewa basi unakuta wadada wengine wanajipendekeza kwake nyie ambao hamna habari nae anatafuta visa tuu mpk mpigane ili upigwe...
 
Hii imekuja kuishia enzi za akina Ben mwalala,mwaikimba nk. siku ya daby kuisha bila ngumi uwanjani ilikuwa nadra sana
 
Zamani hakukua na bifu za wanaume peke ake hata wa kike..unakuta kuna mdada darasani anaeogopewa basi unakuta wadada wengine wanajipendekeza kwake nyie ambao hamna habari nae anatafuta visa tuu mpk mpigane ili upigwe...
Kweli kabisa zamani mwanamke alikuwa akisikia mme wake anatoka na fln hakuna kusuntana wala mipasho ni ngumi tu
 
Sema imepungua coz wameona usela vima umepitwa na wakati ,ila ukifatilia taarifa za polisi mkesha wa mwaka mpya masela wameuana sana ,kuna jamaa alikuwa BETO akakata kamba mkesha wa mwaka mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…