Sasa ni dhahiri Rais wetu Magufuli amekwama

Sasa ni dhahiri Rais wetu Magufuli amekwama

Mkuu Mindi, jee unafahamu wagonjwa wa Corona wanaokufa, huwa wana issues gani kabla?.

Jee unajua health status ya mtu wetu kama na yeye ana any issue, kakolona kakipita kanakula kichwa?.
Do we have to take such risks?. Kama huko alipo is safe heaven, let him be there for as long as it takes.
P.
Nahisi naanza kukuelewa. Ungeongeza sauti kidogo maana kama vile kuna jambo unataka kutueleza, funguka mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal umejibu vizuri Ila mwisho umechapia! Kwa nini imemchukua muda mrefu kuhamia Dodoma kama Ikulu? Ni wazi Ikulu ni zaidi ya majengo na vitanda vya kulalia. Kuna mengi sana ya kuyaweka sawa hasa miundo mbinu ya ulinzi, usalama,mawasiliano na mazagazaga mengine.
Anaweza kufanya kazi zake Chato au hata Tunduru katika mazingira ya kawaida kabisa lakini sio katika taharuki kama hii wiki NNE haupo ofisini?
US kule Camp David kuna kila kitu, lakini wao kama mkuu yuko kule anapumzika lolote likitokea basi anarudi haraka
Mkuu Chakaza, huku sasa ni kuingilia uhuru na faragha za rais na mengine ni kuingilia usalama wa taifa na usalama wa nchi, mtu wa kawaida hatakiwi kujua Ikulu ya Magogoni na Ikulu ya Chamwino kuna nini ambacho hakipo Ikulu ya Chato, asa long as rais wetu Magufuli yuko Chato na kazi zote zinaendelea kama kawaida ikiwemo kuweza kufanya kikao cha ulinzi na usalama, then mwache rais wetu akae mahali tulivu na mahali salama for as long as it takes!. Hayo mengine ya usalama, vifaa na mazagazaga mengine, waachie wenyewe!.
P
 
Uzi bora wa pili kabisa juu ya corona na hatua serikali inaact baada ya ule wa mkuu barafu.
Ubarikiwe mkuu.
Katika hotuba aliyoitoa Rais wetu hivi karibuni kule Chato, kuna mambo kadhaa ambayo yanatuonesha kwamba hali ya nchi kwa sasa ni tete:

1) Kwamba Rais yuko Chato kwa muda mrefu sasa
kwa kawaida Rais wetu Magufuli huenda Chato kwa mapumziko. hivi sasa ni muda umepita tunaona Rais yupo Chato. Corona ilipoanza kuchanganya, Rais wetu aliondoka Dar na kubanisha pale Dodoma, makao makuu. tulishuhudia Rais wetu akifanya MEDITATION kwenye majabali.

Naona baadaye akaona hiatoshi, akaamua kwenda mbali zaidi na hii Corona. na sasa tumeshuhudia akitoa Major Speech yake kutoka Chato. pia ni vema kukumbuka kwamba Rais wetu huwa ni mwoga sana wa majanga. amekuwa na kawaida ya kujitenga mbali na majanga, na kumwachia PM wake. hali kwa sasa ndio hiyo hiyo. Kamanda mkuu kaingia mitini. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

2) Hotuba inayochanganya
Katika hotuba aliyotoa, badala ya kutoa mwanga katika mapambano na Corona, imeleta giza. badala ya kutia matumaini, imeleta hofu zaidi. siyo ajabu sekeseke la Amana lilifuatia mara moja. Hotuba yake inaonesha anatumia zaidi uelewa wake na hisia zake, badala ya kutoa msimamo kutokana na sayansi ya kisasa kabisa, utafiti mpana, mjadala makini na wasaidizi wake, ushauri mpana na makini, na tafakari iliyo pevu. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

3) Anaongea na wakuu wa vyombo vya usalama
Rais Magufuli siku zote anapenda sana majeshi. akikwama popote pale anaita majeshi, na ni zaidi ya Rais yeyote aliyemtangulia. akikwama ujenzi, Jeshi. akikwama madaraja, Jeshi. na hata katika lile JANGA ALILOCHUMA MWENYEWE, JANGA LA KOROSHO, aliita jeshi. Katika kipindi hiki alichochanganyikiwa kabisa, aliona badala ya kuita maprofesa wa tiba na wataalamu wa magonjwa, wizara ya afya na wizara zingine, au hata Task force aliyounda mwenyewe kupambana na Corona, aliita wakuu wa vyombo vya usalama, majeshi.

Na kama alivyoita wanajeshi ili ikiwezekana wabangue korosho kwa buti, kasema wazi kabisa kwamba anataka kutumia jeshi kupambana na korona. na kweli, IGP akatafakari atafanya nini hapa kwa kutumia upolisi wake, akaamua kufanya kile ambacho wengi walishasema siku nyingi. kuzuia raia wa kutoka nje. sasa tunasubiri CDF Mabeyo yeye atafanya nini , atoe amri wanajeshi waitandike buti Corona? Au yule wa Magereza aitie gerezani Corona? Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.

4) Visingizio vya ajabu
Labda katika hali inayoonesha kukwama zaidi, Rais ametoa visingizio. Badala ya kufuata njia sahihi za kukabiliana na Corona, aliamua kuziba masikio na kupokea sifa kutoka kwa wale waliomuona kwamba ni shujaa pale mwanzo.

sasa vifo vinaongezeka kwa kasi, analaumu dawa za kupulizia, analaumu kwamba pengine amehujumiwa kwa kuletewa Barakoa zenye virusi vya Corona! Huyu ni mtu asiyetaka kubeba lawama begani na kujisahihisha. kukubali na kukiri alikosea, na kusonga mbele. Hiyo ni dalili ya kukwama. A desperate president. Clutching at straws.
 
Bahati nzuri hii Corona itatuunganisha maana haichagui CCM wala CHADEMA [emoji1787]
 
Mkuu Chakaza, huku sasa ni kuingilia uhuru na faragha za rais na mengine ni kuingilia usalama wa taifa na usalama wa nchi, mtu wa kawaida hatakiwi kujua Ikulu ya Magogoni na Ikulu ya Chamwino kuna nini ambacho hakipo Ikulu ya Chato, asa long as rais wetu Magufuli yuko Chato na kazi zote zinaendelea kama kawaida ikiwemo kuweza kufanya kikao cha ulinzi na usalama, then mwache rais wetu akae mahali tulivu na mahali salama for as long as it takes!. Hayo mengine ya usalama, vifaa na mazagazaga mengine, waachie wenyewe!.
P
Kuna kitu kinaitwa kubali yaishe. Nakubali, lakini kiu haijaisha.
Nitalianzisha tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu kinaitwa kubali yaishe. Nakubali, lakini kiu haijaisha.
Nitalianzisha tena.
Mkuu Chakaza, kukubali yaishe ni very healthy kwenye mjadala wowote, na kukitokea mabishano yoyote marefu, mnafikia suluhisho la kukubaliana kutokukubaliana, tunasonga mbele.

Siku ukipata facts za ziada, unaliamsha tena.
Mfano kama kwako Ikulu ni wale tausi, then utataka tupeleke tausi Chato, wakapelekwa na wote wakafa, unaweza kuliamsha kuwa Chato hapafai kuwa Ikulu kwasababu Ikulu ni tausj, tausi hawezi ku survive Chato, then Chato hapafai kuwa Ikulu.
P
 
Hakika umenena
Sasa mbona tunaambiwa Rais ni wetu? Kwanini kama ni wetu tusihoji mambo yake tukiyahoji tupewe jibu na Pascal kuwa hayo sio yetu tuwaachie wenyewe? Wenyewe kina nani ambao Rais ni wao?
Hebu tuwe wakweli, tokea aingie madarakani nchi hii imewahi kupita katika mapambano (vita) hatari yeyote kama hii? Kwa nini vita hatari kama hii ambayo yaweza kusambaratisha maisha ya watanzania na uchumi wao HQ ya mapambano ihamie Chato Nyumbani? Kwa sababu katika hali hii anahitaji kuonana na kujadiliana na kiongozi wenzake, wataalamu wa Afya na uchumi kila siku jee lawezekana hilo?
Kujidanganya sio jambo zuri, kama anatatizo la afya na anaogopa maambukizi ajiengue au tuambiwe. Kwa ni maambukizi ya kiingia pale alipo atakimbia na kwenda wapi tena? Madagascar kuliko gunduliwa chanjo asili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu acha kutoa taarifa hizo za vifo tafadhali. Siyo kazi yako. Wapo watu maalumu wenye mamlaka ya kutangaza vifo vya ugonjwa huu. Hao ndio wenye taarifa sahihi. Chonde chonde acha hii tabia, siyo nzuri na siyo utaratibu uliowekwa na mamlaka husika. Tuzingatie hilo jamani.
Tulia dawa iwaingie. Mlifikiri mko zama za Nyerere kuna TV moja tu ikulu. Kipindi hiki hamdanganyi mtu
 
Tujikinge na covid 19,tufuate maelekezo tunayopewa na wataalamu wa afya.
 
Mkuu Chakaza, lets don't assume and insinuates anything!. Mkuu wetu yuko kwao Chato kwa mapumziko, na baada ya mapumziko anaendelea na kazi akiwa Ikulu ya Chato akiendelea kupiga kazi kama kawaida, hayo mengine sii yetu, waachie wenyewe!.
P
Raia wanayo haki kumjadili rais wao. Hata zamani, mtemi akiugua, wazazi wenye mabinti wazuri wanawaondoa nyumbani kuwapeleka ugeni mbali. Mtemi akifariki, sharti azikwe ameshikiliwa na binti mzuri.

Rais ni public property
 
Ukiona MTU mkali mkali sana kwakutumia nafasi yake (majeshi yake) na kujisema kuwa yeye ningangari mara nyingi huwa ni muoga!!
Mtu anaogopa kupanda ndege, anaogopa haendi misibani, majanga anatanguliza wengine nasasa korona anacharu kujifichamo kijjni... Hizi hazifai kuwa sifa za amir jeda mkulu
Umenena mkuu!
 
Yes rais Magufuli ni wetu, ila kuna vitu vyake ni public, sisi wote tuna ruhusa kuvijua ikiwemo alipozaliwa, wazazi, kabila, elimu, marital status na family issues, na akiugua ugonjwa public pia tunapaswa kujua.

Kuna vitu ni private, hatupaswi kujua, hivyo ni kuingilia his right to privacy na kuna vitu ni Confidential vinalindwa na the clauses of confidentiality, maadam tumemuona rais yuko Chato ni kwao, yuko kule mapumzikoni, ila kama ilivyo status ya urais ina two sides, upande mmoja ni human side, rais ni human being, ni binaadamu kama binaadam wengine hivyo akiwa mapumzikoni kwao Chato anakuwa ni binaadamu anayehitaji mapumziko na Chato japo ni nyumbani, pia Chato ni sehemu tulivu, hata mimi nimefika na nina ifahamu, kuna hadi traffic lights, barabarani yanatembea magari ya punda, hayana kelele kabisa!, kwa vile ni kwake na ni kutulivu, rais wetu anatakiwa upumzike kwa amani na utulivu mahali tulivu na salama salmini.

Upande wa pili wa rais, ni Taasisi, presidential institution, hii Taasisi sio human ni Taasisi takatifu, haipumziki, haili wala hailali, hivyo akiwa Chato japo ni nyumbani kwa rais, lakini pia ni Ikulu kwa ile Taasisi ya urais, kazi zote za urais ikiwemo kuendesha nchi, zinaendelea kama kawaida na kila kinachofanyika Ikulu ya Magogoni, au ya Chamwino, kinaweza kufanyika Ikulu ya Chato, au kama kwako Ikulu ni wale ndege tausi na wale wanyama, tunaweza kuwaleta Chato, au hata kama kwako Ikulu ni yale majabali ya Chamwino ili umuone Magufuli akilala juu ya mawe, Chato tunaweza kuyapeleka, lakini kama ni rais Magufuli kuchapa kazi akiwa Chato, mbona anachapa kazi kama kawaida?, sasa why lazima Magogoni au Chamwino?.
P
Rais anaweza kufanya kazi zake hata akiwa safarini. Lakini zaidi Rais wa Marekani yuko better equipped akiwa kwenye Air Force One. Inakuwaje basi kama kuna tukio kubwa, marais wa Marekani na wengine hurejea ofisini? Ni muhimu sana rais kuwa in control na pia aonekane yuko in control
 
Back
Top Bottom