Sasa ni dhahiri kuwa Yanga waliupiga mwingi mwaka 2022, Simba haijafika kiwango kile cha Yanga

Kichaka cha medali mmehama mmehamia ball possession 😂
 
Berkane unamfanisha na Usm Alger.... huwaoni vichaa wenzako wanavyokaa kimya kuepusha hizi aibu ndogo ndogo....
 
Pamoja na ukweli kuwa Yanga na Simba zote zimecheza fainali ya Kombe la Shirikisho, tena na timu za Afrika ya Kaskazini, Yanga inabaki kuwa na fainali bora kuliko Simba.

Yanga ilicheza fainali na USM Algier ya Algeria ikianzia nyumbani Benjamin Mkapa. Ikalala 2-1. Mchezo wa pili kule Algiers, Yanga iliibuka kwa ushindi wa 1-0.

Katika fainali hiyo, mabao manne yalifungwa na kila timu ilifunga mabao mawili. USM Algier walibeba kombe kwa kunufaika tu na bao la ugenini. Aggregate ilisoma 2-2!

Soma Pia: Simba 1-1 RS Berkane| Agg: Simba 1-3 RS Berkane | RS Berkane Bingwa CAFCC 2024/205

Mwaka huu Simba amecheza fainali na RS Berkane ya Morocco. Kule Berkane, Simba amezabwa mabao 2-0. Leo kule Amaan Zanzibar, amepata sare ya 1-1. Aggregate ikasoma 3-1.

Mwaka huu pia, yamefungwa mabao manne kwenye fainali. Kati ya hayo, Simba wamefunga moja tu. Na wamepigwa magoli matatu. Berkane hakuwa na haja ya kunufaika na bao la ugenini.

Hadi hapo, ni dhahiri kuwa Yanga waliupiga mwingi mwaka 2022. Si sawa na Simba. Simba wasijifananishe na Yanga kwenye performance.

Hatimaye, nchi imepoa!

Sisi Yanga njia yetu ya kufika fainali ilijaa wajinga wajinga wengi
Marumo nusu fainali, afu ligi ya nyumbani kwake kashuka daraja

USMA fainali, ila ligi ya nyumbani nafasi ya sita

Simba njia yake imejaa timu ngumu na ukizingatia uchanga wa kikosi chao
Stellenbosch nusu fainali, ligi ya nyumbani nafasi ya tano
Berkane fainali, ligi ya nyumbani ndio bingwa

Kwhyo kwa minajili hio Simba licha ya uchanga wa kikosi Chao ila wamepambana sana

Nawapa kongole watani, nyie ni wakomavu ktk Caf championship
Na isingekuwa refa kuja na maagizo yale basi leo Tz ingeandika historia
 
Berkane unamfanisha na Usm Alger.... huwaoni vichaa wenzako wanavyokaa kimya kuepusha hizi aibu ndogo ndogo....
Usiwe na akili za kushikiwa,,unajua timu alizokutana nazo Simba mpaka fainali zote zilikuwa famba? Akuna timu ata Moja ilishuka kutoka klabu bingwa kuja kucheza shirikisho msimu huu,,kwa maana iyo zilibaki zile timu mbovu mbovu tu zipambane zenyewe,,usilinganishe na yanga timu zilizokuwa zinashindwa kule klabu bingwa zilikuwa zinakuja kucheza shirikisho kwaiyo yanga ilikuwa inakutana na mabingwa wa nchi zao wengi tu
 
Usm Alger alikua bingwa wa nchi gani?
 
Ilikuwa nini
13ade7476a6346eba485e9d3e84d33e7.jpg
 
Usiwe na akili za kushikiwa,,unajua timu alizokutana nazo Simba mpaka fainali zote zilikuwa famba? Akuna timu ata Moja ilishuka kutoka klabu bingwa kuja kucheza shirikisho msimu huu,,kwa maana iyo zilibaki zile timu mbovu mbovu tu zipambane zenyewe,,usilinganishe na yanga timu zilizokuwa zinashindwa kule klabu bingwa zilikuwa zinakuja kucheza shirikisho kwaiyo yanga ilikuwa inakutana na mabingwa wa nchi zao wengi tu
Kwa hiyo kule Morocco bingwa ni mama ako sio Berkane!
 
Alafu usisahau mwenyeji kapata shoot on target 1 tu akiwa nyumbani,,kule ugenini akupata ata Moja na ndio timu iliyokuwa inajimwambafai kubeba kombe sijui wangeliiba au namna Gani🤣
Fuatilieni mpira vilaza nyinyi. Unaweza kuwa na attempt 10 na zero shot on target. Mpira kugonga mwamba ,mlingoti au kupita juu ya lango kama attempt ya kapombe leo hizo zote sio shot on target lakini je sio hatari ya kupata goli? Vilaza mmekariri shot on target.
 
Ndio maana wakawa mabingwa.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Fuatilieni mpira vilaza nyinyi. Unaweza kuwa na attempt 10 na zero shot on target. Mpira kugonga mwamba ,mlingoti au kupita juu ya lango kama attempt ya kapombe leo hizo zote sio shot on target lakini je sio hatari ya kupata goli? Vilaza mmekariri shot on target.
On target iyo ni yakwako unajua maana ya on target? Kwaiyo wewe ni mtaalam zaidi kuliko rekodi za Azam tv? Umepagawa eti
 
Fuatilieni mpira vilaza nyinyi. Unaweza kuwa na attempt 10 na zero shot on target. Mpira kugonga mwamba ,mlingoti au kupita juu ya lango kama attempt ya kapombe leo hizo zote sio shot on target lakini je sio hatari ya kupata goli? Vilaza mmekariri shot on target.
Shot on target ni nusu goli!..
Kwamba kama si kipa inakuwa goli!

Sasa mpira kugonga mwamba hata kama kipa hayupo inakuwaje goli?
 
Back
Top Bottom