Sasa mke wa Makonda ana kosa gani hadi azuiliwe kuingia Marekani?

Na Lemutuz?
 
OK sasa wanaharakati tutaandika barua kwenda embassy kuwa taarifu kuwa marafiki zake akina lemutus, musiba, na hao wasanii, wasiruhusiwe kuingia Us
 
Hata wewe kama unataka kulipa kisasi basi hakikisha unakilipa hata kwa uzao wa mhusika kwani hapo ndipo ambapo kisasi huumiza. Yeye pekee anakuwa amejiandaa kupokea matokeo, unapoumiza wapendwa wake unamvuruga haswa. Ndio maana watu wenye roho mbaya kama akina Hitler hajulikani mwanawe hadi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu waliuliza hivyo hivyo kwa grace Mugabe
 
Nimeshangazwa sana na katazo la mke wa RC kuingia nchini Marekani. Yeye binafsi ana kosa gani?!

Naomba Pascal Mayalla na Nyani Ngabu mkuje hapa kunitoa tongotongo.

Nawasilisha!
Mbona hujashangaa na ndugu zake wa karibu kupigwa ban? Au umemwona mke wake Makonda tu. Hata baba yake, kaka/dada zake, mama yake, wakwe zake sasa ni marufuku kukanyaga States
 
Mke ndiye anaemuwezesha Makonda nguvu za kwenda kudhulumu haki za watu kuishi,kwa kumwandalia musosi unaompatia nguvu ya kubeba rungu na kukandamiza kwenye vichwa vya wale wanaodhulumiwa haki ya kuishi.
 
Kwani Marekani ni mbinguni? Au ukiingia marekani unapewa hela za bure? Au ukiingia marekani ni alama ya kufanikiwa na kutoka kimaisha? Marekani kuna nini mpaka kutishia watu "URUHUSIWI KUINGIA NCHINI MAREKANI" This is the highest level of stupidity!
 
Wiki ijayo EU nao lazima wampige ban maana USA na EU ni ndugu moja
 
Mkuu kuna kupatilizwa... kwani ndio umesikia leo kwa mara ya kwanza?
 
Hahaha labda wamarekani wanaamini ukilala na shetani lazima nawe uwe shetani.

Watatueleza tu, tuwape muda kwanini mkewe naye asiende huko Marekani.

Hivi kwani alikuwa anakwenda sana hadi watangaze kumzuia?!
 
Nimeshangazwa sana na katazo la mke wa RC kuingia nchini Marekani. Yeye binafsi ana kosa gani?!

Naomba Pascal Mayalla na Nyani Ngabu mkuje hapa kunitoa tongotongo.

Nawasilisha!
Hivi wewe mke ni nani kwako. Mbona vitu vidogo tu vinatushinda. Mke ni part ya mwili wako
 
Nimeshangazwa sana na katazo la mke wa RC kuingia nchini Marekani. Yeye binafsi ana kosa gani?!

Naomba Pascal Mayalla na Nyani Ngabu mkuje hapa kunitoa tongotongo.

Nawasilisha!
Siyo mke tu , hata watu wote walio karibu naye wameungua , Kunatakiwa uangalifu sana kwa kundi la wasafi na hasa Diamond , kuna taa nyekundu inawaka kwamba ana uhusiano wa karibu na Makonda , kuna hatihati akatajwa miongoni mwa watakaopigwa pini .

Nachukua nafasi kurudia tena kuwaasa vijana wenye ndoto kubwa waache kuchangamana na watu waovu hata kama waovu hao wana madaraka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…