Sasa mke wa Makonda ana kosa gani hadi azuiliwe kuingia Marekani?

Sasa mke wa Makonda ana kosa gani hadi azuiliwe kuingia Marekani?

Nimeshangazwa sana na katazo la mke wa RC kuingia nchini Marekani. Yeye binafsi ana kosa gani?!

Naomba Pascal Mayalla na Nyani Ngabu mkuje hapa kunitoa tongotongo.

Nawasilisha!

Hizo ni mambo ya kimataifa ambako kiusalama wanaamini wanufaika wako na wewe lenu ni moja, so wanaona kama umepigwa ban ni wewe na familia na watu wako wa karibu!

Ni policy za kimataifa hata kwenye ajira etc kuna hayo mambo!
 
Nimeshangazwa sana na katazo la mke wa RC kuingia nchini Marekani. Yeye binafsi ana kosa gani?!

Naomba Pascal Mayalla na Nyani Ngabu mkuje hapa kunitoa tongotongo.

Nawasilisha!
Hata mimi nimeshangaa sana. Ngoja na sisi tuwawekee vikwazo vya kiuchumi
 
Soma paragraph ya 3 mstari wa 4. Sababu ni "The law also requires the Secretary of State to publicly or privately designate such official and their immediate family members"View attachment 1343469

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa mujibu wa sheria ina maana Makonda na mkewe designation yao ni public hivyo inawezekana kuna watu wake wa karibu wamefanyiwa kimyakimya,akili zitawakaa sawa siku wakienda ubalozini na kunyimwa Visa.
 
kwa sisi ambao hatuna uhakika wa kufika huko ni kawaida sana ila kwa ambaye ana uwezo wa kufika huko na akazuiwa na pigo kubwa sana,,ni sawasawa na kumwambia mbongo asikanyage Dar na ashawahi fika na ana uhitaji wa siku nyingine kufika Dar.
Kwani Marekani ni mbinguni? Au ukiingia marekani unapewa hela za bure? Au ukiingia marekani ni alama ya kufanikiwa na kutoka kimaisha? Marekani kuna nini mpaka kutishia watu "URUHUSIWI KUINGIA NCHINI MAREKANI" This is the highest level of stupidity!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Nicolae Ceausescu wa Romania alipigwa risasi yeye na mke wake mbele ya hadhara.

Haiwezekani mume awe muuaji, mke asijue. Na kwa sababu anajua, na akakubali kuendelea kuishi na muuaji maana yake ni kuwa anaunga mkono uuaji, hivyo anakuwa sehemu ya muuaji.
 
Back
Top Bottom