Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

Sasa hivi kupita mkesha/sikukuu bila ngumi imekuwa kawaida sana kitu ambacho miaka hiyo ilikuwa ni Nadra mno

Sijui ni kwamba watu wameokoka sana hata sielewi kabisa.Miaka ya nyuma mkienda kwenye mkesha ama sikukuu ilikuwa ni lazima ushuhudie ngumi za wanaume zikipigwa katikati ya senta .

Haikuwa sio ajabu kuona wala kusikia kuwa akina J n p jana walizipiga kwenye mkesha.Ni miaka sasa imepita bila kusikia wala kuona ngumi zikipigwa asee hadi najiuliza ama tiyari dunia imegeuka kuwa paradiso?

Leo hii hata ukienda club hadi unarudi hakuna ugomvi wowote utakao ushuhudia asee.Zamani hata mkesha wa disco wa darasa la saba tu tulikuwa tunashuhudia ngumi zikipigwa sana tu.Tena ilikuwa marufu kidato cha nne kukesha kwenye mahafari yao lakini kwa sasa imekuwa kawaida tu madogo wanakesha na walimu wana amani tele.

Kipindi hicho hakuna mwalimu yeyote angeweza kubali kurusu eti tukeshe kwenye mkesha wa kidato cha nne.Pamoja na kwamba sisi tulikuwa tunaanza disco saa4 asbh hadi saa12 jioni lakini bado ngumi zilipigwa tu.

Enzi hizo kulikuwa na mbabe wa mtaa mzima au hata kijiji kizima anafahamika kabisa kuwa flani ndo mbabe wa huu mtaa/kijiji. sasa hivi ni hamna. Nimemiss zana ubabe wa enzi hizo.

Baba mdogo aliwapiga migambo hadi wakapoteana na hapo walikuwa wanne leo hii mgambo mmoja tu anakuijia na anaenda kakupiga jeck njia yote na unatii au yeye anakuwa na baiskeli anakuswaga kama ng'ombe na unakubali tu.Kunakipindi mgambo na police mmoja mwenye siraha walikuja kukamata waunza gongo kipigo walichopata hawakurudia kuja tena kukamata walio bahatika kutokupigwa ni hawa walikuwa na police kwenye kukamata lakini wale waliojitenga wakiwa na marungu tu walipigika vibaya mno vile hata simu hazikuwepo walipigwa mno.

DJ alikuwa akibadilisha wimbo bila mpangilio lazima kipigo kimuhusu na ma DJ wa kipindi hicho walikuwa wababe. Kuna mkesha mmoja zilipigwa kanisani padri anaendelea na ubatizo kisa jamaa mmoja alijamba tu...
tukiwa tunaimba kwaya mara wazamiaji wa kwenye mkesha wakanzisha huko ikabidi ibada isimame.. jenerata ikazimwa makusudi na wababe kukawa giza zilipigwa ovyo ovyo yani unatembea huku unarusha ngumi kujiokoa wachache walikuwa na tochi walisaidia japo nao walikuwa wanamulika watoke mbio hakuna namna..

Finaly Mkong'oto nilioupata mimi kwa kuanzisha vanga ilikuwa mwaka 2011 mr chocolate(Bob junio) walikuwa wamekuja na bonge la nyau mahala fulani kufanya show. kwnye mida ya usiku kama saa7 wakatoka club likabaki la manyani sasa........ nilipigwa na jamaa niliyedhani na mu mudu asee masela wangu wote wakaniachia msala siku 3 uso umevimba sitoki nje masela wananiuguza japo walinikimbia asee.

MAMBO YANABADIRIKA SANA
Enzi hizo washamba mlikuwa wengi kuliko Sasa....
 
Hiki kitu hata mimi nimekuwa nikijiuliza mara kadhaa...

Kijijini kwetu kulikuwa na mnada wa kila mwezi, ilikuwa ni nadra sana. Angalau kila mwezi lazima ugomvi utokee. Ninapoongea ugomvu siyo wa kupigana ngumi tu, ugommvi wa kuchomana visu. Kiufupi ni kuwa kila mnada ilikuwa lazima mtu afe au ajeruhiwe vibaya sana...

Kwenye mikesha ya sikukuu na sikukuu zenyewe ndo usiseme, zilikuwa zinapigwa sana ngumi mitaani. Kuna mkesha mmoja pardi alizichapa na waumini kwenye kilabu cha pombe.

Wanawake walikuwa wanapigwa sana na waume zao. Ilikuwa ni kawaida kila wiki kusikia mwanamke anapiga kelele yavilio kisa kupigwa. But now nipo mkoani kwetu mwezi wa tanoo huu sijawahi kusikia mwanamke analia kwa kipigo, kweli zama zimebadilika.

Mimi nilikuwa mpole na muoga sana, lakini nilikuwa nalazimika kupigana sababu ya kuwa usipopigana unaonekana kama mtoto wa kike.

Siku hizi hizo mambo zimepungua kwa sababu

1. Ugumu wa maisha; Zamani watu walikuwa na uhakika wa chakula ndo maana walikua wanapata nguvu na mawazo ya kupigana. Siku hizi maisha magumu, mtu anakula mara moja kwa siku nguvu za kupigana anazitoa wapi?

2. Afya: Watu wa zamani walikuwa na afya sana, mnadundana ngumi kavukavu lakini fresh tu. Siku hizi unamuona mtu mzima kumbe ana magonjwa kibao. Ukimpiga ngumi moja kazima. Unapata kesi ya mauaji

3. Polisi kuongezeka: zamani hasa vijijini ilikuwa ni nadra sana kuona polisi. Kwa hiyo ugomvi mwingi ulikuwa unaisha kienyeji tu. Siku hizi polisi wamekuwa wengi na kama mjuavyo kuingia polisi ni bure ila kutoka ndo kipengele. Hii imesababisha watu wapunguze ukorofi...

4. Elimu na kustaarabika: Zamani ilikuwa kawaida kuona mtu anajisifia ubabe wa kupiga watu, lakini siku hizi baada ya watu kuelimika wanaona hayo ni mambo ya kijinga. Ubabe wa sasa ni kuwa na pesa nyingi...

5. Masculinity: Nadhani pia homoni za kiume zilikuwa juu sana zamani na kama tujuavyo uanaume unaendana na kuwa aggresive. Lakini siku hizi wanaume tumekuwa siyo aggresive kama zamani. Unakuta mwanaume yupo tiktok yupo busy anasema 'tap tap screen guy, please send me gifts' Huyu ukimwambia apigane anaona kama unampa laana...​
Sasa mkuu wangu Kwan yeye mwamba kuwa tiktok kuna ubaya ugani(japo mimi sipo huko)natumia jf, insta, na WhatsAp bas
 
Sasa mkuu wangu Kwan yeye mwamba kuwa tiktok kuna ubaya ugani(japo mimi sipo huko)natumia jf, insta, na WhatsAp bas
Kama umeshawahi kuingia tiktok unakuwa unaelewa nini namaanisha. Kama hujawahi basi nikuambie tu, wanaume wa tiktok ni walaini sana.
 
Umesahau kitu kimoja🤣kuanzia 1990-2009 kama Jina lazima ujiite Jina kingereza la kimafia utasikia "crazy gun""", knife seven, snake man, ninja B, alafu lazima muwe na makundi mzee mnashindana kudance si unajua sisi ugomvi wetu ulikuwaga ni sambili usiku tunakutana uwanjani watu kama 40🤣Dah utoto Raha sana
 
Nchi imekuwa ya hovyo sana hii, yaani Mwaka unaisha sijapiga ngumi watu watatu wanne?

Ajabu zaidi eti hata kwenye ndoa mwaka unaisha Mwanaume hujamweka Ng'eu Mkeo
 
Umesahau kitu kimoja🤣kuanzia 1990-2009 kama Jina lazima ujiite Jina kingereza la kimafia utasikia "crazy gun""", knife seven, snake man, ninja B, alafu lazima muwe na makundi mzee mnashindana kudance si unajua sisi ugomvi wetu ulikuwaga ni sambili usiku tunakutana uwanjani watu kama 40🤣Dah utoto Raha sana
Mkuu ngumi zilikuwa zinapigwa si watoto tu hadi mibaba ya family tena kwa kosa kidogo zinawaka.Zamani kudaiana mwisho siku 2 ya tatu zinapigwa na deni ndo linaisha hivyo.

Babu alikuwa anatusimulia kuwa alimkopesha mtu ngozi za ng'ombe idadi nimeshahu ila kwa gharama ya zote ni sh100.Siku waliyokubaliana atamlipa ikapita hakuja ksho yake vilevile siku tatu akaendapo kwakwe mapema saa 12 asbh akapiga hodi mke wa jamaa akatoka akasema ameondoka sasahivi tu.

Babu akamwambia basi akija leo mwambie hela yangu aniletee mwanamke akajibu sawa nitamwambia kumbe jamaa alikuwamo tu mle ndani bana.

Siku ya pili yake babu akaenda saa11 maelezo yakawa yaleyale ametoka sasahivi tu.Babu akaaga .Siku ya tatu akenda na yale mafyekeo ya kuunda yali tumikasana kufyeka kwenye mashamba ya mpunga.

Alipofika hakugonga hodi wala nini akakaaa mlangoni bya saa12 jama akasika anamwambia mke wake leo flani naona amechoka kuja kudai hela yake bana mwanamke akacheka akasema nilijua atachoka tu.

Jamaa ile kutoka nje ya mlango tu akakwidwa ngumi mke wake akatoka aje asaidie akapigwa pia.Babu alikuwa na vile viberti kama vya gesi kwa sasa lakini kipindi hicho walikuwa wanaweka mafuta ya taa na kinakuwa na utambii.Akakiwasha na kuchoma ile nyumba ya nyasi majrani wakasikia zile kelele wakawahi kuokoa jamaa kapigwa hajitambui.
 
Umenikumbusha tulikuwa kwenye mkesha wa mwaka mpya mara hali ya hewa ikabadirika ghafla tulivumilia lakini tukashindwa paroko akaagiza aliye rusha hilo yai akamatwe tumpelekee...mayai visa kumbe yalikuwa mengi bana tulipondwa na hatukurudi kanisani tena
😂😂😂😂 alafu mrushaji hamu muoni
Mnaoga uozo na harufu
 
Nilishuhudia Mtu kamwagwa utumboo hivhivi mkesha wa sikukuu, akatishiwa utumbo ukipigwa na upepo tu baaasi biashara yake dunian imeishia hapo,
 
Unaongelea mavarangati ya juzijuzi tu, we kumbe bado dogo uliza wakongwe wakuambie vagi za enzi zao kwenye madisko na mikesha nyie mkasome. Unaambiwa hapohapo kwenye madisko ya shuleni wahuni wa mitaani walikuwa wanakuja na kucheza na mademu zenu wa hapohapo shuleni mnanyang'anywa. Mkono ulikuwa unapigwa haswa kati ya ya raia na wanafunzi au wanafunzi kwa wanafunzi kugombea mademu wa kucheza nao disko la welcome form one/form five na lile disco la kuhitimu form four/six
Shybush enzi hizo Mkuu umenikumbusha tuliingia Mgodini Mwadui sec kubeba mademu aiseeh hiyo vita kama Gaza
 
Umenikumbusha mbali sana , hata siku za x-mass mkono ulikuwa unaopigwa hadi sio poa , sisi home tulikuwa men 12 aisee tulikuwa tunapiga mkono mtu akizingua kata nzima walikuwa wanaelewa , unakuta tena zilikuwa fujo zinaanzia kwenye mpira au madamu kuna siku ndugu yetu anaenda skuli asubuhi jamaa anakuta wanamsubili ikabidi arudi home , tukaamsha wote aisee zilitembea pale jamaa walikalishwa ikabidi wakimbie .
Tangazo la chai JABA hili
 
Shybush enzi hizo Mkuu umenikumbusha tuliingia Mgodini Mwadui sec kubeba mademu aiseeh hiyo vita kama Gaza
Kuna disco moja sisi tukiwa form3 tulifanya fujo sana tukabeba spika na betery la gali na kila kitu kinahitajika tukaenda kugonga kengele saa5 usiku halafu disco likaanza hapohapo shulen walimu walikuwa wanauliza kuna nini lakin?

Tulicheza kumbe wanazengo hawajakubali ulirushwa mkuki ukatua hakuna ayebaki hata wanazengo nao hawakubaki maana tulikimbia ovyo kila mtu. Jtatu mwalimu akatangaza kabla hujatajwa jina lako na unajijua kabisa ulikuwepo hapa unacheza disco pita mbele hakuna aliye tokea ikabidi watuambie tupige kura ajabu tuliwaandika walimu alio kuja kuangalia kulikoni na wao walikuwa wanatujua kabisa lakin hayupoaliyetaja mwanafunzi hata mmoja
 
Back
Top Bottom