ruaharuaha
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 3,586
- 3,857
Trust me sumu aliyoicha Magufuli bado ipo ni baada ya miaka kumi mpaka kumi na tano itadhihirika.
Aliifundisha falsafa yake kwa miaka 5 na miezi 5 ukiachana na wakati wa uwaziri wake ambapo alisimamia viwanja vya ndege,Barbara ya lami dsm to mtwara n.k
Vituo vya kupimia uzito na barabara za ndani ya mji wa dsm kasimamia akiwa waziri mpaka kuwa raisi.
Binafsi huwa naona walichelewa kumkata upepo kwa hizi project tatu kwa kuwa alizianza.. Project ya umeme, reli ya kati ,hamasa ya kufundisha uzalendo juu ya nchi na kutetea watu masikini licha ya kuwa walimpakazia hataki matajiri ili hali alitaka matajiri wasio wanyonya na kudhulumu watu masikini.
Kazi ya dkt. JPM ipo kwenye mioyo ya watu haswa wenye maisha ya kawaida na kati nimepita sehemu nyingi watu wakiona picha yake huwa wanasema hivi " Alikua mwanaume"
Binafsi najua hakutaka upinzani ili apoteze muda wa kubishana alitaka kazi na kushauriana maendeleo(hapa ndipo wengine waliona hataki kushauriwa na kukosolewa kumbe aliwaza akitimiza hayo watanzania wata anza kujitegemea kiuchumi)
Bahati mbaya project zake zilihitaji aishi zaidi ya ile siku aliyopangiwa atuache bila kujua ilikua hiari yake, Mungu au maadui ndio walipanga isipokuwa siku ya kumuaga kijazi alivyodiriki kusema hata yeye anaweza kufa nilihisi kifo chake kinaweza kutokea lakini nilijua ni raisi isingewekana lakini Mungu ndio mpangaji asipotaka ufe hata kama adui kakudumbukiza baharini na jiwe utatoka ila haya yote ni Siri ya muumba.
Kisha umaliza mwendo, bei za vifaa vya ujenzi ni hatari kikubwa matumaini tunayopata na mageuzi ya muda mfupi mengine tuyape muda .
Lala salama Dkt .John Pombe Magufuli.
Ndugu zangu
Sasa ndio nimeelewa kauli ya kusema nimesacrifice maisha yangu kwaajili ya watanzania maskini.
Nimeelewa hivi kiongozi kusacrifice maisha yake kwaajili ya watanzania ni kitendo cha kutumia fedha zote za umma kuijenga Tanzania na kukataa kushirikiana na viongozi wenzake wenye nia ya kuiba, kudhulumu, kuhujumu na kufisadi mali na fedha za umma.
Mtanzania mwenzangu wewe unaelewaje.
Tafadhali toa maana yako.
Huu uzi sio kwaajili ya kuwasema watu bali ni uzi, tunataka tupate maana ya kusacrifice maisha maana yake nini. Kila mmoja ajikite kwenye kutoa maana badala ya kuwasema watu.
Sacrifice, Sadaka ni kujitoa kwa moyo wote kusaidia kulipigania Taifa lako, watu wote. Wanajeshi wanafanya hivyo.
Umeme na maji, barabara, reli ya kati, SGR, umeme wa kudumu.bwawa la rufiji, mikataba ya maana ya madini, elimu bure (watoto millioni kumi) hospitali vituo vya afya nchi nzima, nidhamu serikalini ndio maana ya Sadaka. Kujali watu wako, rasilimali zake na jinsi zinavyotumika kuwasaidia wengi.