Sasa ni dhahiri Bungeni kuna kundi la Rais Samia na kundi la Hayati Magufuli. Spika Ndugai awataka wabunge wa CCM kuitisha kikao cha usuluhishi

Kwani kuna vyama vingapi mle ndani, mm nadhani kikao wangekifanyia mlemle tu ndani, na bunge lenyewe halipo live
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana...
Kwahiyo kunakundi dhuluma na kundi haq
 
Mama achukue hatua na hiyo hotuba yake ya alhamisi iwe clear kabisaa asipepese maneno maana watamzingua.

Hapa kuna watu hawako tayari kuona Mzanzibar anakuwa Rais na mama anataka fair Kati ya Zanzibar na Bara,hiki ndicho wanaona ni tatizo maana mwendazake aliwakanyaga Wazamzibari.

Mwisho mama atumie nguvu zake za kumiliki dola kuwazima baadhi ya watu akitaka kumfurahisha kila mtu ataumia yeye,bahati nzuri au mbaya shida iko ndani ya CCM yenyewe.

Option ya mwisho ni kuwa Mwenyekiti wa chama,anaweza vunja bunge aanze upya kwenye uchaguzi maana aweke watu Royal kwake Ili mambo yaende.
 
Kama Samia ana akili. Arudie uchaguzi wa Ubunge alaf wale team Magu awang’oe. Hiyo ndo solution
Uchaguzi wa wabunge hufanyika kila baada ya miaka 5 na ni takwa la kikatiba na si uamuzi wa mtu binafsi.

Hivyo Rais hawezi vunja bunge kabla ya muhula.
 
HE!! BADO WANADEMKA!!!!
 
Uchaguzi wa wabunge hufanyika kila baada ya miaka 5 na ni takwa la kikatiba na si uamuzi wa mtu binafsi...

Hivyo Rais hawezi vunja bunge kabla ya muhula...
Kwa taarifa yako anaweza. Vipo vigezo vinavyoweza kumfanya avunje bunge na kuitisha uchaguzi. Soma vzr katiba hiyo ya miaka mitano ni kigezo kimoja wapo.
 
Spika wa Bunge Job Ndugai amemuagiza Katibu wa wabunge wa CCM Jasson Rweikiza kuitisha kikao cha kamati ya wabunge wa CCM (party caucus) kwasababu ndio mahali wanaweza kudhibitiana.
Yeye mwenyewe Ndugai yupo kundi la Mwendazake. Hamkubali Rais Samia. Halafu wabunge wote wa kanda ya Ziwa kwa ukabila na ukanda wao wanaendelea kumlilia Mwendazake.
 
Nilichogundua ni kwamba wabunge wa Kanda ya Ziwa na wabunge wa Dodoma lao moja. Wale wa Dodoma wanamwona Mwendazake amewajali kwa kuhamishia makao makuu Dodoma na hivyo kuleta mzunguko wa fedha hapo Dodoma, na wale wa kanda ya ziwa wanateswa na ukabila na ukanda, yaani "Mtu wetu".
 
Kwa taarifa yako anaweza. Vipo vigezo vinavyoweza kumfanya avunje bunge na kuitisha uchaguzi. Soma vzr katiba hiyo ya miaka mitano ni kigezo kimoja wapo.

Akivunja bunge maana yake hata yeye anapoteza sifa za kuendelea kuwa Rais.

Hivyo unaona hapo hakuna dhamira ya moja kwa moja kwamba Rais avunje bunge ili tupate tu wawakilishi/wabunge wapya pekee bali hata yeye cheo chake anakiweka rehani.
 
Jana bungeni kuna kihoja cha mwaka kimetokea. Mbunge wa CCM Lucy Mayenga alimwaga chozi akikemea wabunge wenzie wa CCM wasimsifie Rais mpya mama Samia ila wamsifie Hayati Marehemu Magufuli tu.

Hiki i kioja kwa kuwa ni juzi tu mama Samia aliwaonya wabunge waache KUDEMKA (kujadili utumbo wa kumfananisha yeye na marehemu hayati Magufuli) ila wajikite kujadili bajeti.

Wataalam wa siasa wameshauri mam Samia awafute uanchama wabunge kama hawa kwani hawana hata sababu za kumpinga isipokuwa kutengeneza makundi ndani ya chama.
 
Kumsifia marehemu Haisaidii, Wabunge wabadiri mawazo kwani rais ni Samia Suluhu Hassan sio Marehemu Magufuli.Wafu hawajui lolote na kumbukumbu Leo limetoweka wabunge wajilite , washirikiane na mama Mambo yawndelee.
 
Wewe ni muongo wa kiwango cha SGR. Inawezekana hata hujamsikiliza huyo umsemaye. Kumbuka JF kuna werevu kuliko wewe...bure kabisa!
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nimecheka hadi machozi

Naomba kavideo ka niendelee kucheka tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…