Sasa ni dhahiri Rais wetu Magufuli amekwama

Jiwe ni jiwe kwenye kupambana na upinzani na sio mengine Kama ufisadi,ajira, uchumi,umoja huku jiwe ugeuka ni kokoto tu.
Saa hizi kila kukwama atasingizia corona ndio itakayobebeshwa lawama
Huko tunako kwenda hata ikitokea mwanaume kamshindwa mkewe kumpa tiba usiku, watu watasingizia Mkulu. Mpeni nafasi apumzike. Yeye ni binadamu pia.
 
As long as wagonjwa wanaendelea kupona Mimi binafsi sioni haja ya kumshutumu hpa.

Idadi ya maambukizi na vifo bado iko chini sana ukilinganisha na nchi nyingine. Pia hao wabeberu wa WHO ni ujinga tu ndo umewajaa kwa kusema kuwa Tanzania hatuchukui hatua serious kwenye huu ugonjwa wakati wao nchi zao kila siku idadi ya wagonjwa na vifo inaongezeka,sasa kwa macho ya kawaida kati ya sisi na wao nani hayuko serious na haya mapambano ya covid-19?

Tumuunge mkono Rais wetu kwenye hili jambo na namna tunavyoenda nalo ili mda wa kushinda hii vitu basi wote nchi nzima tuwe ni washindi.
Supported

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi ni msomaji mzuri sana wa makala za Pascal mayalla, kunatoafauti kubwa ya uandishi wake from the day ameitwa bungeni. Hata Mimi kidogo nilipata mashaka kwa kuona ameanza kuandika makala Kama za gazeti la uhuru.lakini ni kinyume chake bado ni mwandishi anayetumia akili na kalamu yake kwa umakini sana hasa kwenye kipindi hichi ambacho media imewekwa mfukoni. Ukitaka kuamini hilo soma between lines alichokoandika kuhusu ushindi wa ccm serikali za mitaa.ukisoma juujuu utahisi amesifia lakini kiuhalisia amekejeli sana kwenye ile makala.pascal ikitokea magufuli akampa udc let say Kama watu wanavyomtabiria, itakuwa ni kwa factor nyingine tu Ila kwenye kujipendekeza hayupo....soma vizuri anachoandika utaelewa ninachokiongea

Sent using Jamii Forums mobile app
Naunga mkono hoja umedadavua vizuri sana,jamaa anatumia akili sana kufikisha ujumbe wake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duh Pascal Mayalla hio ni kweli au sarcasm ?
Kule US Trump aliwambia watu wanywe Jik baada ya kukandiwa akasema alikua anafanya istizai.
Uzuri wa corona haichagui hata uwe nani ukikaribia unaikwaa
Ila ukweli tume kwama kabisa kwenye hii issue imebaki maombi tu.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Katika hotuba aliyoitoa Rais wetu hivi karibuni kule Chato, kuna mambo kadhaa ambayo yanatuonesha kwamba hali ya nchi kwa sasa ni tete:

1) Kwamba Rais yuko Chato kwa muda mrefu sasa
kwa kawaida Rais wetu Magufuli huenda Chato kwa mapumziko. hivi sasa ni muda umepita tunaona Rais yupo Chato. Corona ilipoanza kuchanganya, Rais wetu aliondoka Dar na kubanisha pale Dodoma, makao makuu. tulishuhudia Rais wetu akifanya MEDITATION kwenye majabali.

Naona baadaye akaona hiatoshi, akaamua kwenda mbali zaidi na hii Corona. na sasa tumeshuhudia akitoa Major Speech yake kutoka Chato. pia ni vema kukumbuka kwamba Rais wetu huwa ni mwoga sana wa majanga. amekuwa na kawaida ya kujitenga mbali na majanga, na kumwachia PM wake. hali kwa sasa ndio hiyo hiyo. Kamanda mkuu kaingia mitini. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

2) Hotuba inayochanganya
Katika hotuba aliyotoa, badala ya kutoa mwanga katika mapambano na Corona, imeleta giza. badala ya kutia matumaini, imeleta hofu zaidi. siyo ajabu sekeseke la Amana lilifuatia mara moja. Hotuba yake inaonesha anatumia zaidi uelewa wake na hisia zake, badala ya kutoa msimamo kutokana na sayansi ya kisasa kabisa, utafiti mpana, mjadala makini na wasaidizi wake, ushauri mpana na makini, na tafakari iliyo pevu. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

3) Anaongea na wakuu wa vyombo vya usalama
Rais Magufuli siku zote anapenda sana majeshi. akikwama popote pale anaita majeshi, na ni zaidi ya Rais yeyote aliyemtangulia. akikwama ujenzi, Jeshi. akikwama madaraja, Jeshi. na hata katika lile JANGA ALILOCHUMA MWENYEWE, JANGA LA KOROSHO, aliita jeshi. Katika kipindi hiki alichochanganyikiwa kabisa, aliona badala ya kuita maprofesa wa tiba na wataalamu wa magonjwa, wizara ya afya na wizara zingine, au hata Task force aliyounda mwenyewe kupambana na Corona, aliita wakuu wa vyombo vya usalama, majeshi.

Na kama alivyoita wanajeshi ili ikiwezekana wabangue korosho kwa buti, kasema wazi kabisa kwamba anataka kutumia jeshi kupambana na korona. na kweli, IGP akatafakari atafanya nini hapa kwa kutumia upolisi wake, akaamua kufanya kile ambacho wengi walishasema siku nyingi. kuzuia raia wa kutoka nje. sasa tunasubiri CDF Mabeyo yeye atafanya nini , atoe amri wanajeshi waitandike buti Corona? Au yule wa Magereza aitie gerezani Corona? Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

4) Visingizio vya ajabu
Labda katika hali inayoonesha kukwama zaidi, Rais ametoa visingizio. Badala ya kufuata njia sahihi za kukabiliana na Corona, aliamua kuziba masikio na kupokea sifa kutoka kwa wale waliomuona kwamba ni shujaa pale mwanzo.

sasa vifo vinaongezeka kwa kasi, analaumu dawa za kupulizia, analaumu kwamba pengine amehujumiwa kwa kuletewa Barakoa zenye virusi vya Corona! Huyu ni mtu asiyetaka kubeba lawama begani na kujisahihisha. kukubali na kukiri alikosea, na kusonga mbele. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.
Duh....napita

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mimi ni msomaji mzuri sana wa makala za Pascal mayalla, kunatoafauti kubwa ya uandishi wake from the day ameitwa bungeni. Hata Mimi kidogo nilipata mashaka kwa kuona ameanza kuandika makala Kama za gazeti la uhuru.lakini ni kinyume chake bado ni mwandishi anayetumia akili na kalamu yake kwa umakini sana hasa kwenye kipindi hichi ambacho media imewekwa mfukoni. Ukitaka kuamini hilo soma between lines alichokoandika kuhusu ushindi wa ccm serikali za mitaa.ukisoma juujuu utahisi amesifia lakini kiuhalisia amekejeli sana kwenye ile makala.pascal ikitokea magufuli akampa udc let say Kama watu wanavyomtabiria, itakuwa ni kwa factor nyingine tu Ila kwenye kujipendekeza hayupo....soma vizuri anachoandika utaelewa ninachokiongea

Sent using Jamii Forums mobile app
Sema Pascal siku hizi anacheza miguu yote na Ndugai hawezi kujua akabe mguu gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umeeleza vizi kabisa mm sina cha kuongeza ila namwambia rais ajiandae kutoka ikulu arudi chato kulima kuongoza watu hawezi na katika kipindi hiki kigumu ndipo anaonyesha namna gani hawezi kutuongoza watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi limekatika breki mteremko wa mlima wa Kitonga, dereva ameruka nje kawaacha abiria waangamie. Kilangila.
 
Mkuu Mindi, jee unafahamu wagonjwa wa Corona wanaokufa, huwa wana issues gani kabla?.

Jee unajua health status ya mtu wetu kama na yeye ana any issue, kakolona kakipita kanakula kichwa?.
Do we have to take such risks?. Kama huko alipo is safe heaven, let him be there for as long as it takes.
P.
Hili kweli wengi tulikuwa hatujalifikiri. Wataalamu wamesema corona ni hatari sana kwa wazee, watu wenye maradhi yaletayo udhaifu mwilini kama pressure, TB, Asma , nk. Hii inaonyesha pengine kiongozi wetu ana udhaifu Fulani ambao wale jamaa kitengo wameona ni risk kumuacha kuwepo Dar au Dodoma ili kuepuka kabisa maambukizo.
Anatatizo gani? Hiyo siri ya ugonjwa watajua wenyewe lakini kwetu lakujiuliza kuna sababu ya kuwa na kiongozi mgonjwa aliye hatarini kuwa akiambukizwa kidogo ni kasheshe?
Haya wamemficha kijijini, mbona hatulii tunamuona vijiweni ananunulia watu kahawa? Au anaamini pale hakuwezi kuwa na mwenye maambukizi?
 
Wataalamu wamesema corona ni hatari sana kwa wazee, watu wenye maradhi yaletayo udhaifu mwilini kama pressure, TB, Asma , nk.
Mkuu Chakaza, lets don't assume and insinuates anything!. Mkuu wetu yuko kwao Chato kwa mapumziko, na baada ya mapumziko anaendelea na kazi akiwa Ikulu ya Chato akiendelea kupiga kazi kama kawaida, hayo mengine sii yetu, waachie wenyewe!.
P
 
Ushujaa wake upo kwene nn kwene hili swala la Corona ni wazi magufuli anajaribu kuaminisha wananchi kwamba hii issue ni ndgo kuogopa mapato nchi haina fedha hii, raisi ambae ndio kiongozi anajitia eti hajui takwimu ya ile siku, kiongozi bora huonekana kwene majanga sio tu kujenga barabara kwa Kodi za wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha waisome namba eeh
Dogo kapamba moto yeye haisomi namba bali anawasoma Wabongo
1587794449857.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika hotuba aliyoitoa Rais wetu hivi karibuni kule Chato, kuna mambo kadhaa ambayo yanatuonesha kwamba hali ya nchi kwa sasa ni tete:

1) Kwamba Rais yuko Chato kwa muda mrefu sasa
kwa kawaida Rais wetu Magufuli huenda Chato kwa mapumziko. hivi sasa ni muda umepita tunaona Rais yupo Chato. Corona ilipoanza kuchanganya, Rais wetu aliondoka Dar na kubanisha pale Dodoma, makao makuu. tulishuhudia Rais wetu akifanya MEDITATION kwenye majabali.

Naona baadaye akaona hiatoshi, akaamua kwenda mbali zaidi na hii Corona. na sasa tumeshuhudia akitoa Major Speech yake kutoka Chato. pia ni vema kukumbuka kwamba Rais wetu huwa ni mwoga sana wa majanga. amekuwa na kawaida ya kujitenga mbali na majanga, na kumwachia PM wake. hali kwa sasa ndio hiyo hiyo. Kamanda mkuu kaingia mitini. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

2) Hotuba inayochanganya
Katika hotuba aliyotoa, badala ya kutoa mwanga katika mapambano na Corona, imeleta giza. badala ya kutia matumaini, imeleta hofu zaidi. siyo ajabu sekeseke la Amana lilifuatia mara moja. Hotuba yake inaonesha anatumia zaidi uelewa wake na hisia zake, badala ya kutoa msimamo kutokana na sayansi ya kisasa kabisa, utafiti mpana, mjadala makini na wasaidizi wake, ushauri mpana na makini, na tafakari iliyo pevu. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

3) Anaongea na wakuu wa vyombo vya usalama
Rais Magufuli siku zote anapenda sana majeshi. akikwama popote pale anaita majeshi, na ni zaidi ya Rais yeyote aliyemtangulia. akikwama ujenzi, Jeshi. akikwama madaraja, Jeshi. na hata katika lile JANGA ALILOCHUMA MWENYEWE, JANGA LA KOROSHO, aliita jeshi. Katika kipindi hiki alichochanganyikiwa kabisa, aliona badala ya kuita maprofesa wa tiba na wataalamu wa magonjwa, wizara ya afya na wizara zingine, au hata Task force aliyounda mwenyewe kupambana na Corona, aliita wakuu wa vyombo vya usalama, majeshi.

Na kama alivyoita wanajeshi ili ikiwezekana wabangue korosho kwa buti, kasema wazi kabisa kwamba anataka kutumia jeshi kupambana na korona. na kweli, IGP akatafakari atafanya nini hapa kwa kutumia upolisi wake, akaamua kufanya kile ambacho wengi walishasema siku nyingi. kuzuia raia wa kutoka nje. sasa tunasubiri CDF Mabeyo yeye atafanya nini , atoe amri wanajeshi waitandike buti Corona? Au yule wa Magereza aitie gerezani Corona? Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

4) Visingizio vya ajabu
Labda katika hali inayoonesha kukwama zaidi, Rais ametoa visingizio. Badala ya kufuata njia sahihi za kukabiliana na Corona, aliamua kuziba masikio na kupokea sifa kutoka kwa wale waliomuona kwamba ni shujaa pale mwanzo.

sasa vifo vinaongezeka kwa kasi, analaumu dawa za kupulizia, analaumu kwamba pengine amehujumiwa kwa kuletewa Barakoa zenye virusi vya Corona! Huyu ni mtu asiyetaka kubeba lawama begani na kujisahihisha. kukubali na kukiri alikosea, na kusonga mbele. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.
''A desperate president. Clutching at straws.'' I like this
 
Back
Top Bottom